Jumatatu, 16 Juni 2014

MKAKATI WA KUJIENDELEZA KIIMANI-juma pili 15-06-2014

MKAKATI WA KUJIENDELEZA KIIMANI

- Inatakiwa nijiendeleze kiimani kwasababu Imani za wakristo wengi zime poa kwasababu ya kujeruhiwa na mambo ya mwilini.

- (Imani yangu ikiisha jeruhika inapoteza mawasiliano na Mungu katika roho kwasababu Imani ni daraja la kumuunganisha mwamini na Mungu)

- (Mkakati wa kujiendeleza kiroho utaisaidia roho yangu kupata uwezo wa kupambanua kati ya sauti ya Mungu na roho zidanganyazo)

-Nina shindwa kutumia mamlaka niliyo nayo kwasababu ninawaza vibaya ,kwa hiyo nikiwaza vibaya nitaamini tofauti.

- Nina shauriwa kusoma Neno la Mugu ili ufahamu wangu uwaze sambamba na Neno la Mungu linavyo waza hapo imani niliyo nayo nitakuwa nimeiponya.

- Imani yangu imejeruhiwa na mambo ya mwilini, ndio maana imepoteza uwezo wa kunitoa katika dhiki niliyo nayo.

Kuna mambo mawili makuu yanayo ijeruhi imani za wakristo waamini.

a) Tabia za kale (asili)

b) Mawazo mabaya

Hivi viwili vina athiri Imani za wakristo kwa Mungu

- Mimi ninaye mwamini Yesu kristo, mlinzi wa maisha yangu ya mwilini na rohoni ni Imani, hata Biblia imeyathihirisha hayo,

1Petro1:5

-Ninapo ijeruhi Imani yangu kwa kuto kutii na kwa kutokufuata muongozo wa Roho mtakatifu ninafungua mpenyo wa Imani yangu kushambuliwa.

- Mimi kama mkristo mwamini maisha yangu ya rohoni na mwilini hulindwa kwa Imani, kwa hiyo kama nikiruhusu Imani yangu iwe dhaifu hapo ndipo shetani atakapo pata mpenyo wa kunidhoofisha katika maeneo yafuatayo:-

A) Kiuchumi. Katika suala la uchumi kutatokea mambo haya

i)Kuona uchungu wakati ninatoa fungu la kumi, yaani kuona ile pesa ni nyingi mno

ii)Kupoteza hamu ya kutoa sadaka kanisani, yaani ninaweza kuja na sadaka vizuri lakini wakati wa kutoa nisinyanyuke.

-Kesi ya uchumi haihitaji kuombewa bali inatakiwa mimi kama mkristo mwamini nitembee katika formula ya utoaji na jambo hili limethibitishwa wazi katika Malaki 3:8-12

Angalizo no1

-Nikitoa zaka au michango mbalimbali kwenye madhabahu yenye ugomvi na Mungu itanigharimu sana uchumi wangu yaani hata kufilisika kabisa nikawa sina kitu.

Nisipotoa fungu la kumi kiuaminifu ninaijeruhi Imani yangu ipoteze muunganiko na baraka zangu na Mungu, ndio maana maisha yangu hayaendi juu.

- ( Mimi ninaye chuma na Mungu maana yake ninategemea ufalame wa Mungu kunibariki)

'' (Yesu nisaidie pesa isinitoe kwenye uwepo wako kwasababu ninajaribiwa kupitia kile ninacho kipenda,kama mapenzi yangu yako kwenye pesa nifahamu ndiko anguko langu lilipo)''

-Mafanikio niliyonayo leo hayajalishi niya aina gani, kuna chanzo , na chanzo cha chaweza kuwa kimegawanyika katika sehemu nyingi

a) Katika kudhoofika kiimani, hiyo huwa ni njia rahisi ya shetani kumwingia mtu na kumletea maumivu.Pia maumivu yamegawanyika katika sehemu zifuatazo

i) magonjwa yasiyo tibiwa kwa dawa za kawaida

ii) Madeni

iii) Kukosa kibali na mengineyo

Angalizo no2

Nirahisi nikaruhusu tatizo kuingia, ila kunagharama ya kulitoa tatizo likiisha komaa , kwahiyo hapa inatakiwa niwe makini sana katika maisha yangu ya kiroho.

b) Kudhoofika Kiuchumi

Kudhoofika kiuchumi kutaniathiri seemu hizi katika maisha yangu

i) Ufahamu wangu kushindwa kuzalisha wazo jipya yaani nikabaki katika hali ya mnung'uniko na malalamiko.

ii) Kupoteza kabisa mzunguko wa pesa katika maeneo yote yanayo niingizia kipato

iii) Kila kitakachoingia kushindwa kuitosheleza familia na majukumu mengine kimaisha , hayo

ndio mapigo yanayo ambatana na mkristo naye ishi nje na formula ya maandiko matakatifu (Biblia)

NINI KIFANYIKE ILI IMANI ISIJERUHIKE

-Nikita Imani yangu isijeruhike inatakiwa nianze kudhibiti nafsi yangu.

-Mkisto mwamini anapojitahidi kuidhibiti nafsi yake, huwa anaiandalia mazingira ya kukua kwa kasi sana Imani yake kwasababu mambo yaliyo jaa ndani ya nafsi ndiyo yanayo athiri mfumo wa utendaji kazi wa Imani ya mkristo anaye litegemea Nenola Mungu.

-Nikitaka kuidhibiti nafsi yangu inatakiwa nifahamu ndani ya nafsi yangu kumebeba nini?
Mambo ambayo nafsi yangu imebeba

a) Hisia, ninafahamu wazi hisia huja hisia huondoka

b) Akili

c) Utashi

-Akili na utashi huwa vinategemeana kwasababu vyote huwa katika mfumo wa kunasa na kuelewa.

-Nikisoma Biblia hisia itaondoka itasimama Imani, nikisikiliza Neno la Mungu utashi wangu utanasa , akili yangu itaelewa,italiweka Neno la Mungu katika mfumo wa kukua zaidi katika misingi ya kiimani.

Nikiisha idhibiti nafsi yangu matendo ya mwilini yatakosa mguvu kwasababu Biblia imeielezea wazi matendo ya mwilini na ndiyo yanayo mfanya mtu akose haki yake kwenye uso wa Mungu "Ee Yesu nisaidie mimi mtumishi wako" Wagalatia 5: 19-21

-Matendo ya mwilini yaliyo nenwa katika Wagalatia5:19-21 kwa 100% ndio yanayo ifanya Imani ya mkristo ipoteze muungniko na Mingu, na hapo mkristo asipo jigundua mapema maisha yake ya ucha Mungu yatakuwa yamejengeka katika hisia za kibinadamu , vile vile utashi wake utakuwa unanasa zaidi mambo ya mwilini yaani ya kidunia , hapo ndipo mkristo huzitegemea akili zake mwenyewe katika maisha yake ya kiroho , wakati Bwana alikwisha kutoa angalizo juu ya hilo katiaka mithali 3:5

Swali: Kwanini Bwana alisema tumtegemee kwa mioyo yetu, tusimtegemee kwa akili zetu?

Jibu : Kwasababu mawazo ya mwanadamu siku zote vile vile na akili yake huwaza ubatili, ndio maana Biblia inazidi kuyafua zaidi katika Zaburi 19:14.

Utakatifu wa mkristo aliye okoka huja baada ya mkristo huyo kuwaza kama Neno la Mungu linavyo waza.

Hakuna maoni: