UJUMBE WA LEO
28/12/2014
IMANI NA SADAKA
SEHEMU YA PILI
Sadaka sio agizo la mwanadamu yeyote
bali ni agizo la Mungu mwenyewe ,kwahiyo sadaka ni kitu
kinachotolewa katika mazingira ya imani
.
(Mungu ana wivu sana katika eneo la utoaji ,kwasababu kile kinachotolewa
kinakuwa na lengo kuu la kuimarisha ufalme wake).
(Mkristo anayepinga katika eneo la utoaji wa sadaka huyo
ameshavamiwa na roho ya uasi ,kwasababu
hakuna baraka yoyote ya kifedha inayoweza kumjilia mtu kabla yeye mwenyewe
hajaandaa mazingira ya kumtolea Mungu kwanza).
Nikifanya vya Mungu kwanza kabla ya vyangu Mungu ataniona ni
mwenye imani kwenye uso wake,kwahiyo lazima atanilinda na kila pigo au uvamizi
uliokusudiwa dhidi yangu.
Mkristo asiyetambua uthamani wa sadaka katika nyumba ya Mungu
lazima ataandamwa na mambo haya ili mradi tu kila alicho nacho kiteketee:-
A)Magonjwa –Inafahamika
wazi magonjwa ni kitu kinachogharimu maisha yetu sana kwa pesa nyingi.
(Utoaji ni mfereji wa Baraka ya Mungu kuja kwenye maisha ya
mtu).
Hii ni hatari sana kama mimi sio mtoaji wa sadaka
nitavichuma sawa ila sitavila ,hii ilimtokea dhahiri Anania na Safira katika
kitabu cha Matendo ya Mitume 5:1-6,vilevileilmtokea Kaini mwana wa Adamu
katika Mwanzo 4.
(Sadaka ina nguvu ya utajiri ndani yake vilevile sadaka ina
nguvu ya laana ndani yake ambayo ninaiona laana hii ikimtafuna Anania na
Safira na Kaini na wengine wengi).
Kama sitambui uthamani wa sadaka kwenye nyumba ya Mungu na Mungu hatatambua uthamani kwenye maisha yangu .
(Mafanikio ya wakristo wengi yanajifunga kwasababu si watoaji).
ANGALIZO 1:Nkifahamu
chanzo cha Baraka yangu ni nani basi
itakuwa rahisi kufahamu
wa kumtolea.
Kama sisimami kikamilifu kutoa sadaka kwenye nyumba ya
Munguukweli ni kwamba ulinzi wa Mungu hautakuwepo kwenye maisha yangu hata Maandiko yamethibitisha hili katika Kitabu cha Hagai
1:1-15.
Baraka iliyo halali na yenye uwezo wa kuyabadilisha ni ile inayotoka kwenye mwongozo wa Roho
Mtakatifu.
JE!SADAKA NI NINI
Sadaka ni mbegu ninayoipanda kwenye uso wa Mungu katika mazingira ya utoaji , ndio maana
inatakiwa liwe ni jambo linalotoka katika imani .
SWALI-
Je!nitajuaje udongo una rutuba ya kunizalishia Baraka?.
JIBU-Ni 2 Wakorintho 3:17.
(Jina la Yesu Kristo
linatenda kazi pale nitakapo
tamka kwa imani).
Inatakiwa nitoe sadaka yangu kwenye nyumba ya Mungu kwanza katika
mazingira ya imani ,vilevile nikiwa na matarajio ya kupata Baraka
kutokana na sadaka hiyo.
Wakristo wengi sadaka wanazozitoa huzitoa katika hali ya kawaida ,ndio maana
hazizai Baraka ,hii inatokana na wao kutokutambua uthamani wa sadaka
wanazzozitoa kwenye nyumba ya Mungu.
Nikitambua sadaka ninayoitoa ninapanda mbegu kwenye uso wa
Mungu itatakiwa niongeze kiwango cha kutoa .
(Nikitoa kama desturi siwezi kuona umuhimu wa kumtolea Mungu
chenye maana).
Nikihitaji mpenyo katika suala la uchumi lazima nibadilishe mazingira yangu katika utoaji wa sadaka.
Jinsi ninavyotoa kuwajali wenye shida ndivyo Mungu anavyoniongezea Baraka tele nisipungukiwe
Wagalatia 2:10.
(Maisha ya mtu mchoyo mbinafsi hayana kibali machoni pa
Mungu).
Katika suala la kumtolea Mungu wakristo wengi wanakuwa
wanakaidi kwasababu wanatoa nje na
mapenzi ya Mungu.
Inatakiwa nimheshimu Mungu kuliko pesa nilizonazo nitaongezewa siku za kuishi.
Ni vigumu kuimiliki Baraka ikatulia katika mkono wangu kama
sijapewa ufahamu wenye uwezo wa kunipa
nguvu ya kuzitawala Baraka ,hili jambo ni nyeti sana.
ANGALIZO 2:Nikibarikiwa
wakati huohuo nikawa bado
sijaimarika kiimani nina hatari kubwa
sana inayoweza kunifanya nimuasi Mungu,kwasababu imani ya Yesu Kristo ni vigumu kuitawala pesa.
Ili niweze kuyatawala mafanikio inatakiwa niwe katika misingi ya kweli na haki.
Pesa ina kawaida ya kumfanya mtu kuridhika , na huko
kuridhika ndiko kunakompelekea mwamini kujisahau.
Baraka itakayoniingiza kwenye mafanikio ya kweli na haki
mpaka nikainuliwa na jamii ikanishangaa ipo katika mazingira matatu:-
A)Kutoa shukrani katika kila kitu ambacho Mungu ananisaidia
.
Sadaka ina nguvu ya kurejesha heshima ya mtu kwenye uso wa
Mungu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni