22/08/2014
BORESHA MAHUSIANO YAKO
NA NENO
SEHEMU YA PILI.
SWALI:Kwanini inatakiwa niboreshe
mahusiano yangu na Mungu?
MFANO:Mwili wa mwanadamu hutegemea chakula
kukua,mfano wa chakula Ugali,Wali n.k.
Jinsi mwanadamu anavyoulisha mwili wake chakula kizuri ndivyo
anavyozidi kustawi,yaani kupendeza zaidi.
Katika mambo ya rohoni imani hutegemea zaidi Neno la
Mungu,kwasababu Neno la Mungu ndio chakula halisi cha roho zetu (imani zetu),Kwa
hiyo jinsi ninaivyozidi kuzama katika kina cha Neno la Mungu ndivyo imani yangu
inavyozidi kupata hali ya ufahamu wa kumjua Mungu zaidi.
(Roho yangu ikipevuka kuhusu Mungu lazima maisha yangu
yatabadilika tu)
Nikijiona kuna mambo mengine kwenye maisha yangu ninashindwa
kuyashinda nifahamu wazi roho yangu haijapevuka kuhusu Mungu ingawa
ninaomba,kwahiyo juu ya hili ninahitaji ufahamu wa kina wa Neno la Mungu ili
niweze kupata mpenyo.
Roho ya mkristo ikipevuka,Neno la Mungu hulisikiliza katika
hali ya kiimani, na Neno hil;o huwa na uwezo mkubwa wa kufanya mabadiliko
katika maisha ya mtu.
ANGALIZO 1:Nikisikiliza Neno la Mungu analolifundisha
Mtumishi wa Mungu katika hali ya uziwi,hali ya upofu, kesho nitaposikia
anasemwa vibaya hata mimi nitakuwa mmojawapo katika kuchangia hoja.
( Nikiwa msikiaji tu wa Neno la Mungu sio mtendea kazi Neno
maisha yangu yatakuwa kikwazo kwa imani yangu,hapa au katika hili walokole
huangukia katika mambo mawili
a)Kumlaumu Mungu kwamba hajibu maombi
b)Kuwanung’unikia watumishi wa Mungu kwamba hawana nguvu za
kuwasababishia mabadiliko katika maisha yao,pia huishia kuwatukana na kuwasema
vibaya,kumbe Mungu kila kitu amekiweka wazi sambamba na maandiko Matakatifu
Yakobo 1:21-25.
( ili niweze kuishi maisha ya haki inatakiwa nitafute kina
cha ufahamu wa Neno la Mungu)
( Kama moyo wangu haumuelekei Bwana katika haki Mungu hawezi
kusema chochote kwangu)
( Kutokana na Yakobo 1:21 mkristo anayeishi maisha ya dhambi
kamwe hawezi kuendana na Baraka za Mungu,kwasababu Mungu ni haki na kweli).
( Nahitaji Neema ya kutawala, mafanikio yasije yakanitoa
katika mapenzi ya Mungu)
Agizo la Mungu katika maandiko matakatifu kuhusu wakristo
waamini ni kwamba Neno la Mungu tuliishi katika vitendo,na hii imethibitishwa
kupitia Yakobo 1:22.
Nikiliweka Neno la Mungu katika vitendo nitaambatana na Baraka
za Mungu waziwazi na hii ndiyo inayotushinda wakristo wengi na kuishia kwenye
kuumana na kulana.
Biblia inazungumzia Baraka kwa mkristo ambaye ana mambo
yafuatayo:-
i)Jambo la kwanza kuzingatia sheria ya Mungu.
Wakristo wengi wana bidii kuyazingatia mambo ya mwilini
kuliko mambo ya rohoni. Je! Mambo ya mwilini ni yapi?
i)Tamaa ya mwili
ii)Tamaa ya macho
iii)Usingizi
iv) Chakula,katika mambo haya mkristo yupo radhi akosane na
Mungu ili ayatimize,Tunahitaji Neema ya Mungu kanisa la leo.
( Mambo ya mwilini nikiyapa kipaumbele nitajikuta ninaishi
maisha magumu yasiyokuwa na mpenyo,hii ndio picha wazi ya walokole wengi,ndio maana
unawakuta wanatangatanga katika makanisa ovyo).
Maisha ya mkristo aliyeokoka ili apate mpenyo inatakiwa
atambue kwanza udhaifu alio nao,aweke juhudi za kudhibiti udhaifu huo,hapo
atakuwa ametengeneza mpenyo wa mafanikio ya Baraka za Mungu.
( Nikijifunza kwa Yesu
Kristo maisha yangu yatakuwa na usalama,Biblia imethibitisha hili Yohana 1:17).
Silaha ya mkristo aliyeokoka ni kusamehe.
Mkristo asiyekuwa na uwezo wa kusamehe huyo huitwa mtumwa wa
dhambi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni