Jumapili, 21 Desemba 2014

IMANI NA SADAKA

UJUMBE WA LEO
21/12/2014
                                                                   IMANI NA SADAKA.
Imani na sadaka  ni vitu viwili vinavyoishi sambamba, kwa  maana zaidi ni vitu ambavyo haviachani ,hii yote inatokana na utoaji ni imani


Wakristo waamini walio wengi hawatambui maana ya sadaka  ndani ya kanisa ,ukweli ni kwamba sadaka ni moyo wa kanisa.

Utoaji wa sadaka unahitaji uwe katika msingi wa imani, ndipo sadaka hiyo itapata kibali machoni pa Mungu
Luka 21:1-4.

Utoaji wa sadaka katika haki  uanao nafasi kubwa ya kutuongezea siku za kuishi, kwasababu sadaka ni moyo wa kanisa.

Jinsi ninavyokuwa na bidii ya kutoa sadaka  ndani ya kanisa ndivyo ninavyouimarisha  ufalme wa Mungu.

(Mkristo ambaye amejiepusha na kweli ya Mungu na haki yake , kamwe  hawezi kuwa na roho ya huruma  ndani yake).

Waamini wasiotoa sadaka kanisani bado hawajatambua  nini maana ya kumwabudu Mungu, kwasababu sadaka ni sehemu ya ibada.

Mkristo ambaye haoni uthamani wa kumtolea Mungu sadaka inayoeleweka  yuko mbali kabisa na uwepo wa Mungu, hii  hali inaweza kuathiri maeneo mengi sana katika maisha  ya mwamini.

Nikitaka sadaka zangu Mungu azikubali inatakiwa nitoe katika imani,kwasababu kutoa katika imani  kutanisukuma mimi kumtolea Mungu sadaka inayoeleweka  sio  chenji zilizozidi kwenye nyanya sokoni.

(Sadaka ni kitu kinacho heshimika  sana kwenye ufalme wa Mungu,kwasababu katika Matendo ya Mitume 10:1 ……..inaonyesha picha ambayo Mungu alimtuma Petro Nabii kwa Kornelio,hii ilikuwa ina lengo la kuonyesha dunia uthamani wa sadaka  tunazitoa kwenye uso,ndio maana Kornelio alipata kibali machoni pa Bwana).

Nikihitaji sadaka zangu ziwe na ukumbusho kwenye uso wa Mungu inatakiwa nifanye mambo yafuatayo:-
I)Nitoe kwa imani
II)Nitoe kuujenga ufalme wa Mungu kwa mali zangu.
III)Nitoe kwa lengo la kusaidia masikini.

Nikiwa ninapenda kufanyiwa vitu vizuri au kupewa vitu vizuri, lakini mimi mwenyewe sipendi  kuwafanyia watu vitu vizuri maisha yangu hayawezi kuinuka  yatabaki katika hali ya utumwa  siku zote.

(Siri ya kupata pesa ni kutoa).

Kuna maumivu mengi wakristo tunayoyapata yanatokana na kujikwaa.
(Nisipofahamu cha Mungu ni kipi  kwenye utajiri wangu maisha yangu ninakuwa nimeyaweka rehani).

SADAKA YENYE KIBALI:
Sadaka yenye kibali mbele za Mungu ni sadaka ile anayoitoa mwamini akifahamu moyoni mwake kwamba sadaka hiyo  aliyoitoa italitoa kanisa sehemu moja kwenda sehemu nyingine
Luka 7:40-50.

(Mungu anamthamini sana mtu ambaye ni mtoaji bila kutazama mazingira yake).

Hakuna maoni: