JIHADHARI NA UPOFU WA KIROHO.
SEHEMU YA 2.
- Ukweli ni kwamba ili kanisa liweze kusimama katika misingi hai ya ucha Mungu inatakiwa kuwepo na Roho ya maono ndani
ya Kanisa, kwa nini ? Roho ya maono ndio inayo leta mafunuo na mwanga katika fahamu za watu wanao mtafuta Mungu.
- Ninahitaji Roho ya maono katika safari ya kumtafuta Mungu ndipo safari yangu itakuwa salama.
- ( Roho ya maono ndio inayo toa mwanga wa kufahamu ukweli kuhusu Mungu ).
- Ni vigumu mimi kutambua mambo ya rohoni ikiwa sina muunganiko mzuri na Roho Mtakatifu.
- Kitu ambacho inatakiwa nifanye nikiwa kama mkristo mwamini hazina ya moyo Wangu inatakiwa niielekeze katika Neno la Mungu, hapo nitamnyima shetani uwezo wa kuyaguza maisha yangu na kila kinacho nihusu.
Mathayo : 6:19-21
- Inatakiwa Imani yangu niiaminishe zaidi kwa mambo ya rohoni kuliko mambo ya mwilini, kwa sababu mambo ya rohoni ni utukufu kwa Mungu na mambo ya mwilini ni uharibifu.
- ( Hazina ya moyo wa mtu anaye mwamini Mungu ikiwa katika Neno la Mungu hawezi kukengeuka hata kama atapita kipindi kigumu namna gani.)
- Ukweli ni kwamba hazina ya moyo wa mkristo inatakiwa iwe katika Imani, iwe wakati wa tabu, iwe wakati wa raha, hapo itakuwa umemnyima uwezo shetani wa kugusa kinacho kuhusu.
- Maisha ya mkristo aliye okoka yanatakiwa yawe na Tumaini siku zote bila kutazama mazingira na wakati, bali yasimame katika Imani tu hata maandiko yanasisitiza.
Waebrania 11:6.
- Mungu atakuwa halisi katika maisha yangu kama nikidumu katika Imani, lakini kama nikitetereka katika Imani mapenzi yake yatajificha, kwa hiyo itakuwa ni vigumu mimi kupata muunganiko wa kweli.
- Uhalisia wa kumcha Mungu katika maisha yetu unakuwa mgumu kwa sababu tumeelekeza zaidi Imani zetu katika mambo ya kimwili ndio maana kupata mpenyo ni vigumu sana.
- ( Ukiona mtu anawaza kupita kawaida maana yake moyoni mwake hana hata tone la kumwamini Mungu.)
- Inatakiwa nitafute mapenzi ya Mungu uhalisia wa maisha yangu utakuwa wazi mbele ya kila mtu.
- Nikiwa muathirika wa Neno la Mungu nitauona utamu wa Mungu ulivyo, kwa sababu kila kitakacho toka ndani yangu ni moto.
- ( Kanisa la leo limepoteza uwezo wa mafunuo ya Mungu ndio maana kondoo wa Mungu wamekuwa kama kondoo wasio kuwa na mchungaji ).
Zakaria 12:1- 14
- Wokovu nilio nao inatakiwa usimame katika msingi wa mambo yafuatayo:
a). Imani
b). Kujifunza Neno la Mungu
c). Kudumu katika muongozo wa Neno la Mungu, hapo kutazaliwa Roho ya Upendo itakayo yaunganisha maisha yangu na nafsi ya Mungu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni