16/11/2014
UJUMBE WA LEO
LAZIMA NITAMANI
MABADILIKO YA KIIMANI
Mabadiliko katika maisha ya mwamini yanatokana na mwamini anavyozidi kukua
katika ufahamu wa rohoni.
(Mwamini asiyekuwa na ufahamu wa Neno la Mungu ,hana mvuto
wa kubarikiwa na Bwana)
Mkristo anavyozidi kutamani mabadiliko ya kiimani ndivyo Mungu
anavyomtengenezea wepesi wa kuzifikia Baraka zake ,vilevile Baraka za wakristo
zimegawanyika katika makundi yafuatayo :-
a)Baraka za kiuchumi
b)Baraka za kiafya
c)Baraka za kiroho
Mimi kama mkristo mwamini inatakiwa nifahamu maeneo ambayo
natakiwa nifanye mabadiliko katika maisha yangu
Baraka za mkristo chanzo chake ni Neno la Mungu.
Kutokuitii sauti ya Mungu inayotoka madhabahuni inaonyesha
wazi namna ambavyo mkristo hana ufahamu wowote na Neno la Mungu hata kama kila
siku anaingia kanisani.
Lazima nifanye mabadiliko ya kiimani kwasababu maisha ya
mkristo aliyeokoka yanahitaji msaada wa Roho Mtakatifu kwa asilimia mia moja,
vilevile mwongozo wa Roho Mtakatifuutaimarika katika maisha ya mkristo ambaye
amezama katika kina cha Neno la Mungu.
Mabadiliko ya kiimani yatamsaidia mwamini kutembea katika
misingi ya haki ambayo ndiyo Munguanaitaka aione kwa waamini.
(Nikiyaendesha maisha yangu katika misingi ya kiimani
mabadiliko nitakayoyafanya yataniletea Baraka )
Kwanini Nuhu alipata kibali machoni pa Bwana ?Mwanzo 6:8,9.
Nuhu alipata kibali machoni pa Bwana kwasababu aliishi
katika mazingira haya:-
a)Mazingira ya ukamilifu
b)Mazingira ya haki.
c)Mazingira ya utauwa
Kwanini wakristo wa leo hawapati kibali machoni pa Bwana?,
ni kwasababu
a)Wanaishi katika mazingira ya visasi,na inafahamika wazi
mtu mwenye kisasi ndani ya moyo hana uwezo
wa kusamehe, na hii imesababisha vifo kwa wakristo wengi
b)Wanaishi katika mazingira ya kutokuamini na hili jambo
limepeperusha Baraka za wakristo wengi sana.
Wanaobarikiwa katika uwepo wa Mungu ni wale wanaofuatilia kwa makini mwongozo
wanaopewa na Roho Mtakatifu.
(Wakristo wengi wamepoteza miujiza yao kwa kutokutii
maelekezo wanayokuwa wamepewa na Roho Mtakatifu).
Ukidharau maelekezo maana yake umeidharau nguvu ya uponyaji
hakutakuwa na mabadilikom katika maisha yako, utakuwa ni mkristo aliyedumaa
kiroho.
Mkristo ambaye ametamani mabadiliko ya kiimani maana yake
ameamua kuishi maisha ya utauwa.
Maisha ya utauwa yatampa mkristo faida zifuatazo:-
a)Kibali machoni pa Mungu (Neema)
b)Maombi yake kupata mpenyo wa kuleta majibu Yohana 14:13.
c)Mamlaka itakayoweza kusababisha hali ya wepesi katika
mzunguko wa maisha yake ya kila siku Luka
10:19-20.
Mkristo anayeishi maisha ya utauwa amepewa nafasi ya
kujibiwa hoja yoyote kwenye uso wa Mungu,na hili limethibitishwa katika
maandiko Yohana 14:13, vilevile ni
hali halisi kwa mwamini anayeishi maisha ya utauwa.
Mkristo anayeishi maisha ya utauwa ameamua kujinyima kwa
ajili ya Yesu Kristo.
Nikiwa ni mkristo ninayeishi katika misingi ya imani ya Yesu
Kristo haitakiwi nihukumu juu ya jambo lolote hata kama linanipa maumivu, hiyo
ndiyo njia ya kunionyesha kwamba
nimepata mabadiliko ya kiimani.
Ninapolipiza kisasi maana yake ninausaliti uso wa Mungu.
Luka 10:20 ni
tahadhari nzito kwa wakristo wenye kiburi cha uzima.
Hali ya majivuno husababisha kiburi cha uzima ambalo ndiyo
anguko la wakristo wengi waliokoka.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni