BORESHA MAHUSIANO NA NENO.
Hali ya
kuboresha mahusiano na Neno la Mungu ni jambo la msingi sana,kwasababu maisha
ya kila mwenye mwili yanalitegemea Neno la Mungu kama mwongozo wa kutoa njia au
kupatikana kwa wepesi katika maisha,
ndio maana utamkuta mtu anasema tumuombe Mungu hii ndio picha wazi.
Mahusiano na
Neno la Mungu ninaweza kuyapata kwa njia zifuatazo:-
A) Kutamani kujua undani wa Biblia
(Neno).
B) Kusikiliza Neno
C) Kusoma Biblia,
Hizi ndizo njia zitakazo boresha mahusiano na Neno la Mungu.
Nikitaka mahusiano yangu kuimarika ninatakiwa nisome Biblia katika
mazingira ya kiimani,ili iwe hai kwangu.
Inatakiwa wakati wa kusoma Biblia nihakikishe moyo wangu una
utulivu,dipo nitapokea hali ya uhai wa Neno la Mungu katika imani yangu ndio maana
hata Mungu alisema:-
Yohana 11:21
( Mungu hujidhihirisha kwa mtu kupitia hitaji alilonalo mtu).
Neno la Mungu linayatambua mawazo ya moyo wangu hata kabla
sijaanza kulisoma ,ndio maana ninapoanza kulisoma huwa kwa sehemu kubwa
linayatahadharisha maisha yangu ya kiimani namna ambavyo inatakiwa niishi kama
mkristo mwamini.
Inatakiwa nilazimishe suala la usomaji wa Biblia, kwasababu
Neno la Mungu ni Yesu Kristo mwenyewe, kwahiyo nikijiwekea mazingira ya kusoma
Neno la Mungu kila siku , maana yake ninamsogeza Yesu mwenyewe katika mipango
niliyonayo,vilevil maisha yangu yatapata mpenyo kwa wepesi.
Ufunuo 19:13.
Nikiwa nina bidii katika usomaji wa Biblia, ninarahisisha
hali ya kufanikiwa, vilevile ninapata nguvu ya kushinda madhaifu.
Usomaji wa Biblia unanikinga dhidi ya mawazo mabaya ambayo
shetani huyapenyeza kwa siri sana kuingia ndani ya mtu
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni