MKESHA
HAITAKIWI NIKATE TAMAA
Ø Kukata tamaa huwa kuna onesha wazi hali ya kushindwa kwa mwamini
na hii hali huwa inadhihirika kupitia maeneo yafuatayo:-
Ø Manung’uniko ndani ya kinywa cha
mwamini,kupoteza kabisa hali ya kukiri ushindi au inawezekana.
Ø Kupoteza hali ya kujihudhurisha
kwenye uso wa Mungu
Ø Mfano:Siku za Juma pili vilevile mkesha na vipindi vingine vinavyohusiana na mafundisho ya Neno la Mungu
ANGALIZO:Mkristo
ambaye amefarakana na kweli ya Mungu kamwe hawezi kutoa neno la kunijenga,zaidi ya kuniingizia
roho ya uasi
Ø Kukata tamaa ni hali ambayo humvaa
mkristo katika mazingira yafuatayo:-
a)Pale ambapo mkristo atatazama
mazingira anayoyapitia au yaliyo mzunguka
Ø ( Ili wokovu nilio nao nikitaka ubaki
salama haitakiwi nitazame mazingira ninayoyapitia hatakama yana ugumu kiasi
gani).
Ø ( Mkristo anapokata tamaa huwa anaungana
na ufalme wa giza kuukufuru ufalme wa Nuru “Yesu nisaidie nisiwe mmoja wapo”).
Yoshua 1:6-7.
Ø Neno la Mungu linavyosema “Uwe hodari
na ushujaa”ni tahadhari mbele niendako hakuna urahisi bali ni kupambana, yaani
ni kukabiliana na changamoto(majaribu) bila kukata tama.
Ø Nikitaka mwamini mwenzangu ashinde
vita vya kiroho inatakiwa nimfariji kwa maneno ya imani.
Ø ( Ushindi wa mkristo ni namna anavyokiri)
Ø ( Mtu ambaye amekata tamaa maana
yake, mbele anakokwenda haoni mpenyo)
Ø Mimi kama mkristo mwamini lazima
nifahamu kwamba,kila jambo lina wakati wake chini ya jua,cha msingi nidumu
katika mfumo wa kujihudhurisha kwenye
uso wa Mungu, ili wakati wa kubarikiwa ukifika unikute ndani ya uwepo wa Mungu.
Mhubiri 3:1-8
Ø Mapito ninaoyapitia leo sio mapito
nitakayo yapitia tena kesho ,bali ya leo yatakuwa historia ya kesho ,kinacho
takiwa ni kudumu katika misingi ya ucha
Mungu mpaka yatakapo timia.
Ø Mungu ni rafiki wa mwamini ambaye ana
roho ya uvumilivu, kwa sababu mtu
mvumilivu hana historia ya kukata tamaa,bali hutazama mapenzi ya Mungu mpaka
yatakapo timia.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni