Jumapili, 3 Januari 2016

AMINI NENO LA KINABII ULILO TAMKIWA LITATIMIA

Somo la leo :

AMINI NENO LA KINABII ULILO TAMKIWA LITATIMIA.

- Biblia ni kitabu kilicho sheheni matamko ya kinabii, vile vile ni kitabu ambacho kina Roho ya kinabii ndani yake.


- Kwa maana zaidi ninapo kuwa ninaisoma Biblia nina pewa unabii wa maisha yangu, ndio maana Biblia ina nifahamu mimi hata kama mimi ninaisoma.

- Maneno yaliyo andikwa ndani ya Biblia yanafanya kazi kwenye ulimwengu wa Roho, ndio maana matokeo yake huwa tunayadhibitisha katika mwili.

- Yohana 1:14 ni picha halisi ya Neno ambavyo linaweza kudhibitisha matokeo halisi katika hali ya kimwili. 

- Neno hili si hadithi zilizo tungwa kwa werevu wa ufahamu wa watu fulani, bali ni udhihirisho wa utukufu wa Mungu katika kufikisha kusudi lake kwa watu alio waridhia, udhibitisho wa Neno kuwa mwili ni matamko ya kinabii ambayo walifunuliwa kabla ya hata kizazi hizi hakijakuwepo, maana yake nini? Tamko la kinabii litatimia hata kama litachelewa.
Isaya 7:14, vile vile tamko la kinabii linao uwezo mkubwa wa kubadilisha jambo lolote, muda wowote na wakati wowote, cha msingi ni kudumu katika Imani.

Neno la kinabii nililo tamkiwa inatakiwa niliatamie katika mazingira yafuatayo ndipo litatimia:-
 i). Kudumu katika uwepo wa Neno la Mungu 
 ii). Kukaa chini ya muongozo wa Neno la Mungu 
 iii). Kutafuta ushauri wa Neno la Mungu katika mahitaji yangu yote
 iv). Kuelekeza maombi yangu sambamba na lile tamko nililo tamkiwa ili kuwepo na uvuvio wa nguvu ya Mungu kulinda hilo tamko
 v). Kutubu haraka pale ninapo gundua nimeteleza au nimemkosea Mungu.

- ( Mshauri wangu mkuu inatakiwa awe ni Neno la Mungu kwa sababu Neno la Mungu halina kigeugeu wala haliwezi kunisimanga, lakini mwanadamu aweza kukusaidia baadae akakusema vibaya. )

- Neno la kinabii ninalo tamkiwa ndani yake huwa kuna uvuvio wa nguvu ya Roho Mtakatifu, 

- Ili niweze kuliatamia mpaka litimie inatakiwa nizame katika kina kirefu cha Neno la Mungu ili ndani mwangu kuwe na muunganiko halisi kati ya mimi na Roho Mtakatifu, hapo adui hawezi kupata mpenyo wa kuathiri Neno hilo la kinabii katika maisha yangu.

Nini kifanyike ili Neno hili la kinabii liendelee kuwa hai kwangu:

- Neno la kinabii linaweza kupata wepesi wa kudhibitika kwangu iwapo mimi na Neno la Mungu ni wamoja, hili jambo hata kitabu cha Wakorinto kimezungumza. 
1 Wakorinto 6:17

- Kusudi la Mungu ni nini? 
Ni kuliamini Neno lake na kulitendea kazi Neno lake.

- Ili tamko la kinabii lipate wepesi inatakiwa nijiongeze katika hali ya kiimani, na wote tunafahamu chanzo cha Imani ni kusikiliza Neno la Mungu .

- Katika suala la baraka za KiMungu katika maisha yangu inatakiwa nitamkiwe na mtu wa Mungu aliye valishwa Neema na Mungu juu yake.

- Neno la Nabii ni sheria halidondoki lazima litatimia , hii ina maana kwamba alicho kusudia Mungu kitimie kwako hakiwezi kukengeuka hata kama kutakuwa na vikwazo vya aina gani, bali vitatimia kwa wakati wake,cha msingi ni kuvumilia na kunyenyekea chini ya uwepo wa Mungu.

- Kinacho zuia matamko tunayo tamkiwa na watumishi wa Mungu yasitimie kwetu, ni maisha mabovu tunayo ishi sisi yaliyo kinyume na mapenzi ya Mungu.

- Ikiwa mimi ni mtu mwenye ufahamu, kila tamko ninalo litamkiwa inatakiwa nilipalilie kwa kumtolea Mungu sadaka, kwa sababu sadaka ni Agano kati ya mtu na Mungu. 
1Wafalme 17:9-16

- Neno la kinabii hutamkwa katika kinywa cha Mtumishi wa Mungu kwa njia ya uvuvio wa Roho Mtakatifu, ndio maana Neno hilo huwa na mamlaka ya kulazimisha kitu kikatokea kwa wakati ambao Mungu ameukusudia.

SWALI 
Sababu ya Eliya Mtumishi wa Mungu kutamka Neno la kinabii katika nyumba ya mwanamke mjane ni nini? 

JIBU 
- Ni Imani ya utoaji aliyo idhihirisha mwanamke mjane bila kumzuilia Mungu nafsi yake hata kama alikuwa na kidogo.

- ( Ninapotii Neno la Mungu kupitia kinywa cha Nabii lazima maisha yangu yatacheka ).



Hakuna maoni: