UJUMBE WA LEO. INATAKIWA NITAMBUE MAANA HALISI YA MFUNGO
Kuomba ni mbinu ya kiroho inayousaidia moyo wa mwamini kupata utulivu wa kumsikia Mungu, ndio maana nikiwa katika kipindi cha mfungo inatakiwa mambo haya muhimu.
A)Nihakikishe nina muda wa kutosha wa kusoma Neno la Mungu
Tunapata ugumu wakati wa kuomba kwasababu ya kukosa msingi wa Neno katika mioyo yetu)
.B) Nihakikishe nina muda wa kulisikiliza Neno,maana katika kusikiliza ndiko imani inapopata nguvu,Hili jambo hata Maandiko Matakatifu yamesema Warumi 10:17.
(Katika kusikia ndiko kunakofanya imani yangu iongezeke zaidi katika kuamini).
C) Nihakikishe nina muda wa kuomba,na katika hili inatakiwa umakini sana kwasababu_ _ _(Kumbuka maombini mazungumzo kati ya mtu na Mungu,na kwa mujibu wa Biblia Mungu anasikiliza maombi ya mtu wa aina hii Zaburi 51 6-14
( Kinachozuia maombi ya mtu yasipate mpenyo ni dhambi iliyoatamia maisha ya mtu).
ANGALIZO:Dhambi yoyote ambayo mkristo hajaitubu inakuwafungamana naye mpaka aitubu ndipo inatoweka.
Mfungo webye nguvu na unaoleta matunda kwa mwamini ni mfungo ambao
Mungu ameuzungumza kupitia kinywa cha Nabii Isaya58:6-14 ,Yakobo 1:26,27
Mungu ameuzungumza kupitia kinywa cha Nabii Isaya58:6-14 ,Yakobo 1:26,27
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni