Jumapili, 17 Agosti 2014

ANGUKO LA WAKRISTO



17-08-2014
ANGUKO LA WAKRISTO
Wakristo wengi wameanguka katika anguko la kuto kumuheshimu MUNGU, vilevile anguko la kuto kutii sauti ya MUNGU pale inaposema. 
Swali: je sauti ya Mungu au agizo la Mungu nitalisikiaje?
Kuna njia kadha wa kadha za kuisikia sauti ya Mungu:-
a). sauti ya Mungu nitaisikia kwa kusoma Biblia
b). sauti ya Mungu nitaisikia kwa kutoa muda kulisikiliza Neno la Mungu

c). sauti ya Mungu nitaisikia kupitia watumishi wake kwa uweza wa Roho mtakatifu
Lazima awepo mwanadamu aliye uvaa mwili ambaye Mungu anamwamini kupitishia ujumbe wake.
Anguko langu mimi linatokana na kudharau muongozo ninaopewa na mtumishi wa Mungu,ambaye ndiye kiongozi wangu wa kiroho katika mambo kadha wa kadha.
Wakristo wengi huwa wanasikiliza Neno la Mungu katika hali ya uziwi wa kiroho, ndio maana huwa hawana utayari wa kutendea kazi muongozo wanao pewa na Roho mataktifu katika maisha yao, hiyo ndiyo inayosababisha vile vile huathiri maisha ya wakristo wadumae katika maeneo haya:- 
     i.            Eneo la uchumi. 
ii.            Eneo la afya 
iii.            Eneo la familia kukosa msimamo 
   iv.            Eneo la ndoa kukosa kibali
( Kitendo cha kukaidi muongozo anao toa Roho mtakatifu kupitia mtumishi wake ni laana ambayo huathiri watu wengi sana ).
(Sio kusudi la Mungu niwe na maisha magumu niliyo nayo, bali ni laana inayo tokana na mimi mwenyewe kushindwa kuheshimu agizo la Mungu linalotoka katika uwepo wake).
Maisha ya wakristo wengi yameathirika sana kwasababu ya kudharau sauti ya Roho mtakatifu, jambo hili lilimkuta mfalme Sauli.
1Samweli 15
Mtumishi wa Mungu anapotoa agizo nikalikaidi nisilitendee kazi,maana yake nimekaidi sauti ya Roho mtakatifu,kwahiyo Mungu atatoa mkono wake wa ulinzi  kwangu vilevile  mkono wa Baraka.
Agizo la Mungu linapo toka huwa lina makusudi mema kwa kusanyiko la watu wa Mungu.
( Bila kuzilingana hukumu za Mungu hakuna mpenyo kabisa).
Hali ya majuto na maumivu hutokea katika maisha ya wakristo pale wanapo ikana sauti ya Mungu na kuto kuitendea kazi, kwamaana zaidi mwamini anapoikana sauti ya Mungu inayo mpa mwongozo katika maisha yake maana yake anamkana Mungu wazi wazi , na inafahamika wazi hata kimaandiko “ Mtu anapo mkosea mwenzake Mungu aweza kumsamehe, lakini mtu anapomkosea Mungu ni nani awezae kumsamehe?”.
1Samweli 15:13 Imeonyesha picha dhahiri ambavyo Sauli alivyo idhihaki sauti ya Mungu makusudi , kwasababu, hilo alilo jisifia sio agizo la Bwana alilolinena Samweli, Sauli alitendee kazi; bali agizo la Bwana ambalo Samweli nabii alimueleza Sauli linathibitishwa kwenye mstari wa tatu.
Makosa ya Sauli ya kukaidi agizo la Mungu yanathibitishwa na mstari wa tisa, na hapo ndipo mwanzo wa laana yake ilipo anzia,vilevile huwa ndio mwanzo wa laana kwa wakristo waamini katika kanisa la leo maisha yao kuharibika.
Ninapo kataa kutii agizo la Mungu ninajisababishia athari katika maeneo yafuatayo ndani ya maisha yangu:-
A.     Kuzuiliwa Baraka za Mungu: Mtu ambaye Baraka za Mungu zimezuiliwa juu ya maisha yake huandamwa na mambo yafuatayo:-
i.                    Magonjwa, hii husababisha pia mlipuko mbalimbali  wa kuathiri afya.
ii.                  Kuathirika katika suala la uchumi, hii husababishia madeni, biashara kukosa wateja,kufukuzwa fukuzwa kazi ovyo, vilevile  kukataliwa.
iii.                Familia kuambukizana roho za kurithi,vilevile roho za udhoofishaji, ndio maana unakuta familia ufukara unaanzia kwa baba, mjukuu mpaka kwa kitukuu.
NAMNA YA KUEPUKA ANGUKO KATIKA MAISHA YANGU
Ninaweza kuepuka anguko nitakapo ruhusu nia ya moyo wangu kuambatana na sauti ya Mungu inayonipa mwongozo.
Hali ya nidhamu na utii nikiviruhusu kuambatana na maisha yangu ya wokovu  hiyo ndiyo njia itakayo nisaidia kuepuka anguko lililo kusudiwa .
Nikitaka kuepuka matatizo kwa jinsi zake katika dunia ya leo ninayoishi inatakiwa nikubali kuongozwa na uwepo wa Mungu.
Hali ya nidhamu na utii ikinitawala , bahati mbaya kukatokea matatizo katika maisha yangu(majaribu), nitakapo muita Mungu kuwa mtetezi ataitika, ndio maana Mungu alisikia kilio cha nabii Esta kama ilivyo andikwa,
Esta 4:
Siku zote kiongozi wangu wa kiroho akiwa anaufahamu wa Neno la Mungu kwa kina, anauwezo mkubwa wa  kunifikisha mwisho wa maono yangu niliyonayo.
Ili maisha yangu ya wokovu yaweze kustawi inatakiwa nitafute ufahamu wa rohoni yaani  ufahamu unaotokana na Neno la Mungu,ndiyo itakuwa njia pekee ya kutoka niliko kusudiwa.
Nikitaka kupona katika anguko lililokusudiwa katika maisha yangu, inatakiwa nizame zaidi katika Neno la Mungu , ili nipate kibali cha kunivusha.
(kibali anakipata mtu anapopata ufahamu wa rohoni).

Hakuna maoni: