11/7/2014.
UJUMBE: VITA VYA KIROHO.
- Vita vya kiroho maana yake ni vita vya kiimani katika ulimwengu wa roho.
- Ni vigumu kushinda vita vya kiroho nikiwa sina mahusiano mazuri na Neno la Mungu, kwa sababu Neno la Mungu ndilo linalosaidia imani ya mkristo kutawala katika roho.
- Ninaweza kushinda vita vya kiroho (vita vya kiimani) kama nia ya moyo wangu imeamua kuambatana na Neno la Mungu
.
- ( Vita vya kiroho vinahitaji ukomavu wa kiimani).
- Mimi kama mkristo mwamini ninatakiwa niishi maisha ya utawala katika roho, ndio maana Biblia imesisitiza jambo hili
Wagalatia 5:25.
- Biblia inasema “Tukiishi kwa roho na tuenende kwa roho” maana yake zaidi tukiishi kwa imani na tuenende kwa imani, huu ndio unaotakiwa uwe msingi wa mkristo aliye okoka.
- Nikiamua kuishi maisha ya imani yaani maisha ya wokovu,inatakiwa niwe tayari kujinyima baadhi ya vitu fulani ,ili kuilinda imani yangu inayomkiri Yesu Kristo isijeruhike.
- ( Mkristo aliyesimama katika misingi ya kiimani ndiye mwenye uwezo mkubwa wa kushinda vita vya kiroho).
- ( Imani ikidhoofika ndani mwamini ndipo mpenyo wa dhambi hutokea).
- “Mkristo asiyekuwa na tabia ya kusamehe ana ugonjwa wa roho’’, mtu wa aina hii hata uso wake unaonyesha wazi kabisa, yaani hupoteza asili yake ya kawaida , bali huvaa kwenye uso wake asili ya hasira.
- Siwezi kupenya katika vita vya kiroho kama sijaruhusu nia ya moyo wangu kupata mabadiliko kupitia Neno la Mungu
Warumi 12:1-3.
- ( Chimbuko la dhambi ni mawazo mabaya, yaani nia mbaya ndani ya moyo).
- “ Shetani huja kumjaribu mwamini katika umbo la kiroho,kama ufahamu wangu ni mdogo katika Neno la Mungu, nitamgundua akiwa tayari amekwisha kuniangusha katika dhambi”
- Mkristo anayeishi maisha ya imani yaani maisha ya kumwamini Yesu Kristo hupata faida zifuatazo ;-
a)Utawala wa rohoni.
b)Kibali machoni pa Mungu.
c)Baraka za Mungu kwa jinsi zake.
- Nikidhibiti tabia zinazo nitoa kwenye uwepo wa Mungu hapo nitapata mpenyo wa kutawala katika roho , vilevile Mungu aweza kujifunua kwangu.
- ( Nia ya moyo wangu ikiwaza sambamba na Neno la Mungu , ni rahisi mimi kama mwamini kudumu katika mapenzi ya Mungu ).
- ( Vita vya kiroho nitavishinda iwapo utu wangu wa ndani utaamua kuishi sambamba na mapenzi ya Mungu ).
- Mkristo aliye mwamini Yesu Kristo sio wito wake kuishi maisha ya dhambi, huwa wanalazimisha tu, ndio maana huangukia katika hali ya kujihukumu na kukosa amani mioyoni mwao
Mithali 1:23-31.
- Lazima niweke mikakati ya mabadiliko katika njia zangu ili ziendane sambamba na Baraka za Mungu, ili wakati wa kujaribiwa Mungu aingilie kati.
.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni