Ijumaa, 4 Julai 2014

USIOGOPE: SEHEMU YA PILI



USIOGOPE: SEHEMU YA PILI

Mambo ambayo shetani huyatumia kuuchafua moyo wa mwamini upoteze uvumilivu.
a) Hofu.
b) Kutokusamehe.
c) Mawazo mabaya.

UFAFANUZI WA KIPENGELE ‘B’ KUTOKUSAMEHE.

Kutokusamehe ni hali ambayo huunyima moyo wa mkristo ushindwe kutambua mapenzi ya Mungu ni yapi katika maisha yake.

Mkristo ambaye hana uwezo wa kusamehe huyo haishi na Mungu ndani mwake, hata kama anashinda kanisani usiku na mchana.

Mtu mwenye uwezo wa kusamehe ni yule ambaye moyo wake umeamua kuambatana na Neno la Mungu.

Kama moyo wangu unaambatana na Neno la Mungu msamaha nitakao utoa ndani mwangu utakuwa unatoka rohoni yaani kwenye nia ya ndani  ya moyo wangu.

( Haijalishi nimetendewa nini cha kuumiza , bali inatakiwa niwe mtu wa kusamehe na kusahau ndipo Baraka za Mungu  zipate mpenyo wa kuingia katika maisha yangu).

( Kuna mambo mengi sana yanajifunga katika maisha ya waamini ingawa wanaomba usiku na mchana hakuna mafanikio , hii  hutokana na kushindwa  kusamehe  na kusahau).

ANGALIZO  1: Maisha ya dhambi hapa chini ya jua husababisha wakristo kufa mapema kabla ya wakati ambao Mungu amekusudia , ndio maana mkristo anayeishi katika dhambi hana ufahamu
wowote kuhusu mapenzi ya Mungu.

Nikiwa mkristo ambaye ninatabia ya kusamehe na kusahau maana yake ninakuwa ninaishi sambamba na mapenzi ya Mungu, jambo hili hata maandiko yamesisitiza zaidi ;
Marko 11:25,26.

Jinsi ninavyo ruhusu moyo wangu kutangaza msamaha dhidi ya walionikosea au kinikwaza vile vile kiniumiza , maana yake ninakuwa ninaruhusu mapenzi ya Mungu kuingilia kati katika maisha yangu ya wokovu, vilevile Mungu ataniatamia.

Kutokusamehe ni roho ambayo inatakiwa niikemee katika maisha yangu , kwasababu hali hii ya kutokusamehe  husababisha ufahamu wa rohoni wa mkristo mwamini kujifunga.

Mimi kama mkristo mwamini inatakiwa hali ya kusamehe iwe ni tendola kila siku katika maisha yangu , hapa ninaweza kusema ninadumu katika mapenzi ya Mungu, kwasababu mtu ambaye hasamehi amefarakana na imani ya Yesu Kristo.

Ninapotangaza msamaha hatakama jambo hilo limenijeruhi kwa kiasi gani , ninakuwa ninamruhusu Mungu mwenyewe kuingilia kati;
Warumi 12:14-21.

 ( Ninapo samehe ninaonyesha wazi asili ya Mungu inayoishi ndani mwangu )

( Kusamehe huwa hakutazami maumivu,bali hutazama mapenzi ya Mungu).

Kitendo cha mimi kusamehe maana yake ninamkabidhi Mungu kutoa maamuzi ya haki.

(Siku zote hukumu ya kweli na ya haki ni ya Mungu peke yake).

Suala la kusamehe liwe ni tendo endelevu katika maisha yangu ya wokovu pasipo kukumbuka maumivu ya jana, hapo nitakuwa mkristo anayeishi katika haki ya Mungu kweli kweli.

( Kusamehe ni upendo)

Siku zote mtu anayekuchukia mtendee mema, mwisho wa siku roho yake itaona aibu.

Upendo ulioko ndani ya mkristo utaimarika zaidi atakapo chukua hatua za kuutamka mara kwa mara”.

Hakuna maoni: