21/09/2014
PALILIA IMANI SEHEMU YA TATU
UFAFANUZI WA KIPENGELE (C )
NGUVU (POWER).
Wakristo waamini tunapata nguvu ya Mungu kupitia Neno (
Biblia).
Neno la Mungu ndilo linalompa
mkristo mwamini nguvu( uwezo ) wa kukabiliana na ufalme wa giza
( Mkristo atakaye mwuona Mungu ni Yule atakayeweka mizizi katika Neno
la Mungu).
Katika kufundishwa Neno la Mungu(Biblia
) ninapata faida ya upeo wa ufahamu wangu kuongezeka ,kwahiyo itanisaidia namna
ya kuambatana na Baraka za Mungu.
Nguvu ya Mungu inajiumba kwa
mkristo ambaye ameamua kuutia moyo wake ufahamu wa kufundishwa Neno la
Mungu.
( Nikiwa kwenye uwepo wa Mungu nahitaji
kuwa na uhalisia wa kile kinacho tamkwa ndipo nitafanikiwa).
Wakristo wengi wanaokuwa kwenye
uwepo wa Mungu wanapoteza uhalisia wa kupokea Baraka zao kwasababu misingi ya
imani yao imejijenga katika vinavyoonekana.
Biblia ni nguvu ya mkristo
anayemwamini Yesu Kristo.
Mkristo anayesoma Neno la Mungu
katika imani lile neno linakuwa hai kwake kwahiyo hata atakapo kutana na
majaribu atapata wepesi wa kupenya kwasababu nyuma yake kuna nguvu ya Neno la
Mungu.
Mkristo
aliyelifanya Neno la Mungu kuwa sehemu ya maisha yake akawa analisoma katika misingi ya kiimani
akaliheshimu na kuliamini hila yoyote ya shetani haiwezi kumsogelea kwasababu Neno la Mungu humfunua
shetani na kumuacha uchi mbele ya macho
ya mkristo anayeliamini Neno la Mungu Waebrania 4:12.
Ninapolisoma Neno la Mungu moyoni
mwangu ninajengeka katika nguvu za kiroho,kwahiyo
kila jambo nitakalolifanya au
nitakalolikusudia moyo wangu utanipa ishara kwamba ni sahihi au si sahihi.
Wakristo wengi wametumia
nguvu nyingi sana katika kujiharibu,
tena sanasana jamii ya waaminio ,kuliko kutumia nguvu nyingi kujijenga katika
imani.
Mkristo akifundishwa Neno akapata
nguvu za rohoni shetani hawezi kupata nafasi ya kuingiza uvamizi.
Nguvu inakuja katika moyo wa
mwamini kadri mwamini anavyoongeza juhudi ya kulisoma Neno la Mungu
Zaburi 119:11
Madhaifu yanaingia katika maisha
ya wakristo ,kwasababu mioyo yao inakuwa tayari imepoteza nguvu ya Neno la
Mungu.
Moyo wa mkristo ambao umepoteza
nguvu ya neno tabia za mwilini yaani za
kimwili huanza kujidhihirisha.
Nikiona tabia Fulani ya kimwili
inaambatana na mimi au inanisumbua sana inatakiwa niongeze juhudi katika
kusoma Biblia na kufundishwa Neno la
Mungu hapo nitapata mpenyo wa ushindi.
Tabia yoyote iliyofungamana na
maisha ya mtu isiyompendeza Mungu ili iweze kun’gooka inatakiwa roho ya mtu huyo ielimishwe na Neno
la Mungu kwelikweli kwasababu tabia haina tofauti na roho chafu,
ndio maana Biblia Zaburi 119:9 imetoa siri ya ushindi.
Njia ya kuyafanya maisha yangu ya
wokovu yawe safi ni namna nitakavyokuwa na juhudi katika kujifunza Neno la
Mungu , hii husaidia zaidi kuyafanya maisha ya
mwamini kuwa karibu na uwepo wa Mungu.
FAIDA YA NGUVU YA NENO:
Moyo wa mwamini ukiimarika katika Neno la Mungu ndani
mwake huzaliwa imani yenye uwezo wa
kuumba ,jambo hili lilimkuta Petro na Yohana wakielekea hekaluni .
Matendo ya Mitume 3:1-.
Katika Matendo ya Mitume 3:4. Kuna
kipengele ambacho Petro alisema “ tutazame sisi” alikuwa akidhihirisha wazi nguvu ya Neno la
Mungu iliyojawa ndani mwake.
( Kupokea kwa mkristo anayemwamini
Yesu Kristo kunaanzia katika Roho).
Hata kitendo cha kutokuliamini
Neno la Mungu ni uzinzi tayari.
Maisha ya wokovu nilionao yatakuwa
salama kama nikiweka jitihada za kutosha
za kufundishwa Neno la Mungu ,faida nitakayoipata katika hilo maisha yangu
yatakuwa chini ya uwepo halisi wa Kimungu
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni