UJUMBE WA LEO
11/1/2015
JIMIMINE KWENYE NENO.
Kujimimina
kwenye Neno la Mungu kutanisaidia kunipa ufahamu wa rohoni ambao ndio
utakaonisaidia kuniunganisha na uwepo wa Mungu (Yesu Kristo).
Kuna hatari inayomkumba mtu sanasana jamii ya waaminio kupotoshwa nah ii mara nyingi inawakumba wakristo wavivu katika maeneo makuu mawili
i)Usomaji wa
Biblia
ii)Ufundishwaji
Biblia (Neno la Mungu).
Watu wengi
wamepotoshwa na hii inatokana na fahamu zao zao za kiroho kujifunga ,sentensi
hii inanitahadharisha mimi kama mwamini yakwamba kila linaloingia masikioni mwangu lazima nilipime
katika Neno.
Maisha ya
wakristo sansan jamii ya waaminio Baraka zao zimejifunga ,kwasababu wameruhusu
mioyo yao kubebeshwa laana ambazo hazikuwa nazo,Hii imetokana na wakristo wengi kukosa upeo wa ufahamu wa kupambanua
,ndio maana inatakiwa nisome sana Biblia ili niwe na asili moja na Mungu.
2Timotheo 4:1-8.
Mwamini
akilisikiliza Neno la Mungu na wakati huohuo ana upofu wa kiroho maisha yake
yana hatari kubwa ya kukosa mpenyo kwasababu moyo wake utapingana na kile ambacho masikio yake
yamesikia .
Nikiruhusu
moyo wangu kujimimina kwenye Neno la Mungu, nah ii ndio itakayo
nitengenezea mtiririko wa Baraka za
Mungukatika maisha yangu ,ndio maana katika kitabu cha Wakorintho kimesema wazi
1Wakorintho 6:17.
Ninaporuhusu
moyo wangu kukaa chini kulisikiliza Neno la Mungumaana yake ninatengeneza
muunganiko wa siri na Mungu ambao ndio utakaoleta hali ya urejesho wa kiimani.
(Magonjwa yanayowakumba
wakristo yaanza kwenye ndoto,ndio maana tunashauriwa kutia bidii katika usomaji
wa Biblia ,vilevile kuhudhuria kanisani).
Kujimimina
kwenye Neno la Mungu kutanisaidia kunizamisha kwenye maisha ya kweli ambayo
ndio Mungu anahitaji kila mwenye imani aishi.
Maisha ya
kweli ndio yanayompelekea mwamini kujibiwa maombi wakati wote anapohitaji
kwenye uso wa Mungu
2 Yohana 1: yote na 3Yohana 1:yote.
Mwamini
anayetembea klatika kweli ya Mungu maisha yake hayana ubaguzi kwa maana zaidi
atawabeba watu wote kama ndugu zake waliotoka katika tumbo moja.
Baraka za
watu zimejifunga kwasababu wanaishi maisha ya visasi na hila ndio maana
wamekosa mipenyo katika maisha.
Ili niwe
sambamba na Baraka za Mungu (Yesu Kristo) lazima niyalazimishe maisha yangu
yaendane na kweli ndipo karama za Kimungu zitajifunua kwngu dhahiri.
Suala la
kutembea katika kweli ni la mkristo aliyeamua kuikana nafsi yake kwaajili ya
Mungu.
Sisi ambao ni
jamii ya waaminio tunahitaji hekima sana ya kuishi na jamii ya
wasioamini,kwasababu jamii ya wasioamini wako makini sana kuchunguza mienendo
yetu ili watuhukumu nayo.
Ili niweze
kuwa na nguvu ya ushawishi katika jamii ya wasioamini inatakiwa mimi
kamamkristo nizame katika mambo makuu yafuatayo:-
i)Nisome
Biblia ,katika usomaji wa Biblianitapata kufahamu kwa undani maisha aliyoishi
Yesu Kristo na mienendo yake ,hapo itakuwa rahisi kwangu mimi kuanza kupambanua ni namna gani
ninatakiwa niishi kama mkristo niliyejaa imani.
Maeneo haya
yanathibitishwa na kitabu cha Yohana
14:1-30.
Katika kitabu
hiki cha Yohana 14Yesu alizungumza
na wanafunzi wake (kanisa) kabla ya kuuvua mwili wa damu na nyama.
Yohana 14:19 kwenye kipengele ambacho Yesu anasema ninyi mtakuwa hai
kama mimi nilivyo hai anadhihirisha
wazi kwa ulimwengu katika ile jamii iliyoandaliwa kuurithi ufalme wa Munguyakwamba
maisha ya Yesu Kristo wakati ameuvaa mwili aliishi katika haki na kweli,kwahiyo
mimi ili niwe sambamba na andiko hili inatakiwa
niyazamishe maisha yangu katika kweli ndipo Baraka za Mungu vilevile
kuurithi ufalme wa Mungu utakavyokuwa
sehemu yangu.
B. FAIDA ZA KUJIMIMINA KWENYE NENO LA
MUNGU
Zipo faida
nyingi ninazoweza kupata zitokanazo na kujimimina kwenye Neno la Mungu:-
a)Faida ya kwanza nitakayoipata katika
kujimimina kwenye Neno la Mungu nitapata imani yenye uwezo wa kukabilianan na
kila aina yoyote ya jaribu linaloweza kujitokeza katika mzunguko wa maisha
yangu ya kila siku, katika jambo hili la kiimani ni la msingi sana lakini jamii
nyingi ya waamini hupuuzia, ndio maana maisha yao hukosa mwanga wa mafanikio
ingawa wanamuomba Mungu,hata Biblia imethibitisha Waebrania
11:6.
Ninashauriwa
kuishi katika misingi ya imani kwasababu imani ni kiunganishi kati ya mtu na
Mungu,vilevile imani inarahisisha mwamini kupokea Baraka zake pale tu anapoomba
kwenye uso wa Mungu.
b)Faida ya
pili itokanayo na kujimimina kwenye uwepo wa Mungu ni kibali,Kibali ni jambo la
msingi sana kwa kila mwanadamu mwenye mwili,kwasababu kibali kinampa mwamini
fursa ya kukubalika mahali popote anapoingia,vilevile kibali huweka wepesi wa
mkukubalika mbele ya jamii iliyomzunguka.
ANGALIZO 1:Nikipoteza kibali maana yake
nimepoteza mwelekeo wa maisha inatakiwa nirudi
magotini, na jambo hili wakristo wengi
wamejikwaa kwa kuwalaumu Watumishi wa Mungu.
Hali ya
kufundishwa Neno la Mungu ndio inayonisaidia mimi kama mwamini kunipa ufahamu
wa kutambua,Je! Nina kibali kwa Bwana cha kupokea Baraka zangu? Ndio maana hata
Zaburi 199:130 inaweka wazi kila
kitu.
Kufundishwa
Neno la Mungu kunaleta hali ya mwanga katika maisha ya mwamini itakayomsaidia
kumpa uwezo wa kupambanua vilevile kujisimamia katika imani.
(Hali ya
wakristo kushindwa kujisimamia inatokana na udhaifu wa imani waliyonayo).
Nikidhoofika
kiimani nitakuwa jalala la matatizo na magonjwa ,kwahiyo ili niweze kuliepuka hili inatakiwa niruhusu maisha
yangu yaongozwe na Neno la Mungu.
c)Faida ya
tatu itokanayo na kujimimina kwenye Neno la Mungu nii kupata mtiririko wa maombi na watu wengi jambo hili hawajui
kama ni la maana sana.
Mtiririko wa
maombi unakuwepo ndani ya mwamini mwenye kina cha ndani cha Neno la Mungu, na
maombi yanayojibiwa kwenye uso wa Mungu ni yale yanayoombwa sambamba na Neno la
Mungu.
Kuna
mahusiano kati ya neno YESU KRISTO na MUNGU, ndio maana Yesu Kristo akasema mtu akiomba sambamba na jina langu hilo atalifanya ili baba atukuzwe
ndani ya mwana,ila hapa kuna siri nzito.
Yohana 1:1-2 ,14
Wafilip 2:8-11.
Imani ndio
inayo niimarisha kwenye misingi ya wokovu,Wokovu ndio unaonirithisha uzima wa
milele.
(Nikitaka
kushinda vita vya kiroho ishu ni Neno).
(Nikmitaka
kubadilika kitabia na asili zote ziniache inatakiwa nikubali kufundishwa
Biblia).
ANGALIZO 2: Nikitambua uthamani wa kumheshimu Mungu sitaruhusu maisha yangu
yadhalilishwe
na kitu ambacho nina
uwezo wa kukiepuka.
Maisha ya
Neno la Mungu ndani ya mtu ili yaweze kumletea mabadiliko inategemea mahusianao ya mtu aliyonayo na
imani ya Yesu Kristo.
MFANO:
Nahitaji
kubarikiwa kwenye uchumi wangu lakini Mungu anatazama mahusiano yangu mimi na
utoaji ndipo ufungulie Baraka.
Nikitaka
maisha yangu yapate mabadiliko lazima niruhusu moyo wangu uelimishwe na Neno la
Mungu (Biblia).
Kitendo cha
Neno la Mungu kuelimisha moyo wangu maana yaek ni Yesu Kristo mwenyewe
anaelimisha moyo wangu, kwasababu Biblia imethibitisha Ufunuo 19:13.
(Kitendo cha
kusoma Biblia maana yake moyo wangu
unazungumza na Mungu moja kwa moja,kwahiyo nahitaji suala la nidhamu
wakati wa kusoma Biblia).
Je! Inatakiwa
nidhamu hii iwe katika mazingira gani?
i)Wakati wa
kusoma Biblia inatakiwa nijifungie mahali ambako hakuna kelele hii itanisaidia
moyo wangu kupata utulivu wa kupokea.
MFANO WA MAHALI AMBAKO HAKUNA KELELE
Chumbani.
ii)Wakati wa
kusoma Biblia inatakiwa nizime simu na vifaa vinavyoweza kuashiria kelele,
MFANO WA VIFAA VINAVYOASHIRIA KELELE:-Televisheni,Redio ,Feni ,Simu n.k.
Kelele za
vifaa hivi vilivyotajwa hapo juu huaribu mfumo wa ufahamu wa mtu katika kupokea
sauti ya Mungu kupitia Neno.
d)Faida
nyingine nitakayoipata kutokana na kujimimina kwenye Neno la Mungu ni mamlaka,
na jambo hili ni nyeti sana kwasababu
mamlaka ndiuo inayomsaidia mkristo anayeliamini Neno la Mungu kushinda katika
roho.
Mamlaka
iliyoko ndani mwangu nikizidi kuipalilia
katika Neno la Mungu ndivyo nitakavyozidi kunizalishia faida na siku
zote mamlaka hiushi katika kinywa cha mwamini ,ndio maana Mithali 18:20,21.
Imethibitisha wazi maneno haya.
Ulimi una
nguvu hai ya kuumba vilevile kuua, kwahiyo inatakiwa niwe mkristo mwenye
nidhamu sana kwenye moyo wangu ili maisha yangu yapate mpenyo.
ANGALIZO 3:Nikimuona mtu yupo kwenye uwepo wa
Mungu yaani kanisani alafu
anachukia kufundishwa maana yake hakuja kanisani kwa nia
njema,kwahiyo mtu wa
aina hii atapata madhara
yafuatayo:-
i)Laana
ii)Magonjwa
yote na matatizo wanayofunguliwa watu wengine huambatana nay eye, vilevile mtu
wa aina hii huwa ana roho ya
udhoofishaji ndani yake.
Rafiki
asiyetaka kwenda kusali kanisani ni kuwa naye makini,kwasababu roho anayokuwa
ameibeba ni ya udhoofishaji, kwahiyo nisipokuwa naye makini anaweza kuniua kiroho.
Somo litaendelea wiki
ijayo…………………………..
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni