Jumapili, 1 Februari 2015

NAMNA YA KUDHIBITI UDHAIFU NILIONAO

UJUMBE WA LEO
01/2/2015
NAMNA YA KUDHIBITI UDHAIFU NILIONAO
Kwanza kabisa kila mwanadamu mwenye mwili anao udhaifu ndani mwake,lakini udhaifu huu huwa unatofautiana kila mmoja kwa jinsi yake .

Udhaifu ni hali fulani  ndani ya mtu vilevile ni mapungufu anayokuwa nayo mtu, wakati huohuo akiwa ana taarifa hiyo ndani mwake, kwa maana zaidi ni roho anayopagawa nayo akiwa na akili timamu.


Udhaifu ni hali ambayo inaweza kuepukika iwapo mwamini ameamua kufanya mabadiliko .

Udhaifu ni hali ambayo inaweza kuwa kipingamizi cha maombi ya mwamini ,vilevile kizuizi cha kufanya majibu ya maombi ya mtu kuchelewa.

Bila kudhibiti udhaifu nilio nao ni vigumu kupata mpenyo, kwasababu udhaifu huo unakuwa ni kibao kinachosimama mbele za Mungu na kunishitaki .
Zaburi  51:3.

Waamini walio wengi wana bidii ya kumjua Mungu lakini hawana bidii ya kupambana  na madhaifu ambayo ndio kikwazo kinachozuia wasimjue Mungu ingawa wanamtafuta usiku na mchana .

(Udhaifu ni kipingamizi kinachoyafanya maombi ya mtu kutokujibiwa kwa wakati, kwasababu katika mahakama ya kiroho mwamini anapoanza kuomba kitu kitu cha kwanza katika mahakama hiyo  kinachotazamwa ni  mwenendo  wake, kwahiyo mwenendo wako kwenye mahakama ya kiroho ndio ushahidi wa wewe kujibiwa au maombi yako kuzuiliwa).

Mfano mzuri ni ni katika mahakama ya kidunia ;Hakimu  hawezi kuhukumu kesi bila ushahidi anaouthibitisha  taarifa nzima  ya mashatakiwa
Yakobo 2:23-26.

Mimi kama mwamini inatakiwa imani niliyonayo kwa Mungu niiweke katika mazingira ya matendo ,kwasababu yale matendo ndio ushahidi wangu mimi kwenye mahakama ya kiroho kwamba ninastahili kubarikiwa  au sistahili kubarikiwa.

Kwenye mahakama ya kiroho ili nibarikiwe au nisibarikiwe ni unatazamwa ule mwenendo  wangu wa kila siku,kwahiyo nikikutwa mwenendo wangu unaendana sambamba na imani yangu mbingu inanibariki, ndio maana Biblia ikasema iamni pasipo matendo imekufa.

Udhaifu nilio nao lazima nijilazimishe  mimi binafsi kupingana nao ndipo hali ya mabadiliko itakapoanza kujitokeza.

Nikishapata ufahamu ya kwamba udhaifu nilio nao ni kipingamizi cha maombi yangu yasijibiwe ndio mwanzo wa kuanza mikakati ya kupindua utawala wa udhaifu huo ndani mwangu.

Kitendo cha mtu kutambua chanzo cha shida yake, hapo huwa ndio mwanzo wa mtu kuingia katika hatua ya kushinda hali hiyo.

Kama udhaifu nilionao na hapohapo  ninajitambua kwamba ninao, Basi hata kuushinda inawezekana .
Wakristo wengi sanasana jamii ya waaminio wamepoteza Baraka zao kwenye uwepo wa Mungu,kwasababu kuu mbili:-
A)Kukata tamaa , kukata tama inafunua wazi moyo wangu kwenye uso wa Mungu kwamba mimi ni mvivu wa kusibiria , kwahiyo hata siku moja mtu wa hivyio maisha yake huwa hayana mpenyo vilevile kibali mahali popote.

(Mtu mwenye hali ya kusuburia  ndani mwake ana upendo ulio hai, kwa lugha nyingine  ana imani yenye matendo).

Kama ilivyo mwili pasipo roho umekufa basi, ndivyo ilivyo imani bila uvumilivu haizai matunda

B)Kushindwa kuamini kwamba alilolinena Mungu ni kweli
Jamii nyingi ya waaminio maisha yao yamekwama na sababu kuu ya maisha yao kukwama  wamekosa uvumilivu wa kusubiri ahadi za Mungu.

Mfano Mungu akisema atanibariki badala ya mimi kuweka maandalizi thabiti ya kumiliki Baraka zile ninaanza kunung’unika, kwahiyo ni vigumu katika nafasi hiyo kubarikiwa.

HATUA YA KWANZA YA KUDHIBITI UDHAIFU
Ili niweze kudhibiti udhaifu nilionao inatakiwa niuimarishe ufahamu wangu katika Neno la Mungu.
Kwanini inatakiwa niimarishe ufahamu wangu ,ni kwasababu ufahamu ndio unaopokea taarifa zote za moyo wangu
2Wakorintho 10 :3-5.

Bila mimi kuimarisha ufahamu wangu katika Neno la Mungu itakuwa ngumu kumiliki Baraka za kiroho ambazo ndizo  huyafanya maisha yangu ya kimwili kuheshimika.

Mkristo  mwamini akiimarisha  ufahamu   wake katika Neno la Mungu huwa ana mambo matatu:-
A)Mamlaka ya kuumba
B)Nguvu ya Rohoni
C)Upendo.

A)UFAFANUZI KUHUSIANA NA MAMLAKA KWA UFUPI
Mamlaka ni hali Fulani ya nguvu ya Mungu inayoyavaa maisha ya mtu aliyeimarisha ufahamu wake vizuri katika Neno la Mungu,vilevile ni uwezo anaoupata mtu kutoka katika serikali ya mbinguni kupitia Maandiko Matakatifu a,mbyo ndio katiba ya kiroho, lakini katiba hii hainaga mapinduzi.

(Katiba ya kiroho ni Neno la Mungu (Biblia).

Hiki kitu ni cha kuwa nacho makini sanan majivuno yanaathiri mfumo wa ufahamu sana , kwahiyo ili niweze kuepuka hilo inatakiwa niwe mtu wa kutaka kujua kitu kila siku kutoka kwenye Neno la Mungu, hapo nitakuwa nimeuokoa ufahamu wangu, ndio maana katika kitabu cha Yakobo amesema neno hili
Yakobo 4:13-17.

Kukuza ufahamu wangu kwa kusoma Maandiko Matakatifu ni jambo la muhimu sana , kwasababu hatua za kuyaishi maisha Matakatifu,Maisha ya Baraka, Maisha yenye faida kwa Bwana, zinaanzia pale ambapo ufahamu wangu umepevuka.,Jambo hili lilimkuta Mtumishi wa Mungu Danieli,
  ufahamu wake ulipevuka kwa kusoma vitabu ,akatambua nyakati amabzo Neno la Mungu lilinjia Yeremia NabiiDanieli 9:1-3.

Ufahamu wangu utaongezeka kadri nitavyotia bidii ya kusoma Maandiko Matakatifu.

Ili nikue kiufahamu na nizae matunda yaliyo bora inatakiwa nijifunze kwa Yesu Kristo.

Nikiukuza ufahamu wangu   kupitia Maandiko Matakatifu kumbukumbu yoyote ya dhambi  ambayo tayari nimekwisha itubu kwenye uso wa Mungu itafutika na hapo kutazaliwa hatua zaidi za kuimarika  kiroho.

Kumbukumbu ya mambo yaliyopita kwenye maisha ya mwamini mara nyingi huwa inaathiri ukuaji wa ufahamu wa amkristo, kwasababu kitendo cha kukumbuka jambo  ambalo Mungu amekwisha kunisamehe na nimekwisha kulitubia ninamfanya Mungu  kuonekana muongo, ndio maana  akatoa tahadhari kupitia kitabu cha Isaya 43:18.

(Nikiona nimeanza kuona aibu juu ya jambo lolote ninalomkosea Mungu au dhambi  ninayoifanya kwa siri nijue wazi maisha yangu Mungu ameshaingilia kati , kwahiyo inatakiwa nitie bidii kuudhuria ibada na wakati huo huo nikitarajia mabadiliko).

Nikiyang’ang’ania mambo yaliyopita na  kuyarejesha  kwenye ufahamu wangu kuendelea kuyawazawaza ninaonyesha jinsi nilivyo mchanga kiroho, kwahiyo ni vigumu sana mtu wa aina hiyo kuzishiriki Baraka za Mungu.Udhaifu wowote ulioko juu ya maisha ya mtu  ataushinda pale atakapo amua kusoma Maandiko Matakatifu, vilevile na vitabu ,mbalimbali  vilivyoandikwa na Watumishi wa Mungu wenye nguvu, hata Danieli Biblia alitambua  nyakati za Neno la Bwana lilivyomjia Nabii Yeremia kwa kusoma vitabu, hii inaonyesha ni Maandiko Matakatifu vilevile ni vitabu vilivyoandikwa na manabii waliopita.

B)UFAFANUZI MDOGO KUHUSIANA NA KIPENGELE ‘B’ NGUVU  YA ROHONI.
Nguvu ya rohoni inayavaa maisha ya mwamini pale ambapo mwamini huyo ameamua kusoma Biblia, vilevile kusikiliza Neno la Mungu.

Nguvu ya rohoni ni jambo la muhimu sana sanasana katika maisha ya jamii ya waaminio , kwasababu mapambano au vita vya waamini na shetania hufanyika katika roho, kwahiyo kuvishinda vita hivyo  inatakiwa niwe  imara katika  nguvu ya rohoni, ndio maana Biblia ikasema katika kitabu cha  Waefeso 6:10-15.

Nivigumu kuushinda ulioko juu yangu kama sina uwezo wa kutawala katika roho,kwasababu nguvu ya udhaifu  inaanzia katika roho, ndio maana Kitabu cha Waefeso 6:12 kimesisitiza  kwamba vita vyetu ni vya kiroho.

Wakristo wengi wanashindwa na madhaifu yaliyowakalia kwasababu ya upungufu wa kina cha Neno la Mungu ndani yao, na upungufu huo huwa unaondoa kibali kwenye maisha ya mtu.

Kibali kikiondoka katika maisha ya mtu ataandamwa na mambo yafuatayo:-
i)Magonjwa
ii)Kukataliwa
iii)Kufilisika kiroho na kimwili
iv)Kuandamwa  kila baya hata kama hakuusika  atalazimishwa kahusika.

Kibali ndiyo mafanikio.



Maoni 1 :

Gerd Ulrich alisema ...

Maisha yangu Maajabu yanashangaza ushuhuda, Jinsi nimepata kisanduku chenye nguvu sana ambacho sasa ni pesa yangu mara mbili kutoka mia hadi elfu ya pesa ndani ya masaa 24, na pia jinsi nimerudisha mpenzi wangu wa zamani, sababu kuu niliwasiliana na Dk Lomi kwa msaada mimi kumrudisha mpenzi wangu wa zamani, basi ananisaidia ni nguvu kubwa ya kumrudisha mpenzi wangu wa zamani, na ananipenda na ananithamini sasa, basi mimi na Dr Lomi tukawa marafiki, baada ya mazungumzo kadhaa namuuliza ikiwa kuna njia anaweza kuniganga ili nipate pesa, hapo ndipo aliponiambia juu ya sanduku hili la uchawi, akaniambia kuna aina na saizi tofauti ya sanduku, aliniambia aina zote za sanduku, ningeweza kumudu ndogo tu ya sanduku, baada ya maombi muhimu anayofanya kwenye sanduku, ananipeleka kupitia huduma ya kujifungua, aliniambia niweke pesa ndani, niliweka ndani ya sanduku 100 euro baada ya masaa 24 nikagundua ilikuwa elfu 10 euro ndani, na nimekuwa nikitumia sanduku kwa miezi 7 sasa, mimi na mchumba wangu tunaishi maisha bora, ikiwa unahitaji b ack mpenzi wako au pesa spell wasiliana na Dr Lomi kwa barua pepe: lomiultimatetemple@gmail.com au WhatsApp namba +2349034287285 unaweza pia kumwandikia kupitia Jina la Mtumiaji la Snapchat: drlomi20 atakusaidia nje, asante kwa kusoma,

Kwaheri Gerd Ulrich