UJUMBE WA LEO
14/12/2014
RUHUSU IMANI ITENDE KAZI:
SEHEMU YA PILI:
(A)IMANI
INAVYOTENDA KAZI
Kila mwanadamu anayeishi katika mwili amepewa kiasi cha
imani ,mwendelezo wa imani hii
aliyopewa na Mungu utatokana na namna
ambavyo ataruhusu moyo wake kumwamini
Yesu Kristo, vilevile na kinywa chake kumkiri Yesu Kristo,hapo ndiko
kunakotokea chimbuko la wokovu
Warumi 10:9,10
Imani ya mwamini inapata nguvu ya kutenda kazi ikishakuwa na
muunganiko wa ndani wa Neno la Mungu.
Ili imani niliyonayo iwe msaada na maisha yangu inatakiwa
nisimame katika msingi wa mambo mawili:-
A)KWELI
B)HAKI.
(Maisha ya ukweli,maisha ya haki ni ufunguo wa Baraka zangu
kwenye uwepo wa Mungu).
Maisha ya kweli katika jamii ya waaminio ndiyo yanayotakiwa,
kwasababu jamii kubwa ya wasioamini inatakiwa washawishike kumjua Mungu kupitia
maisha yetu sisi kama waamini.
(Mkristo yeyote anayemcha Mungu anastahili kuishi maisha ya
kiimani ndiyo yanayozaa haki na kweli ndiyo maana hata Biblia imesema Zaburi 51:6).
Sababu ya imani ya mkristo kuwa na upofu inatokana na
kutokuishi maisha ya kweli na haki ,vilevile ndicho kimekuwa chanzo cha Baraka
za wakristo kujifunga yaani kutokupata mpenyo.
Jamii kubwa ya waaminio wanazikosa Baraka za Mungu kwasababu
wanaishi kinyume namapenzi ya Mungu.
Maisha ya kweli na haki huisaidia imani ya mkristo
kudhihirisha mamlaka yake waziwazi na hapo ndipo unapotokea mwanzo wa mafanikio
katika maisha ya mwamini.
Imani yenye uwezo wa kutenda kazi inayavaa maisha ya mtu
pale ambapo mtu huyo ataamua kuruhusu Neno la Mungu kuiendeleza roho yake,Hili
jambo lipo hata katika maandiko
Warumi 10:17.
(Nikihitaji kwenda sambamba na Baraka za Mungu lazima
niruhusu hali ya ukuaji wa kiimani).
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni