UJUMBE WA LEO
25/1/2015
JIMIMINE KWENYE NENO
SEHEMU YA TATU
II)UJASIRI
Ujasiri ndani mwangu utakuwepo pale ambapo moyo wangu
utaamini katika kile ninacho jiamini nacho.
Siku zote ujasiri unapotea juu ya kitu ambacho sina uhakika nacho.
(Shetani anatumia udhaifu
wetu wa hofu kuyaathiri maisha
yetu ,juu ya jambo hili lazima niwe makini)
(Mimi ninayelitumia
jina la Yesu Kristo sipaswi kuwa muoga kwenye uwanja wa mapambano ,kwasababu
kwenye uwanja wa mapambano kuna mambo makuu mawili
a)Kushinda
b)Kushindwa,kwahiyo hali yoyote nitakayoionyesha ninapokuwa kwenye uwanja wa mapambano ndio
matokeo nitakayoyapata)
Siku zote kinachotesa maisha ya waamini Mungu sawa lakini
hawana ujasiri wa kukabiliana na
changamoto katika uwanja wa mapambano ,ndio maana hupata matokeo kimyume na vile
wanavyoamini ,hata Biblia imeyathibitisha 1Yohana
4:18.
(Hofu ikitanda kwenye moyo wangu hata kile ninachokiamini
kitayeyuka).
Kuna silaha moja kuu na hii ndio itakayoweza kutupa ushindi
kwenye uwanja wa mapambano na silaha
hiyo ni upendo , kwasababu ndani ya upendo tunapata mambo kadha wa kadha :-
i)Tunapata msamaha Warumi
12:19-21
ii)Tunapata Imani Waebrania
11:1,6,8,11 na 17
iii)Tunapata uvumilivu
Mathayo 10:22
iv)Ujasiri 1Yohana
4:17.
Silaha ya kushinda vita vya kiroho ni upendo,cha ajabu neno
upendo huwa hawaoni ni kitu cha maana kwenye maisha yao.
Mwamini ambaye hasamehi huyo haishi na Mungu.
Maisha ya visasi ndiyo yanayowafanya wakristo waamini
kushindwa kwenye uwanja wa mapambano, kwasababu katika visasi hamna upendo vilevile hamna imani.
ANGALIZO:Lazima
nitambue maisha ya visasi , kutokusamehe,hofu,woga,wasiwasi,mashaka hayana Baraka
kwa Bwana ,kwahiyo nahitaji mabadiliko haraka sana.
Kama sina uvumilivu katika imani yangu siku zote nitakuwa
mtu wa kushindwa.
Uvumilivu ndio unaoimarisha misuli ya ujasiri kwenye imani
ya mwamini kwahiyo ili niwe mtu wa
kushinda popote pale ninapokutana na changamoto
inatakiwa niboreshe zaidi mambo
yafuatayo katika maisha yangu :-
a)Mahusiano na Neno la Mungu (Biblia)hapa ndipo chimbuko la
utawala katika roho linapoanzia.
Inatakiwa niyaishi maneno ya Mungu yaani niyatendee kazi
maandiko ninayoyasikiliza kila siku kanisani , ndipo neno la Kinabii ninalotabiriwa na Mtumishi wa Mungulitatimia
juu yangu.
(Wokovu ndiyo mpango wa Mungu kwa wanadamu wote wenye mwili).
1Yohana 4:17 ni
picha wazi ya kwamba Yesu Kristo aliyaishi maisha ya utakatifu humuhumu ulimwenguni,kwahiyo nikitaka niyaishi maisha
aliyoyaishi Yesu Kristo inatakiwa
niboreshe mahusiano yangu na Neno la Mungu
ndipo nitakapoweza kuyatimiza yaliyoandikwa humo.
Mahusiano yangu na Neno la Mungu yataniponya sehemu
zifuatazo:-
1)Nitaponywa Ufahamu
2)Nitaponywa Akili
3)Nitaponywa Moyo , na hiki ndio kiungo kikuu sana kinacholeta madhara hata Biblia
imeyathibitisha haya Yeremia 17:9.
Mwenye uwezo wa kuutawala moyo wake ni Yule anayesoma Biblia kupita kiasi.
Ili utumishi wangu usilaumiwe inatakiwa nitie juhudi
nyingi katika usomaji wa Biblia
,kwasababu usomaji wa Biblia utanisaidia kina cha maarifa ya rohoni kufunguka ,
kwahiyo hapa ndipo nitakapopata ufahamu
wa kupambanua ndani mwangu neno
lolote ninalolisikia ndani mwangu kabla ya kulitamka.
Kila neno ninaliolitoa katika kinywa changu inatakiwa
lihakikishwe na Neno la Mungu ambalo tayari nimeshaliamini moyoni mwangu ili nisiwe kikwazo kwa
wanaolisikia bali liwe msaada, kwahiyo
kinywa changu kitaitwa kinywa chenye hekima
sambamba na Maandiko Mtakatifu
katika kitabu cha Malaki 2:7.
Kile ninachokitoa kwenye kinywa changu ndicho kipimo cha
imani niliyonayo ,kwahiyo nikilitambua
hilo inatakiwa niwe na bidii sana kwenye kusoma Biblia ili kuongeza maarifa
zaidi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni