Jumatatu, 14 Julai 2014

NAHITAJII KUTAMKIWA NENO TU. SEHEMU YA PILI.



13/7/2014:
NAHITAJII KUTAMKIWA NENO TU.
SEHEMU YA PILI.
C) TAMAA YA MWILI.

  • Tamaa ya mwili ikimvaa mkristo mwamini huwa inamtoa katika mtiririko wa Roho Mtakatifu, huo ndio unaokuwa mwanzo wa mwanzo wa tamaa  ya mwili kuthibitika katika hali ya uzinzi , kwasababu uwepo wa Mungu  unakuwa umekwisha mvuka  mtu.

                 Maana yake nini? Nikiruhusu tamaa ya mwili kuniongoza mapenzi ya Mungu ninakuwa 
                      .                          tayari nimeyavua

  • Tamaa ya mwili ina tabia ya kupofusha macho ya kiroho kwa mkristo mwamini.

  • Tamaa ya mwili inasababisha kifo cha kiroho kwa mkristo aliyejiwekea mazingira ya kumcha Mungu.

ANGALIZO 1:Hapa ni umakini tu unatakiwa , tamaa ya mwili haina cha mzee,kijana,
                        wala mtoto, kwasababu tamaa ya mwili ni roho kamili ya shetani.

  • Tamaa ya mwili huondoa heshima aliyonayo mtu kwanza kwenye uso wa Mungu,vilevile kwenye jamii iliyomzunguka,kwasababu tamaa ya mwili (uzinzi)ni jambo la kijinga ,hata Biblia imedhibitisha kauli hii

Mithali 6:32

  • Uzinzi ni roho yenye fedheha na aibu kamwe haiwezi kumpa mwamini uhuru ndani ya moyo wake wa kumcha Mungu mpaka mwamini huyo afunguliwe (delivarance)

NAMNA YA KUSHINDA TAMAA YA MWILI:

  • Ili niweze kuishinda tamaa ya mwili inatakiwa niruhusu asili ya Mungu inivae ,hapo itakuwa rahisi kupata ushindi dhidi ya tamaa ya mwili.

  • Asili ya Mungu ni Neno, kwahiyo nitakapo valiwa na asili hiyo nitakuwa tayari nimeungwa au nimekuwa asili moja na Mungu

1 Wakorintho 6:17.

  • Nikiwa asili moja na Mungu  yaani na Neno lake nitapata ushindi au nitaweza kudhibiti maeneo yafuatayo katika maisha yangu:-

                 a)Tamaa ya mwili.
                  b)Hali ya kushindwa katika roho, kwasababu kushindwa katika mwili ni matokeo ya   
                     kushindwa katika roho, ndiyo maana ukimkuta mwamini  ana hali mbaya katika mwili
                      katika roho ana hali mbaya zaidi.

  • Mkristo atakaye iruhusu nia ya moyo wake kuambatana na mapenzi ya Mungu (Neno la Mungu)huyo atakuwa ni kristo anayeishi maisha Matakatifu na hiyo ndiyo inayotakiwa kwa kila mwamini

Yohana 6:28.

  • Yohana  6:28 ni swali aliloulizwa Yesu Kristo.

  • Mkristo atakaye amua kuishi katika misingi ya Neno la Mungu ndiye atakayeweza kushinda tamaa ya mwili.

Hakuna maoni: