USIOGOPE KUJARIBIWA
-Majaribu ni aina Fulani ya changamoto anayokutana nayo mwamini katika maisha yake ya ucha Mungu.
-Ni vigumu kupanda ngazi nyingine ya kiroho bila kujaribiwa ,kwa hiyo
majaribu ni sehemu ya kukuza imani ya mkristo (kuimarisha).
-Majaribu yananipima uwezo wa ufahamu wangu nilionao katika maandiko (katika kumwamini Mungu).
-( Inatakiwa niendeleze roho yangu ili maisha ya mwilini niliyonayo yaongozwe na maisha ya rohoni, hapo itakuwa rahisi kupita kila mapito bila kukata tamaa au kumkufuru Mungu).
-Wakristo wengi huendeleza akili zao kuliko roho zao wanapokutana na
changamoto za kiroho hushindwa kwa sababu hawana ufahamu kabisa na
mambo ya rohoni watu wa aina hii kibiblia huitwa wadadisi au watafiti
na Biblia imewazungumzia kwenye kitabu cha Tito 1: 16.
-Nikitaka kushinda vita vya kiroho (majaribu) inatakiwa nimtafute Mungu katika maarifa .
-Mkristo bila kujaribiwa ni vigumu kutambua ufahamu nilio nao katika kumwamini Mungu.
-Majaribu niayo kutana nayo huwa yanaruhusiwa kwangu makusudi, lengo ni
kunisaidia mimi kama muamini kubaki katika mfumo wa ucha Mungu,
kwasababu mambo yakiwa safi kila eneo hata Mungu nitamsahau.
Yakobo 1:1-4
( Ili niweze kushinda matatizo ya kiroho inatakiwa nitafute ufahamu wa kutosha wa Neno la Mungu)
( Kumcha Mungu ni jambo la maana sana kuliko fedha na dhahabu)
-Sifa ya mtu mvumilivu hakati tamaa kamwe wala hawezi kujiandalia
mazingira ya kukata tamaa, kwasababu anakuwa ni mtu mwenye msingi wa
kiimani.
-Wakristo wengi wakati wakujaribiwa humtukana Mungu na
kumkufuru Mungu na hii hutokana na kukosa hali ya ufahamu wa maandiko
matakatifu katika maisha yao.
-Ufahamu wa maandiko matakatifu ndio silaha ya mkristo muamini dhidi ya mambo yafuatayo:-
A) Magonjwa. Hili jambo limethibitishwa pia wazi kimaandiko
Mithali 4: 20-22
( Kujifunza Neno la Mungu kutanipa ufahamu wa kutawala maeneo nyeti sana katika maisha ya mwanadamu).
i. Maisha ya rohoni.
Katika maisha haya ya rohoni nitapata uwezo wa nafsi yangu kuzungumza na nafsi ya Mungu.
ii. Kutawala katika misha ya mwilini
Hapa nitapata faida ya kuvuka majaribu bila kuathirika kiimani.
-Mithali 4:20-22 ni maneno ya Mungu kwa mwandamu mwenye mwili asije
akaathirika na magonjwa yatakayo mtoa nje ya maisha rohoni.
Mithali 1:25-29
-Mbinu anayoitumia shetani kuathiri maisha ya wakristo waliookoka ni
kuipiga mioyo yao na kupoteza hali ya utulivu ; moyo ukiisha poteza
utulivu Imani ita yumba ; Imani ikiyumba ndio mwanzo wa mambo
yafuatayo:-
i. Kupoteza kibali yaani hali ya kukubalika kwenye uso wa Mungu vilevile kwenye uso wa wanadamu pia
ii. Magonjwa yasiyo tibika kwa dawa za kawaida
Mfano: -Presha
-Kisukari
-Kansa
-Ukimwi
-Pumu
-Tauni , n.k
-Haya ni magonjwa ya kiroho na mgonjwa haya hutibiwa kwa Neno la Mungu
B) Umaskini.
Ni hali ambayo humvaa mkristo pale anapo uibia ufalme wake anao uabudu.
-Katika suala la uchumi ni jambo ambalo halihitaji maombezi bali ni
jambo linalohitajika kwa mwamini kufuata formula ya maandiko mtakatifu
yanavyo eleza katika sehemu za matoleo.
-( Mkristo akitoka nje ya formula ya utoaji,shetani huanza kushikilia uchumi wake na kuuelekeza katika maeneo yafuatyo :-
i. Kutibu magonjwa na hiyo huwa ni suala la mara kwa mara ilimradi tu afilisike .
ii. Kuingia katika madeni asiyokuwa na utayari nayo.
iii. Kujikuta anaangukia katika hali ya kudhulumiwa kazi atapata, lakini atadhulumiwa.
iv. Kutwishwa majukumu kuliko kipato alicho nacho,ilimradi afilisike
A. Nikitaka kuyavuka majaribu bila kuathirika kiimani
-Nikitaka kuyavuka majaribu bila kuathirika kiimani ninatakiwa itafute
hali ya ufahamu zaidi wa kibiblia ,na hali hii ya ufahamu wa kibiblia
ninaweza nikaupata katika mazingira yafuatayo :-
i. Kujisomea Biblia , hapa katika kujisomea
Biblia nitapata faida :-
a. Roho yangu kupata uwezo wa kupambanua kati ya sauti ya Mungu na roho zidanganyazo
( Kusoma Biblia kunamsaidia mkristo kukua katika Neema ya Mungu).
ii. Kisikiliza Neno la Mungu.
-Kusikiliza Neno la Mungu kutausaidia moyo wangu kupata hali ya
utulivu vile vile kukua katika misingi ya kiroho kwasababu Biblia
imeyathibitisha hayo wazi katika Warumi 10:17
-Moyo wa mkristo
ukiisha pungukiwa na Neno la Mungu Imani inadhoofika.
-Nikitaka kuishi maisha ya utajiri , maisha ya baraka,
maisha ya afya njema, maisha ya kuto kupungukiwa kitu, maisha ya kuwa
na kibali kwa Mungu na wanadamu inatakiwa niutendee haki moyo wangu
kuupa chakula cha kiroho ambacho ni Neno la Mungu ( Bibilia).Hapo
nitakuwa ninaitwa mkristo anayedumu katika misingi ya kiimani katika
ucha Mungu.
-Jinsi ninavyo uhudumia mwili wangu kwa chakula
yaani asubuhi ukinywa chai, mchana ukala chakula na jioni ukala chakula
pia, ndivyo ambavyo nahitajika kuuhudumia moyo wangu kuulisha Neno la
Mungu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni