BIBLE STUDY
MAZIGIRA YA UOMBAJI
Maombi ni
mahojiano kati ya nafsi mbili,nafsi inayoishi mwilini vile vie na nafsi inayoishi rohoni,yaani
nafsi ya Mugu na nafsi ya mwanadamu.
Nafsi hizi
mbili huwa zinaungana kupitia imani iliyo simama katika misingi ya Neno la
Mungu .
Nafsi ya
mwanadamu ni vigumu kuishawishi nafsi ya Mungu kuleta mabadiliko ka
mkristo mwamini kama mkrosto huyo hajaunganisha nafsi yake na Neno la Mungu
kuwa kitu kimoja.
Nafsi ya
mwanadamu chimbuko lake ni Mungu, hili jambo alilithibitisha Yesu Kristo
mwenyewe
Yohana 1:14.
Mimi
nimeumbwa kwa Neno la Mungu, ndi maana intkiwa niishi maisha ambayo yanaendana
na muongozo wa Neno la Mungu hii itanisaidia
hali ya utakatifu kuumbika ndani mwangu
Hali ya
mwamini kukosa mtiririko wa maombi inatokana
na upungufu wa kina cha Neno la Mungu
ndani yake,hii husababisha madhara ya imani ya mkristo kuwa dhaifu.
Imani ya
mkristo ikiishakuwa dhaifu ianakuwa haina uwezo tena wa kuhojiana na nafsi ya
Mungu katika roho au wakati wa kuomba,
jambo ambalo litamkuta mkristo ni kuomba
sambamba na mapenzi yake, wala si
mapenzi ya Mungu “Haya maombi hufanywa na
asilimia 75 za walokole,kuomba
sambamba na mapenzi yao binafsi, ndio maana maombi yao hayana matunda”
Mathayo7:7-11
Maneno
yaliyoandikwa katika Mathayo 7:7 yatakuwa hai vilevile yataleta mafnikio kwa
mkristo ambaye ataamua kuinyenyekeza nafsi yake kudumu katika mapenzi ya
Mungu,juu ya hili hakuna anguko
Nikiishi
katika mapenzi ya Mungu, ninalo likusudia kwa Mungu litatimia hata kama
litachelewa.
Mkristo
akitaka kufanikiwa katika maombi anayoomba kila siku kwenye uso wa Mungu,anatakiwa afanye yafuatayo:-
A)Maombi yake ayaweke katika vitendo
Mfano
wa kuweka maombi katika vitendo
i.
Ninaomba
kupata kazi lazima nichukue hatua za kufuatilia kazi kwenye makampuni, sio kuomba kupata kazi , nikalala nyumbani eti zita nifuata ,huo ni
uksefu wa ufahamu
ii.
Ninaomba
nishinde dhambi, lazima nichukue hatua za
juzuia mazigira yanayo nisababishia dhambi
(Nikiigeuza
hoja yangu ninayoomba kwenye uso wa Mungu katika vitendo itazaa matunda )
(Imani yangu
itakuwa hai zaidi nitakapo ijengea mazingira ya kusikiliza Neno la Mungu mara
kwa mara yaani kulifanya Neno kuwa sehemu ya maisha yangu ya kila siku, kama
nimnavyo kula chakula cha mwili kila siku(ugali na maharage)
Amen
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni