Jumapili, 28 Septemba 2014

MSAMAHA -28/09/2014



MSAMAHA
Msamaha ni neno dogo sana lakini lina maana kubwa  na nzito sanasana kwa jamii inayomcha Mungu.

Msamaha ni hali fulani inayotoka ndani ya mtu, vilevile ni hali ya kufuta kumbukumbu ya jambo ambalo ni baya ulilotendewa na mtu mwingine.

Maisha ya mkristo aliyeokoka akiwa anajifunza kwa Yesu Kristo, kusamehe kutakuwa ni jambo la kawaida katika maisha yake ,kwahiyo mtu kama huyu kila Baraka inayotoka kwa Mungu itayavaa maisha yake
.
Nikiamua maisha yangu yawe chini ya mwongozo wa Neno la Mungu kusamehe ni lazima bila kutazama mazingira ya kutendwa ,au mazingira ya maumivu ninayoyapata.

( Kushindwa kusamehe kunazuia mpenyo wa Baraka za Mungu katika maisha ya mkristo)

( Mkristo anayeshindwa kusamehe  ndani mwake kumejengeka asili ya kulipiza kisasi).

Ninaposhindwa kusamehe maana yake ninamzuia Mungu asiingize utetezi katika maisha yangu.

Kusamehe kunamsaidia mkristo kumwondolea hali ya maumivu  katika moyo wake ,ambayo yangeweza kumsababishia mabo yafuatayo:-
i)Kuzuia mpenyo wa Baraka za Mungu.
ii)Kusababisha moyo wa mkristo kushindwa kupokea taarifa za Mungu anaposema naye.
iii)Kumsababishia magonjwa, hii ni mbaya zaidi kwasababu moyo ukizungukwa na mambo mengi na yanayosababisha maumivu ndani yake ina athiri mfumo mzima wa mambo haya ;
a)Ufahamu
b)Mawazo
c)Fikra, hivi vitu vitatu vikiathirika katika moyo wa mwamini ndipo matatizo yanapoanzia ya kuharibika kila kitu katika maisha yake.
Moyo wangu nisipouondolea maumivu ya kujeruhiwa nikasamehe kila kitu ninachokifanya hakitafanikiwa
Luka 22:1-71

( Mkristo hata kama ameokoka akiwa hajafanyiwa  ukombozi (Deliverance) hana uwezo wa kusamehe).

Sina budi kusamehe hata kama jambo hilo limenijeruhi kiasi gani inatakiwa nisamehe ili maandiko yatimie
Mithali 25:21

Kumtendea adui yangu mema ninaonyesha uhai nilio nao katika ucha Mungu wangu,hapo ninadhihirisha zaidi kwenye uso wa Mungu kwamba nimejitoa muhanga kwaajili ya Yesu Kristo.
Kutoa msamaha ni jambo linalohitaji Neema ya Mungu kuingilia  kati
.
Kabla ya mimi kutangaza msamaha kwa aliyenikosea inatakiwa kwanza nijisamehe mimi mwenyewe ndipo msamaha nitakaoutoa utakuwa katika Roho ,kwasababu niliowakosea na kuwajeruhi ni wengi kuliko wanaonijeruhi mimi.

Nikifahamu kuna ambao mimi niliwakosea sina budi ya kusamehe kila anayejikwaa kwangu,hapo nitarahisisha maandiko kutimizwa katika maisha yangu,ndio maana Biblia ikasema wazi
                                                                           Mithali 24:17.

Mtu ambaye ni kikwazo kwangu inatakiwa niingie kwenye maombi mpaka niing’oe roho iliyomvamia hapo nitakuwa ninaitenda sawasawa sheria ya Mungu.

Ninaposamehe ndio mwanzo wa kuruhusu hekima ya Mungu kuniongoza.

( Ni aibu sana mkristo aliyeokoka kulipiza ubaya kwa ubaya).

Kushindwa kusamehe kumewafanya wakristo wengi kufarakana na baraka za Mungu.

Kila mtu atakaye jikwaa kwangu kwa namna yoyote ile nifahamu tu ameteleza ni ubinadamu ndipo nitapata wepesi wa kuachilia msamaha kwa haraka,vilevile haijalishi amejikwaa mara ngapi kwangu au amenijeruhi mara ngapi ninachotakiwa mimi kama mkristo aanayemcha Mungu aliye hai niyatende maandiko,Hata Biblia imekonyeza juu ya hili
Luka 17:3-4

( Inatakiwa nilazimishe kusamehe ili ijengeke Roho ya Mungu katika maisha yangu,na Roho ya Mungu ni Upendo).

Mimi ambaye nimeamua kutoa msamaha inatakiwa niwe na tahadhari kuu  nisije nikajikuta ninajaribiwa kupitia hilo.

NINI KIFANYIKE ILI NIWEZE KUSAHAU NILICHO KISAMEHE:
(Msamaha hauendi kwa mtu ambaye hajakiri  na kutubu kosa).

Ili niweze kusahau nilicho samehe inatakiwa kwanza mimi nitambue uthamani wa msamaha alioutoa Yesu Kristo katika maisha yangu,hapo ndipo mwanzo wa asili ya kusamehe itakapojengeka katika imani yangu.

Mwanzilishi wa msamaha ni Mungu mwenyewe,aliusamehe ulimwengu kupitia damu ya Yesu Kristo,kwahiyo kama mimi ni mcha Mungu sina budi kuyaishi maisha ya Biblia ili neno msamaha liwe hai katika maisha yangu.

MSEMO:-Nikiyatukana ninayoyashuhudia na kuyasifu mbele za watu kwamba Mungu anaweza basi hata mimi ninaonekana ni mkosaji vilevile ni mnafiki kwenye uso wa Mungu’’
   SOMO HILI LITAENDELEA WIKI IJAYO…………….

Hakuna maoni: