Jumapili, 18 Januari 2015

JIMIMINE KWENYE NENO SEHEMU YA PILI

UJUMBE WA LEO
18/1/2015
JIMIMINE KWENYE NENO        SEHEMU YA PILI
HASARA ZA KUTOKUJIMIMINA KWENYE NENO LA MUNGU
Kutokujimimina kwenye Neno la Mungu maana yake ni  kutokuupa moyo wangu uhuru wa kuambatana na Neno la Mungu .


Mkristo mwamini jinsi anavyounyima moyo uhuru wa kufundishwa Neno la Mungu ndivyo  anavyozidi  kujiathiri katika maeneo muhimu  yafuatayo katika maisha  yake :-
i)Afya njema
ii)Uchumi
iii)Mahusiano  na Jamii
iv)Ndoa. ,haya ndiyo maeneo muhimu sana katika maisha ya mwanadamu yatakasyoathirika  pale ambapo mwanadamu huyu atakataa  kuongozwa na ufahamu wa Neno la Mungu.

Mkristo mwamini akiruhusu maisha yake yaongozwe na ufahamu wa Neno la Mungu 
(Biblia)mawazo yake yataendana  sambamba na mawazo ya Mungu,kwahiyo mkristo huyu ndani mwake kutatoka mambo yafuatayo:-
i)Hekima
ii)Busara
iii)Nidhamu
iv)Utii,kwahiyo mtu wa aina hii anaitwa mkristo aliyeyalingana mapenzi ya Mungu.
Siku zote aliyeyalingana mapenzi ya Mungu kitokacho ndani mwake  ni msaada kwa jamii inayosikia ,ndiyo maana Biblia inatusisitiza sana kuimarika katika imani  na pia imenena kitu kwa mtu anayeishi katika misingi ya kiimani,mbona hata Biblia imeyafunua haya katika kitabu cha Warumi 1:17.

(Imani ndiyo inayonitengenezea mazingira ya mimi mwamini kupata kibali kwenye uwepo wa Mungu)

Ili roho ya Bwana isigeuke idumu na mimi siku zote inatakiwa nijijunganishe na Neno la Mungu (Biblia).

Hasara nyingine inayoweza kutokana na kutokujimimina  kwenye Neno  ni hali ya kuvamiwa katika roho ,hali hii ya kuvamiwa katika mazingira ya ndoto, vilevile magonjwa mengi yanayowatesa jamii ya waaminio huanzia katika ndoto.

MFANO:Ninaota nakula nyama mbichi ,nisipofunguliwa  mapema kutatokea vidonda vya tumbo ,uvimbe tumboni.

Ili niweze kushinda mfumo wa ndoto  za kishetani katika roho inatakiwa nifanye mambo yafuatayo:-
i)Kabla ya kulala inatakiwa noisome kwanza Biblia

MAELEZO KUHUSIANA NA SENTENSI HAPO JUU
Nikisoma Biblia kabla ya kulala ninakuwa nimejiunganisha moja kwa moja na sauti ya Roho Mtakatifu,kwahiyo taarifa zote  nitakazozipata au kwa lugha ya kawaida ndoto itakuwa inahusiana namambo haya kwenye maisha yangu:-
i)Itanipa mwongozo wa maisha ya leo baada ya kuamka usingizini

MFANO: 1
Nimepanga kwenda kazini asubuhi lakini usiku nimeota nimegombana na mfanyakazi mwenzangu  ,maana yake haitakiwi niende kazini siku hiyo,kwasababu nitakapoenda kazinikuna hatari ya ugomvi kutokea na kazi ikawa ndio mwisho siku hiyo.

MFANO :2
Nimeota ndoto jirani yangu amepata ajali lakini mimi ninampango wa kusafiri,maana yake ndoto hii ni tata,lazima niende kwa muonajianipe mwongozo juu ya hili.

NAMNA YA KUEPUKA HASARA ZA KIROHO ZINAZOWEZA KUNIATHIRI
Ili niweze kuepuka hasara  za kiroho zinazoweza kuniathiri inatakiwa niruhusu moyo wangu ,vilevile niulazimishe kufundishwa Biblia,kwasababu hasara za kiroho anazoweza kuzipata mtu mara nyingi zinasababishwa na upofu wa kiroho.

(Kufanikiwa  kwangu kunatokana na jinsi ninavyoongezeka  kiufahamu)

Yeremia 23:23,24

Mungu yupo katika mfumo wa namna mimi ninavyoamini,kwahiyo nikiongezeka katika kuamini ndivyo Mungu anavyoongeza Baraka zaidi,katika sentensi hii ni kuiruhusu akili ikubali.

Yeremia 23:23 inadhihirisha wazi uhalisia wa umbo la Mungu kwamba ni Roho.

Yohana 4:24

Neno ni Mungu anazungumza waziwazi na kanisa, ndio maana  tunashauriwa kusoma Biblia sana.

Ili niweze kupata ufahamu wa kutosha kwamba Neno ni Mungu anazungumza waziwazi  ni pale ambapo moyo wangu unakuwa umeghafirika, ninaposhika Bibliakusoma amani inarejea kwenye moyo ,kwanini kwasababu akili inakubali urejesho wangu uko ndani ya Neno la Mungu.

Mkristo aliyejiunganisha na uwepo wa Neno la Mungu ndani yake kuna mambo haya ni :-
I)                    Mamlaka, mamlaka hii ndiyo humtengenezea  mwamini mfumo  wa kijiamini sambamba na Neno la Mungu linavyosema katika Luka  10:19.

Mamlaka inazaaje mfumo wa kujiamini ndani ya mtu?
JIBU:Ni kwasababu akili ya mtuinatambua nafasi aliyonayo mtu, ndiyo maana moyo wake unaamini  nafasi hiyo hakuna mtu anayeweza akaipindua .

Kwanini mioyo ya wakristo inapoteza nguvu ya kuamini , ni kwasababu akili zao zinawashuhudia  matendo yao kwamba yako kinyume na kile wanachokiamini

3Yohana  1:1-4

Maisha ya wakristo yanakatishwa yaani wanakufa kabla ya wakati wa Bwana ,kwasababu wanajikwaa kwenye Neno la Mungu.

Kutokutambua Mungu yu karibu na mimi kunaathiri sana imani ya mtu kwenye eneo la kupokea Baraka kutoka kwa Mungu, nini kifanyike ? inatakiwa  nikisimamie kile ambacho nimekiamini na kukiri kwenye kinywa change mpaka kitoe matokeo,hapo nitaitwa mkristo aliyeokoka ,vilevile mkristo mwenye mamlaka .

Ili niweze kushinda vita vya kiroho inatakiwa moyo wangu ujengwe katika misingi ya kiimani si katika misingi ya kihisia ,kwasababu hisia ina tabia moja huja na kutoweka.

II)                  Ujasiri
Maelezo na ufafanuzi kuhusiana na Ujasiri.

Somo hili bado litaendelea  wiki ijayo………………

Hakuna maoni: