Jumapili, 7 Septemba 2014

Somo la Leo: PALILIA IMANI



SOMO LA JUMAPILI: 7/9/2014

Somo la Leo:    PALILIA IMANI

• Inatakiwa niipalilie imani yangu kwa sababu imani yangu ndio msaada wa maisha yangu, vilevile Imani niliyo nayo nikiipalilia vizuri ndio itakayo nisaidia kupata utawala wa rohoni, na ndicho kinachotakiwa kwa mkristo anayemwamini Yesu Kristo.


ANGALIZO NO. 1 :
      • Majaribu yaliyonizunguka yataondoka kwangu kadri Imani     yangu  inavyokua .

      • Namna ambavyo naweza kuipalilia Imani yangu ikawa na mizizi ambayo itanisaidia kukabiliana na changamoto yoyote ile ni kuruhusu moyo wangu uelimishwe na Neno la Mungu ( Biblia ).  

       •Hii inasikitisha wakristo wengi hupuuzia kujifunza Neno la Mungu ( kusoma Biblia ) ndio maana shetani amepata uwezo wa kuwaweka waamini chini ya mgandamizo

      • Mgandamizo hauwezi kuruhusu imani ya mkristo kupokea Baraka zake kutoka kwenye uso wa Mungu, kwa sababu mgandamizo huyapofusha macho ya imani ya mkristo ,kwa hiyo ni vigumu mkristo kutambua kusudi la Mungu katika maisha yake.

       •( Macho ya imani yakipofuka mkristo ataishi chini ya utumwa wa dhambi  )

       •Mkristo aliyepofuka macho ya kiroho hawezi kuwa na ufahamu wa kutambua Baraka za Mungu zinakuja kwake kwa njia gani.

               -Jambo la kufahamu katika maisha yangu kama mwamini wakristo tuliookoka lazima tuwe makini sana tunaishi katika maisha yenye changamoto na vipingamizi vingi sana, ndio maana inatakiwa kuziendeleza roho zetu katika kumfahamu Mungu zaidi ili tupate wepesi wa kuyafikia maono yetu

       • Nisipo ruhusu roho yangu kuendelezwa na Neno la Mungu Imani yangu itapoteza ujasiri wa kukabiliana na utawala wa giza.
              - Mfano mzuri katika Biblia wa mkristo aliyepoteza utawala katika roho ( ujasiri ) ni wana wa Skewa.  Matendo ya Mitume;  19:13-16
       •Mkristo anayeishi chini ya mgandamizo ndani yake hana mamlaka yoyote ya kukabiliana na ufalme wa giza.

       •Mkristo anayeishi maisha ya dhambi maisha yake hukosa mpenyo, vilevile mwanga wa ki-Mungu Mstari wa 16,

       •Imani ya mkristo ikikosa ujasiri ni vigumu kuruhusu mpenyo wa  Baraka

       •Mkristo ambaye haishi maisha ya ukweli kila jambo mbele yake litampa utata.

       •Mwamini akiamua kuipalilia imani yake kupitia Neno la Mungu changamoto zitakazo jitokeza mbele yake hazitakuwa na nguvu.

        •Ili niweze kuvuka kila changamoto inayojitokeza mbele yangu inatakiwa niruhusu Neno la Mungu kuyaongoza maisha yangu. Yohana 5:5-9 
         •Mgandamizo ukiyakalia maisha ya mwamini, imani aliyonayo hupoteza mwelekeo yaani hata kile anachokijua anakisahau
         *(Mkristo anayeishi katika maisha ya mgandamizo kamwe hawezi kuishi maisha ya ukweli mpaka afunguliwe, na inafahamika wazi maisha ya ukweli ndio yanayo ruhusu Baraka za Mungu kuambatana na mtu. )*
          •Sauti ya Mungu ni Neno lake kwa maana zaidi ninaposoma Biblia najibishana na Yesu Kristo uso kwa uso.
          •Wakristo wa leo hawaamini kwamba Biblia ni hai katika maisha yao ndio maana kanisa la leo  halisisitizwi kabisa katika kusoma Biblia, ndio maana wakristo walio wengi wameweka tegemezi zaidi katika kuombewa kuliko kukaa chini na kujifunza neno la Mungu likampa maarifa ya kumtoa katika matatizo aliyonayo.

NIKIIPALILIA IMANI YANGU ITANIPA FAIDA ZIFUATAZO : 
A. Kutembea na Roho Mtakatifu
B. Kupata mamlaka ya Neno ( Uumbaji )
C. Nguvu ( Power )

UFAFANUZI WA VIPENGELE HAPO JUU:
A. Kutembea na Roho Mtakatifu.
     o Mkristo anayeishi maisha ya Imani ndiye mwenye uwezo wa kutembea na Roho Mtakatifu kwa sababu mwamini wa aina hiyo anakuwa anaishi sambamba na mapenzi ya Mungu.
     o Roho Mtakatifu anajifunua kwa mkristo mwenye kina cha Neno la Mungu.
     o Nikiwa Mkristo nisiyekuwa na kina cha Neno ninakuwa ni Mkristo kimwili lakini kiroho sio Mkristo.
     o Mwamini anayetambulikana kwamba ni Mkristo katika roho ni Yule ambaye maisha yake anayaendesha kama Neno la Mungu linavyosema hata kitabu cha Warumi kimesisitiza . WARUMI 8: 13- 16,  

ANGALIZO NO. 2
     o Mkristo mwamini akiishi kwa kufuata maumbile ya kibinadamu yaani mapenzi ya mwili hawezi kuungana na Baraka za Mungu, kwa sababu Mungu kuna kitu amesema katika kitabu cha Wakorinto.
      o 1 wakorinto 6 : 17  -( Lakini yeye aliyeungwa na Bwana ni roho moja naye ).
Nini maana ya kuungwa na Bwana kama inavyosema  1kor 6:17 ?
      • Maana ya kuungwa na Bwana ni kuyafanya maisha yangu yakae chini ya muongozo wa neno la Mungu maana yake Biblia.

Wiki Ijayo message hii itaendelea

Hakuna maoni: