UJUMBE WA LEO
9/11/2014
NAMNA AMBAVYO
IMANI INAATHIRIWA:
Inafahamika wazi imani ni kuwa na hakika na mambo
yanayotarajiwa ,vilevile ni bayana ya mambo yasiyoonekana ,kwa maana zaidi imani ni
kitu cha Rohoni.
Ninaposema nina imani maana yake ninatamka kitu chenye umbo la kiroho ,na
ukweli ni kwamba umbo la kiroho halishikiki kwenye mikono ya damu na nyama,
ndiyo maana tuna heri sisi tunayemuona Yesu Kristo katika misingi ya kiimani kuliko wale waliomuona katika misingi ya kimwili ,kwahiyo haitakiwi
nijidharau.
Yohana 20:27-29.
Mkristo anayepiga magoti na kumuomba Mungu katika imani ya
Yesu Kristo huyo ni mkristo mwenye kibali kwenye uwepo wa Mungu, kwa hiyo
katika jamii iliyomzunguka atakuwa ni mtu wa tofauti, kivipi yaani atakuwa ni
mtu anayeyaendesha maisha yake na maisha ya watu wengine kwakutumia mamlaka ya
Roho Mtakatifu.
Katika suala la kuamini
inatakiwa niutii utu wangu wa ndani ndiyo unaonipa uthibitisho,kwasababu
Roho Mtakatifu anaishi ndani ya utu wa ndani wa mkristo mwamini.
Katika suala la kuamini inatakiwa niwe mimi mwenyewe na utu wangu wa ndani hapo
kutatoka imani hai.
(Utu wangu wa ndani ukikosa msaada wangu mimi siwezi kupata
mabadiliko)
Kwa asilimia sabini
na tano imani za wakristo zinaathiriwa na mawazo mabaya.
(Mawazo mabaya yakishauvaa
moyo wa mkristo mwamini hata kile anachokifahamu kizuri kuhusu Mungu
atakikataa)
Jambo hili ni la kuchunga sana na kuwa makini nalo jinsi
ninavyoruhusu hali ya kuwaza vibaya moyoni mwangu ndivyo ninavyo tengeneza taswira ya kuamini kinyume
na Mungu.
Namna ambavyo ninaruhusu mawazo mabaya kuuvamia moyo wangu
ndivyo ninavyotengeneza sumu ya kuathiri imani yangu kuhusu Mungu.
Mfanikio ya kiroho katika maisha yangu yatakuja kadri
ambavyo ninakaribisha mawazo ya Mungu ambayo ni Neno lake katika maisha yangu.
Mwanzo wa maisha ya wakristo kuharibika ni kuruhusu mawazo mabaya kujijenga katika
mioyo yao,ninaporuhusu mawazo mabaya kujijenga kwenye moyo maana yake
ninaruhusu utawala kamili wa shetani kuyaharibu maisha yangu ya kiroho.
Dhambi yoyote anayoifanya mwanadamu anakuwa na akili zake
timamu ,ndiyo maana dhambi ni ugonjwa wa ufahamu.
Nikiamua kufunga milango ya vitu visivyokuwa na utukufu kwa
Mungu maana yake ninailinda imani.
Ili niweze kujijenga kiimani haitakiwi moyo wangu niuweke
wazi kwa mambo yasiyokuwa na utukufu kwa Mungu.
(Ninapomjali mtoto mdogo maana yake ninamjali Mungu,kwahiyo
inatakiwa nimjali mtoto katika maeneo haya yafuatayo:- i)Mavazi
ii)Chakula kizuri
iii)Shule nzuri.
iv)Kumuonyesha upendo vilevile kumuonya katika mazingira ya upendo.
Ili kuzishiriki Baraka za Mungu inatakiwa niwe mbunifu sana.
Haitakiwi nikumbuke
ninacho samehe kwa mtu,ndiyo silaha ya kuilinda imani.
Imani ya mwamini itapona kama mwamini huyo ataruhusu Neno la
Mungu kuingiza wazo jipya ndani ya moyo wake.
Inatakiwa niruhusu imani ya Yesu Kristo kusimama moyoni
mwangu, kwasababu ndiyo inayonisaidia kukabiliana na mazingira yoyote yale.
Mimi nikiruhusu Neno la Mungu kuingiza wazo jipya kwenye
moyo wangu, maana yake ninajikabidhi kwenye milki ya Mungu kuyaongoza maisha
yangu.
Mkristo anavyoongeza bidii ya kujifunza Neno la Mungu ndivyo
maisha yake ya kiroho na kimwili yanavyo badilika
1Timotheo 4:16.
Usalama wa maisha ya mkristo upo katika mafunuo ya Roho
Mtakatifu.
Kanisa lisipoimarishwa kwenye misingi ya mafunuo (Neno la
Mungu)lazima lipoteze mwelekeo,kwahiyo kanisa litakuwa hai kama lina misingi ya
mafunuo ya Roho Mtakatifu.
MBINU ZA KUILINDA
IMANI ISIPOTEZE MWELEKEO
(Inatakiwa nifanye kitu ili kumgusa Mungu,ili niwe mwanzo wa
Baraka zangu kwenye uwepo wa Mungu).
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni