UJUMBE WA LEO
07/12/2014
RUHUSU IMANI
ITENDE KAZI
Wengi tunafahamu nini maana ya imani , vilevile tumejifunza
mengi kuhusu imani lakini kuna wengine wasio fahamu imani ni nini ingawa
wanasema tunaamini.
Ili niweze kufahamu nini maana ya imani inatakiwa nifahamu
kwanza imani inapatikanaje.
Imani kama imani chanzo chake ni hutokana na kusikia ujumbe wa Neno la
Mungu,hapo huwa ndio mwanzo wa mwamini kuwa na hofu na Mungu.
Warumi 10:17.
Imani ya mkristo inakua anavyozidi kujiwekea mazingira ya
kusikiliza Neno la Mungu,mkristo akiongeza bidii ya kusoma Biblia,kusikiliza
Neno la Munguyaani kufundishwa imani itakayojengeka ndani mwake itakuwa na
uwezo mkubwa wa kusababisha kitu kutokea.
Mkristo asiyeruhusu imani yake kutenda kazi anakabiliwa na
mambo yafuatayo:-
a)Ufahamu wa rohoni kujifunga
b)Kina cha maarifa ya rohoni kushindwa kupambanua
c)Kifo cha kiroho, mtu ambaye ameingia katika mazingira haya
ya mambo tajwa hapo juu anakuwa hana tena muunganiko na Baraka za Mungu kwa
maana zaidi akifanya biashara itakosa mpenyo,akiajiriwa atapoteza mpenyo kwa
bosi wake kifuatacho ni kufukuzwa kazi na mengine mengi yanayofanana na haya.
Nikitaka kuijenga upya familia yangu katika misingi ya hofu
ya Mungu inatakiwa nianze upya kuruhusu imani yangukutenda kazi kwa maana zaidi
kuliruhusu Neno la Mungu kuielimisha roho yangu.
Huduma ya Yesu Kristo wakati akiwa katika mwili ilikuwa na
nguvu kubwa sana na jamii nyingi ya waamini iliongezeka sana kwa wakati
ule,vilevile miujiza na ishara maajabu
mengi sana yalithibitika , ni kwasababu aliliimarisha kanisa katika misingi ya mafundisho na Biblia
inayathibitisha haya:-
Mathayo 9:35,36
Mathayo 8:1,5
Mathayo 7:28 na Marko 2:1,2.
(Hakuna muujiza wowote unaoweza kuthibitika bila imani ya
Neno la Mungu kuhusika).
Ili mkristo aweze kutoa hekima katika kinywa chake ,na
hekima hiyo iwe msaada kwa watu wengine inatakiwa awe katika mfumo wa mambo
haya:-
i)Awe ni msomaji wa Biblia sana,kwasababu hekima ya kweli na
haki iko ndani ya Neno la Mungu.
ii)Awe muombaji hiyo itamsaidia muda wote kuwa na muunganiko
na Roho Mtakatifu.
(Mkristo mwenye kina kirefu cha imani ana uwezo mkubwa wa
kupambanua sauti ya Mungu anaposema)
Nikitaka kuisikia sauti ya Mungu inatakiwa nitafute kina cha
imani.
Marko 2:1,2 ni
picha wazi inayodhihirisha huduma ya Yesu Kristo kwamba ilikuwa chini ya msingi
wa mafundisho , ndio maana kanisa liliimarika.
(Fahari ya kwanza inatakiwa iwe kwenye Maandiko
Mtakatifu yaani Biblia).
IMANI INAVYOTENDA
KAZI
Siku zote imani inatenda kazi katika mazingira magumu yaani
mazingira yaliyoshindikana , na hii inatokana na iamani ni kitu cha rohoni kwa
maana zaidi ni kitu kisichokuwa na umbo maalumu.
Nikitaka mazingira yanisaidie kumwamini Mungu nitakuwa sina
tofauti na mtu aliyekufa lakini anatembea ambaye Biblia ilimsema katika kitabu
cha Ufunuo 3:1.
Ili mkristo awe hai kiroho inatakiwa imani aliyonayo
airuhusu kutenda kazi, na imani ili iweze kazi inategemea ushirikiano wa mtu
binafsi.
Mkristo anapomwamini Mungu tayari anakuwa na muunganiko
katika roho na sio katika hali ya kimwili.
Mkristo asiporuhusu imani yake kutenda kazi maono yake hayawezi
kutimia hata kama anaomba usiku na mchana .
Ili niweze kuifahamu
imani yangu imekuwa hai ni pale ambapo nitakapoanza kutendea kazi kila
mwongozo nitakaopewa na Roho Mtakatifu kupitia mtumishi wake.
(Hichi kitu inabidi nikiache
kabisa nizaliwe upya .Je! kitu gani?)
Ushabiki wa kiroho ni mbaya sana unaharibu makanisa ‘Yesu
nisaidie’)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni