Somo la leo 1/1/2016
MUONGOZO WA ROHO 2016
- Watu wengi wamepoteza uaminifu kwa yule ambaye ndio chanzo cha baraka zao, ndio maana maisha ya wakristo wengi hayaendi
mbele huwa yanakumbwa na vikwazo vingi, na hii mara nyingi inasababishwa na wakristo walio wengi hawataki kuishi maisha ya haki, bali maisha ambayo huishi ni ya hila na visasi.
- ( Ukweli ni kwamba maisha ya hila na visasi huwa yanafunga muunganiko wa baraka za Mungu na mtu, ni sawa na kusema ana jina lililo hai lakini amekufa ) Ufunuo 3:1
- Mwanadamu anaishi katika mazingira ya aina mbili kwa wakati mmoja
Maelezo kuhusiana na point hii,
- Yaani anakuwa ameuvaa mwili lakini Kwa wakati huo huo anaishi katika ulimwengu wa Roho, ndio maana Biblia inasema, Waebrania 11:6 lakini pasipo Imani haiwezekani kumpendeza Mungu kwa maana kila mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba yeye yupo pia huwapa thawabu wale wamtafutao, hii iko wazi kwamba Mungu anazungumza na mimi nilioko katika Roho ambapo kwa wakati huo huo nimeuvaa mwili.
- Kinacho leta shida ni nini mpaka unakuta watu tumeokoka lakini bado tunaishi maisha ya hila na visasi.
- ( Inatakiwa nijiboreshe mimi wa kiroho niwe hai ndipo mapenzi ya Mungu yatatimia, kwa sababu baraka za Mungu zinaanzia kwenye ulimwengu wa Roho kabla ya kudhihirika mwilini, ndio maana inatakiwa kwenye Roho nichunge nisipoteze muunganiko Wangu na Mungu. )
Namna ya kusamehe kirahisi,
- inatakiwa mimi wa kiroho ambae wakati huo huo niko mwilini inatakiwa nitangulie kusamehe kabla ya mimi wa kimwili, huo msamaha utakuwa katika Roho na kweli.
Namna ya kujijua mimi wa kiroho kwamba nimesamehe:
1. Lile jambo nililo lisamehe haliwezi kuzunguka tena kwenye ufahamu wangu.
2. Lile jambo nililo lisamehe siwezi kulizungumzia tena kwenye kinywa changu kwa mtu mwingine, kwa maana zaidi mimi wa kiroho Nikisha samehe inatakiwa niulinde mlango wa moyo Wangu usije ukarejesha kumbu kumbu ya kile ambacho nimekwisha kisamehe, ndio maana inatakiwa ninapo tangaza msamaha mimi wa kiroho kwa haraka sana nifanye mambo yafuatayo ili kujilinda zaidi:
i). Moyo Wangu niushibishe Neno la Mungu
ii). Masikio yangu niyasikilizishe mafundisho ya Neno la Mungu vile vile na maneno yenye kujenga.
Namna ya kujijua mimi wa kimwili kwamba nimesamehe na hapo ndipo mtihani ulipo.
- Katika hili ukweli ni huu mimi wa kimwili huwa sisamehi, ndio maana naweza kusema nimemsamehe mbele ya macho ya watu na masikio ya watu yakasikia lakini ikawa bado kinywa changu kinanena yaliyo mabaya dhidi yake, moyo Wangu unawaza yaliyo mabaya dhidi yake, vilevile na ufahamu Wangu una tafakari yaliyo mabaya dhidi yake.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni