UJUMBE WA LEO
8/2/2015
KOMBOA NDOTO ZAKO
Nini maana ya ndoto?
Ndoto ni hali fulani inayokuja kwa mtu akiwa amelala
usingizi yaani viungo vyote vya mwili
vinakuwa havina ushirikiano.
Tafsiri ya pili
Ndoto ni malengo au matarajio anayokuwa nayo mtu na wakati huo
huo anakuwa ana akili timamu yaani akiwa macho hajalala usingizi, vilevile ni
mipango ya mtu.
Wakristo wengi wana ndoto lakini wameshindwa kuzifikia ndoto zao, kwasababu wameyakataa
maarifa ya Neno la Mungu.
(Jambo hili ni la kuwa nalo makini sana jinsi ninavyopwaya
katika Neno ndivyo nitakavyopwaya katika mafanikio, kwahiyo lazima niweke bidii
katika kutafuta maarifa ya Neno la Mungu)
Mithali 1:25-33.
(Nikipwaya kwenye Neno udhaifu nilio nao utanidhalilisha,
hii yote inatokana na kukosa ufahamu wa Kimungu).
Chanzo cha ndoto zangu nilizo nazo kupoteza mwelekeo ni pale
ambapo ninaukataa ufahamu wa Neno la Mungu.
Ninapoukataa ufahamu wa Neno
la Mungu maana yake nimeukataa mwonngozo wa Roho Mtakatifu, vilevile
nisipotoa muda wa kusoma Biblia kwa siku maana yake moyo wangu sijautendea haki ya kuzungumza na Roho Mtakatifu.
Nikisoma Biblia ninapata nguvu ya rohoni , kwahiyo ni rahisi ndoto nilizo nazo zikatimia bila kuathiriwa na adui.
Sababu kuu ya kutokusikiwa na Bwana wakati wa maombi
inatokana na mimi kwa kutokujiwekea utaratibu wa kuyaishi Maandiko Matakatifu.
Ndoto zangu zitatimia iwapo nitafanya mambo makuu mawili:-
1)Nikiruhusu hali ya kuwepo kwenye uwepo wa Mungu mara kwa
mara.
2)Nikiruhusu hali ya kujisomea Neno la Mungu wakati wowote lakini isipite siku
sijasoma.
Katika haya mambo mawili yatasababisha kibali cha Kimungu
kuyavaa maisha yangu, kwahiyo nafasi ya upendeleo itakuwepo tu hata iweje.
Nikiweka mikakati ya usomaji wa Biblia na usikilizaji wa
Neno la Mungu ,kwa maana zaidi kutokuruhusu hali ya kukosa kwenye uwepo wa
Mungu ndoto zangu nitakuwa nimeziokoa.
Ikiwa nina ndoto na ninajifahamu kwamba nina ndoto za
siku zijazo inatakiwa niziatamie ndoto
hizo ndipo zitapata wepesi wa kutimia.
Ndoto niliyo nayo itatimia iwapo maarifa ya Biblia yataniongoza,
maarifa ya Biblia (Neno la Mungu) ,ndiyo yanayoshinikiza imani ya mtu kufika
kile kiwango cha kuamuru jambo na likatimia.
NAMNA YA KUSIMAMIA
NDOTO ZANGU
Ili niweze kutambua ni namna gani ya kuzisimamia ndoto zangu
inatakiwa nijifunze kwa walionitangulia ambao ninawasoma kwenye Maandiko Matakatifu (Biblia).
Mfano mzuri ambao tunaweza kuutumia ukatusaidia tunaupata
kwa Yusufu Mwanzo 37:5-----.
Upofu wa kiroho mara nyingi husababisha ndoto za mtu
kutotimia , mara nyingi hii inatokana na
mwamini kushindwa kupambanua pale ambapo Mungu anasema naye.
Watu wengi ndoto zao zimeathiriwa kwasababu wanashindwa wao kama wao kusimama
kuziatamia bali wanashirikisha watu wengine wasiokuwa na maharifa nayo,
kinachotokea ni nini , hiushia katika kukatishwa tamaa na kuvunjwa moyo , ndiyo
maana Mungu akasema kupitia Ezekieli 2:1.
Mungu anazungumza na mkristo ambaye ameamua maisha yake kuwa
chini ya mwongozo wa Neno lake.
Wakristo wengi wasiposimama vizuri katika Maandiko
Matakatifu, yaani katika kulisikiliza Neno la Mungu kwa undani mwisho wa siku
watazikuta ndoto zao zimezimika .
Ndoto za wakristo zinazimika kwasababu asilimia kubwa ya
waamini hawana msimamo katika suala zima la kumcha Mungu.
Mwamini mwenye uwezo wa kumsikia Mungu akisema huyo ana
uwezo wa kuatamia ndoto zake mpaka zikatimia.
Kama simsikii Mungu akisema na mimi uwezo wa kuatamia ndoto
zangu ni mdogo mno. Kwasababu ili ndoto za mwamini zitimie zinahitaji mwongozo
wa Neno la Mungu.
Hii inasikitisha sana ndoto za waamini wengi zimeishia njiani yaani hazijatimia hii
imetokana na waamini kushindwa kuziatamia ndoto zao kupitia Neno la Mungu.
Neno la Mungu peke yake ndio lina uwezo wa kusababisha ndoto
za mtu zikatimia.
Katika Mwanzo 37:11b
pale anaposema ‘baba alilihifadhi neno
hili’’, ni ufahamu kwangu leo kwamba kila nitakayoiota ninahitajika kuandika
yaani kuweka kumbukumbu mpaka siku itakapotimia.
Kila jambo linalotokea kwenye maisha yangu ukweli ni kwamba Mungu alishanieleza kwenye
ndoto shida inakuja kwamba kushindwa kupambanua vilevile kutokukumbuka, ndio
maana inatakiwa kila ndoto niiandike kwa kumbukumbu siku za usoni.
JINSI YA KUZILINDA
NDOTO ZANGU ZISIATHIRIWE
Ili niweze kuzilinda ndoto zangu zisiathiriwe inatakiwa
niikuze mamlaka italazimisha hali ya
utiisho katika kila roho inayopambana na mimi, ndio maana Biblia ikazungumza Isaya 54:17.
Silaha ya shetani inakosa nguvu kwa mwamini mwenye mamlaka
ya Neno la Mungu ndani mwake.
Hali ya kushindwa kwa mwamini inatokana na mamlaka aliyonayo
imeshapoa yaani imepoteza uwezo.
Mwamini aliyepoteza mamlaka sanasana hukumbukwa na mambo
yafuatayo:-
i)
Hana kabisa ulinzi wa Mungu juu yake, ndio maana
waweza kuwa kituo cha magonjwa , kwahiyo katika hili huwa tunapata matokeo ya mwamini kudhoofika kiafya.
ii)
Asili ya
udhaifu alionayo kwenye mwili wake huwa inainuka , sasa basi hapa inategemea ni
udhaifu gani alionao Mfano:Muongo,
Mzinzi, Mlevi, Tapeli, na mengine mengi yanayofanana na haya.
iii)
Shetani
humwibia ufahamu wa kile anachosikia kuhusu Mungu, vilevile utayari wa kukaa
chini kufundishwa, ndio maana inaweza
ikatokea mwamini asije kanisani asiwe na kazi maalumu hiyo yote inatokana
kashaibiwa ufahamu.
iv)
Maisha yake hufanywa jalala la kila matatizo.
Ndoto za mwamini
zinalindwa kutokana na jinsi mwamini anavyozidi kukua kiroho yaani kuongezeka
zaidi kimaarifa, maarifa ndani ya mtu yakiongezeka kina cha ufahamu wa rohoni hufunguka na mtu
huyo mbekle za uwepo wa Mungu huitwa mtu wa imani.
Silaha itakayoweza kuyalinda maisha ya mkristo ni ile roho
ya kupambanua itakayoyavaa maisha yake.
ANGALIZO :Nikiwa
ni mkristo mwamini na wakati huohuo sina uwezo wa kupambanua ni vigumu
kuvishinda vita vya kiroho , ndani ya kupambanua ndipo tunapopata ufahamu wa
kujua sauti ya Mungu ni ipi na sauti ya roho zidanganyazo ni zipi, tofauti na
hapo hutoki kwenye mtego.
Kutimia kwa ndoto za mwamini kutokana nay eye anavyoongezeka
kiukaribu kati ya yeye na Mungu.
NINI KIFANYIKE ILI
NDOTO ZANGU ZIZAE MATUNDA:
Ili ndoto zangu ziweze kuzaa matunda haitakiwi nitoke nje ya
kanuni za Neno la Mungu, hata inapotokea nimekosea inatakiwa nijirudi haraka
ili nisitoke nje ya ule mfumo wa Baraka za Mungu, ndio maana Yoshua alipewa
maagizo katika Yoshua 1:7,8.
Jambo hili ni la kuwa nalo makini sana
Shetani anapitia katika lile jambo ninalolipenfda kuyaathiri
maisha yangu.
Ili niweze kuidhibiti hali
hiyoiliyozungumzwa kwenye point ya juu inatakiwa ufahamu wangu
niulazimishe kumheshimu Mungu ndipo nitakapopata uwezo wa kuyatambua mapenzi ya
adui kabla hajaniumiza.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni