UJUMBE WA LEO
23/11/2014
LAZIMA NITAMANI
MABADILIKO YA KIIMANI
SEHEMU YA PILI
Mabadiliko ya kiimani yanaanza kuonekana kwa mkristo mwamini
pale ambapo anaruhusu hali ya utii inayotoka chini ya mwongozo wa Neno la
Mungu.
Mkristo mwamini anaporuhusu hali ya utii ndani ya moyo wake maana
yake amefungua milango ya iamni yake kupevuka yaani kukua.
Utii alionao mkristo katika Neno la Mungu ndio unaotengeneza
mazingira ya imani yake kukua siku hadi siku.
Utii ni hali ya kukubali
na kutendea kazi mwongozo unaopewa.
(Ni ngumu sana kupata
mpenyo kama niko kinyume na mwongozo).
Mungu amedhihirisha
wazi Baraka inayoambatana na mwamini mwenye utii katika moyo wake,
vilevile amedhihirisha laana itakayompata mwamini asiyetii mwongozo wa Neno la
Mungu
Isaya 1:19-20.
Baraka ya Mungu iko wazi katika maisha ya mkristo mwenye
hali ya utii wa Neno la Mungu katika moyo wake.
Suala la utii lisiwe ni jambo la kuja na kutoweka bali
inatakiwa liwe ndio mfumo mzima wa maisha yako ya ukristo.
(Utii alionao mkristo ndio unaomtengenezea kibali kwenye
uwepo wa Mungu).
Ninapopewa taarifa nikaacha kuitendea kazi maana yake moyo
wangu umemdhihaki Mungu waziwazi hii ni hatari sana , ndio maana watu
wengi chini ya jua wanakufa kabla ya ule umri ambao Mungu aliunena
kupitia kwenye kinywa chake.
Jinsi ninavyoruhusu hali ya utii katika moyo wangu ndivyo
ninavyokaribia uwepo wa kubarikiwa.
(Utii ndio unaozaa hali ya unyenyekevu katika maisha ya mtu
, vilevile ni hali inayorahisisha wepesi wa maisha ya kupata mpenyo).
Wakristo wengi wana hali ya kutokutii, nah ii ni kwasababu
macho yao ya kiroho yamepofuka.
Hali ya utii kwenye moyo wa mtuitakua kulingana na mwaminianavyoongezeka
katika ufahamu wa Neno la Mungu.
ANGALIZO :1.Nikienda
kinyume na mwongozo wa Roho Mtakatifu maana yake ninajiharibia
mzunguko mzima wa Baraka zangu
katika maisha yangu yote, vilevile kutatokea
hali ya kupoteza uhalisia wa ucha Mungu, kwahiyo ndio utakuwa mwanzo wa
mwamini kuyaishi maisha ya dhambi.
Nikitaka kushinda katika maisha ya kiroho niliheshimu Neno
la Mungu, vilevile niishi chini ya sheria ya Mungu.
Namna ambavyo ninaonyesha
katika kile ambacho Mungu anasema na mimi ndivyo ninavyorahisisha hali
ya ukuaji wa kiimani.
Bila kuruhusu hali ya utii kukua ndani ya moyoy wangu ni
vigumu kupata utulivu wa kupambanua sauti ya Roho Mtakatifu pale anaposema na
mimi, ndio maana waamini wengi humkemea Roho Mtakatifu pale anaposema nao katika mioyo yao.
(Ufahamu ni ishu nyeti sana katika maisha yamwamini vilevile
ni kitu ambacho kila mwamini anatamani kuukulia
ufahamu, maana bila ufahamu wa kiroho maisha yanakwama).
Nikiwa nina utii ninajiongezea asilimia za kukubalika kwenye
uwepo wa Mungu.
Jinsi ninavyotii mwongozo wa Neno la Mungu ndivyo
ninavyojiongezea hali ya kibali kwenye uso wa wanadamu.
2 Petro 1:1-11.
Mwamini anaporuhusu hali ya utii wa Neno la Mungu kuwa kama
kiongozi katika maisha yake basi kuna misingi ya mambo kadha itakayojijenga na kuambatana na imani yake :-
a)Wema
b)Maarifa.
c)Kiasi.
d)Saburi.
e)Utauwa.
f)Upendo,kwahiyo mwamini mwenye misingi hii ataitwa haki
kwenye uso wa Mungu.
NINI KIFANYIKE ILI
HALI YA UTII IUMBIKE NDANI MWANGU:
Nikitaka hali ya utii ijiumbe ndani ya moyo wangu inatakiwa
niruhusu roho yangu kuelimishwa na Neno la Mungu (Biblia).
Jinsi ambavyo ninatoa ushirikiano wa kujiendeleza kiroho
kupitia Neno la Mungu ndivyo ambavyo Neema ya kukua zaidi kiimani itakavyoimarika ndani mwangu.
Bidii nitakayoionyesha
katika kujifunza Biblia ndani yake kutazaliwa Neema itakayo nirahisishia
mpenyo wa mabadiliko ya kiroho.
Kumbukumbu la Torati 28:1.
Nini maana ya kusikilizasauti ya Mungukwa bidii? Maana yake
ni kuliweka Neno la Mungu katika hali ya vitendo.
Bidii ya mwamini katika kumtafuta Mungu huonekana katika
mazingira ya vitendo siku zote.
Bidii ya mwamini katika kumtafuta Mungu inaanzia pale ambapo
mwamini anaamua kujinyima vitu ambavyo
ni haki yake kwa ajili ya Mungu
Mfano wa vitu ambavyo ni haki yangu;-
I)Kula na kunywa ,itanilazimu nijinyime hivi kwaajili ya
kumtafuta Mungu yaani kufunga ,ndio
maana hata Biblia ikazungumzia kitu juu
ya vyakula
Warumi 14:17-23.
ANGALIZO .2:Ninaposhindwa
kutoa sadaka kanisani vilevile fungu la kumi kiuaminifu
ninaonyesha
wazi utovu wa nidhamu kwenye uwepo wa Mungu, kwahiyo katika hali ya
uhalisia
wa kimungu hakuna Baraka yoyote inayoweza kuingia kwangu zaidi ya laana ,
kwahiyo ili niweze kupona katika hili inabidi
nionyeshe hali ya utii kwenye Neno la
Mungu kama ilivyoandikwa katika Malaki
3:8-10.
(Ufalme wa Mungu ni kufungua moyo wangu kwa utii wa mambo
mema ).
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni