JUMAPILI 6/7/2014.
UJUMBE : NAHITAJI KUTAMKIWA
NENO TU.
- Maisha yangu ya kiroho yatapata mabadiliko nikikaa chini ya mtumishi wa Mungu mwenye nia moja na Neno la Mungu (Yesu Kristo).
- Neno nitakalo tamkiwa kuyabadilisha maisha yangu ndani yake kunakuwa na mamlaka ya uumbaji, na mamlaka hiyo ndiyo inayo lazimisha jambo lolote kuwezekana nililotamkiwa katika maisha yangu , ndiyo maana inatakiwa niishi maisha yaliyo sambamba na Neno la Kristo.
- ( Mamlaka za waamini zinaathirika kwasababu nia ya mioyo yao imejaa hila , kwa hiyo uwezo wa kutamka neno na kuuumbika hauta kuwepo ,mtu kama huyo atamwabudu Mungu katika hali ya mazoea wala si katika uhalisia).
- Nitakapo tamkiwa Neno wakati huo huo moyo wangu uko sambamba na Neno la Mungu muujiza unaumbika papo hapo , kwa sababu moyo wangu unakuwa umeambatana na kweli ya Mungu ambayo ndiyo inayotakiwa katika maisha ya mkristo , hata Biblia imetoa tahadhari katika hilo, yaani imefunua katika ;Amosi 3:3.
- Ninapo patana na Neno la Mungu maisha yangu hufunikwa na asili ya Mungu kwa hiyo kila neno nitakalolitamka kwenye uso wa Mungu ninakuwa katika mzunguko wa mapenzi ya Mungu.
- Nikitaka mabadiliko nisafishe nia ya moyo wangu inie sambamba na mapenzi ya Mungu , hapo nitakuwa nimepatana na Neno la Bwana , kwa hiyo Baraka za kiroho zitakuwa ni sehemu yangu vilevile Baraka za mwilini zitanifuata.
- Nisipo safisha nia ya moyo wangu ikawa sambamba na Neno la Mungu nitakuwa mkristo jina tu wala si halisi, hata kitabu cha Ufunuo kimeelezea;
- Ili niwe mkristo halisi na ambaye ndiye mkusudiwa na Baraka za Mungu inatakiwa nia ya moyo wangu niielekeze katika kuyatenda mapenzi ya Mungu , hapo nitakuwa mkristo niliyejikomboa na mauti ya kiroho.
- ( Nia ya moyo wangu inatakiwa inie mema mda wote ili Baraka za Mungu zipate mpenyo wa kupitia).
- Mkristo akitaka kufanikiwa katika Baraka za kiroho na kimwili inatakiwa nia ya moyo wake isitoke nje na Neno la Mungu.
- Imani niliyo nayo haina uwezo wa kupokea lile neno nililo tamkiwa , na hii huwa inasababishwa na mambo yafuatayo katika maisha ya mkristo:-
A)Kiburi cha Uzima.
UFAFANUZI KUHUSU
KIBURI CHA UZIMA.
- Kiburi cha uzima ni hali fulani ya majivuno inayo uvaa moyo wa mkristo na kuibadilisha nia ya moyo wake kuhusu Mungu, vilevile ni hali ambayo huondoa roho ya utii kwa mwamini na kuuvalisha hali ya ukaidi.
- (Kiburi cha uzima ndicho kimeharibu nguvu ya kanisa la leo )
- ( Kiburi cha uzima kikiuvaa moyo wa mtu hata kile anachokifahamu kuhusu Mungu atakipinga).
- Kiburi cha uzima huwa kinamtoa mkristo katika mfumo wa Baraka za Mungu juu ya hili nahitaji kuwa makini sana.
ANGALIZO 1:
Madhabahu iliyo niunganisha na Baraka za Mungu na zikadhihirika katika
sehemu zifuatazo:-
i.
Pesa.
ii.
Uponyaji.
iii.
Kutolewa katika mitego mbalimbali kwa sauti ya
kinabii.
iv.
Familia yangu kuwa na afya bora.
v.
Mpenyo kuonekana katika kazi zangu na biashara
yangu, hiyo ni madhabahu ya kunyenyekea siku zote hata Biblia imezungumzia
jambo kuhusu unyenyekevu na utii:-
Webrania 13:17.
- Ninapotii mwongozo wa Mtumishi wa Mungu alionipa, Roho Mtakatifu hufurahi kupitia moyo wa Mtumishi wake,kwa hiyo maneno atakayozidi kuyatamka katika furaha ya Roho Mtakatifu yatanipa kibali zaidi cha kuvuka majaribu yote vilevile kibali cha mafanikio zidi.
B)Tamaa ya Mali
UFAFANUZI KUHUSU
TAMAA YA MALI.
- Tamaa ya mali ni roho ambayo hujeruhi kabisa mafanikio ya mkristo anayechuma na Mungu
- Nikijiona ninashindwa kutoa sadaka kanisani au fungu la kumi nifahamu wazi nimekwisha valiwa na hiyo roho, kwa hiyo nisipo funguliwa dhidi ya roho hii ninaweza kujikuta ninaangukia katika hali ya umasikini wa milele.
- Tamaa ya mali nisipo jitenga nayo ninaweza kujikuta ninaathiri mzunguko mzima wa kipato changu.
UJUMBE UTAENDELEA WIKI IJAYO…………
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni