<<<<<SUNDAY SERVICE 01/06/2014>>>>>
NAMNA AMBAVYO IMANI INATENDA KAZI (SEHEMU YA PILI)
-Imani inatenda kazi na mkristo aliye simama katika kweli ya Mungu.
-Nikiwa ninajuhudi katika kufunga, nikawa na juhudi katika kuomba, lakini kama sijasimama katika kweli ya Mungu, ni vigumu maisha yangu kubadilika hata kama nitaombewa.
-Kinacho badilisha maisha ya mkristo akanawiri, ni mkristo huyo kuifahamu kweli.
-Kuifahamu kweli inatokana na juhudi za mwamini kuzama kwenye kina cha maarifa ya Neno la Mungu.
-Swali: Je, kweli ni nini? Hata Yesu Kristo neno hili alilitamka katika Yohana8:31,32.
-Neno la Mungu ndilo linalo zaa kweli, kwasababu Mungu ni Neno, na hii ipo wazi katika Yohana1:1-3.
-(Mamlaka ya wakristo waamini zimepoa kwasababu zimetoka nje na kweli ya Mungu.
-Imani= Neno
-Rho= Kweli
Mtu anaye tembea katika kweli maisha yake huwa rohoni muda mwingi.
-(Imani ndiyo inayo leta muunganiiko wa mkristo kudumu katika roho).
-(Neno la Mungu ndilo linalomfanya mkristo kuishi maisha ya kweli)
-Nikitaka kudumu katika kweli vilevile katika misingi ya rohoni inatakiwa nijiwekee mikakati ya usomaji wa Biblia.
-Nini maana ya Biblia?
Biblia ni mkusanyiko wa vitabu vingi vilivyo andikwa na mitume na manabii kwa uvuvio wa Roho mtakatifu,vilevile Biblia ni kitabu cha ajabu.
-Biblia inanifahamu hata kama mimi ninaisoma. ndio maana inauwezo wa kunielezea jinsi mimi nilivyo, vilevile ina uwezo wa kunifunulia siri za Mungu,kwahiyo nikizama katika kina cha Neno ambayo ni Biblia, ndani mwangu kunaumbika asili ya Mungu ya uumbaji.
-Biblia ni kiabu kinacho nipa muungozo wa namna ya kuzungumza na Mungu katika maombi,kwahiyo nkizama katika kina cha Neno hili nikaingia katika maombi nitapata mtiririko wa Roho Mtakatifu.
-Kama sijajijengea mazoea ya kusoma Biblia na kusikiliza Neno la Mungu nitakapo ingia kwenye maombi, maombi yangu yatakosa kibali kwenye uso wa Mungu, kwasababu nitakuwa ninaomba nje na Roho Mtakatifu,hata Biblia jambo hili imelifunua
Mithali28:9
-Wakristo waamini maombi yao hayajibiwi kwasababu hawasimamii misingi ya maandiko wakati wa kuhojiana na Mungu,bali huongozwa na hisia zao zinazo toka katika kukariri baadhi ya maneno anayo yasikia kwa mwenzake,ndio maana ndani ya kanisa mmoja akisikika anasema ...tatatataataaataa...kanisa lote linaiga hivyo, hii ndio mbinu ambayo shetani anayo itumia kuvunja makanisa.
-Nikizama kwenye kina cha Neno katika kulisikiliza , kulisoma, kulitendea kazi kina changu cha maarifa ya rohoni kitaongezeka kwa kasi, yaani nitakuwa ni mwamini niliye onganishwa na baraka za Mungu moja kwa moja
BY PASTOR BAB G POWER @Kapernaum church, Arusha
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni