UJUMBE WA LEO
30/11/2014
LAZIMA NITAMANI
MABADILIKO YA KIIMANI
SEHEMU YA TATU
Hali ya kutamani mabadiliko
ndani mwangu ndiyo itakayonipa
ujasiri wa kulazimisha mabadiliko kutokea .
(Nikijiona ninamkosea
Mungu hiyo ni picha wazi bado nina udhaifu katika imani )
Roho ya uaminifu inajiumba katika maisha ya mtu pale ambapo
ataruhusu roho yake kuendelezwa na Neno la Mungu.
Mwamini akiwa bado hajaruhusu hali ya mabadiliko ndani mwake ni vigumu kuambatana na Baraka za
Mungu hata angekesha na kuomba
Amosi 3:3.
(Suala la ufahamu katika kumtafuta Mungu ni jambo la muhimu
sana).
Mtu wako wa nje ambaye ni wewe mwenyewe ukiishi sambamba na
mtu wako wa ndani Baraka za Mungu
zitakuwa kama maafuriko ya mto,kwasababu siku zote mtu wa ndani ni mkamilifu na mnyenyekevu.
Dhambi ndiyo inayoharibu uthamani wa maisha ya mwamini.
(Kama ninahitaji Baraka za Yesu Kristo lazima nifanye
mabadiliko katika maisha yangu ya kiroho).
Maisha ya kiroho yanahitaji mambo haya yafuatayo
i)Uaminifu
ii)Kuishi katika kweli.
iii)Kujinyima .
Ni vigumu kuiokoa imani yangu bila kujinyima mambo mengine
ambayo ni haki yangu
Mfano wa mambo ambayo ni haki yangu:-
i)Chakula
ii)Starehe za kimwili n.k.
Misingi ya uaminifu nitakayoamua kuijenga kuanzia sasa ndiyo itakayo rejesha heshima yangu kwenye uwepo wa Mungu, vilevile
kunipatia kibali kwa upya kwenye uwepo wa Mungu.
(Chanzo cha magonjwa katika
maisha ya mwanadamu mwenye mwili ni dhambi, ndiyo maana Kumbukumbu la Torati 28:15-62
inathibitisha hili).
Ukamilifu wa maisha ya mwamini ni pale ambapo anaporuhusu
kuishi maisha ya kweli yote ya Mungu.
Ninashindwa kuyatawala maisha yangu ya kimwili kwasababu
sina ufahamu wa kutosha wa Neno la Mungu, mara nyingi hali ya mwamini
kudhoofika kiimani inatokana na kukosa
ufahamu wa Neno la Mungu.
Namna ambavyo ninweza kuruhusu hali ya kupata ufahamu ni
pale ambapo nitaruhusu roho yangu kuendelezwa katika misingi ya Biblia.
Ni vigumu kuishi maisha Matakatifu kama sijaamua kufuata
nyayo za Yesu Kristo.
SWALI: Je!
Yesu Kristo aliishi maisha yapi?
JIBU
a)Aliishi katika haki
1Yohana 2 :28-29
b)Aliishi katika Upendo
c)Aliishi katika
kusaidia (utoaji)
d)Aliishi katika
Uvumilivu.
UFAFANUZI KUHUSU
KIPENGELE ‘A‘ KINACHOZUNGUMZIA HAKI
Yesu Kristo aliishi katika maisha ya haki ndiyo maana kila
jambo alilolikusudia lilithibitika
palepale.
Nikitaka Baraka ya Yesu Kristo niishi katika haki.
1Yohana 2:29 ni hali halisi katika maisha yangu
kama mcha Mungu yaani Baraka za Ibrahimu ,Isaka na Yakobo, na ni uthibitisho
uliopo wazi bila haki hakuna Baraka .
Asilimia sabini na tano za wakristo hupata Baraka za umoja kutoka kwenye uso wa
Mungu, Je! Zipi hizo? Zile alizozinena kwenye maandiko Matakatifu ya kwamba
huwanyeshea mvua walio haki na wasio haki na ndizo Baraka ambazo waamini wengi
wameridhika nazo,ndiyo maana hawana
mwamko wa kuruhusu mabadiliko katika masiha yao ili waweze kuendana na zile Baraka
ambazo Mungu amewaahidia wenye haki yaani Baraka za Ibrahimu ,Isaka na Yakobo.
Nini maana ya Baraka za Ibrahimu, Isaka na Yakobo ?
Maana yake ni Baraka ya
kuurithi ufalme wa Mungu pamoja na haki yake.
*Pesa sio ishu ,ishu ni upako*
ANGALIZO 1:Safari
ya kutafuta haki ya Mungu ni safari ndefu sana ambayo inahitaji uvumilivu wa hali ya juu.
UFAFANUZI KUHUSU
KIPANGELE ‘B’ KINACHOZUNGUMZIA UPENDO:
Siku zote mwanadamu ana upendo wa kibinafsi ,na upendo huu
uliofungamana na maisha ya mwanadamu ndiyo umekuwa kipingamizi cha kwanza
kinachozuia Baraka za Mungu kuyaneemesha maisha yake.
Ili upendo wa mwamini uwe katika kweli ya Mungu unatakiwa
uwe katika mfumo wa mambo haya yafuatayo:-
i)Usomaji wa Biblia kwa kina
ii)Ufungaji (kuomba ) mara kwa mara
iii)Uaminifu.
Kama sijaruhusu maisha yangu kuwa chini ya mwongozo wa Maandiko Matakatifu ile asili ya Mungu
ambayo ni upendo haiwezi kujijenga , kwahiyo kama ninataka kuimarika katika
upendo wa Mungu ni haki yake .
Lazima niandae mazingira ya kuheshimu mwongozo wa Roho
Mtakatifu unapotoka kwa maelekezo fulani.
Mkristo akitaka wokovu wake uwe salama inatakiwa aruhusu
upendo wa Mungu ujijenge ndani yake hapo
atakuwa ameiokoa imani
1Wakorintho 13:13.
Upendo ulio katika maisha ya mwamini ndiyo
unaodhihirisha kiwango cha imani
aliyonayo katika maisha yake , nah ii ni kwasababu Biblia imethibitisha upendo
ni roho ya Yesu Kristo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni