Jumapili, 1 Novemba 2015

IMANI NA MAISHA

Somo la leo: 

IMANI NA MAISHA

- Katika somo la leo tutapata tafsiri ya Imani, pia tutapata tafsiri ya Neno maisha.

Tafsiri ya Neno Imani kulingana na somo la leo :

- Imani ni kitu cha rohoni, yaani utenda kazi wake upo kwenye ulimwengu wa roho, kwa hiyo ninapo sema Imani nazungumzia kitu ambacho hakionekani kwenye macho ya damu na nyama.

Kwa tafsiri nyingine:-

- Imani ni sheria ya kiroho yaani ina uwezo wa kufanya mapinduzi katika maisha ya mtu kwenye ulimwengu wa roho.

Tafsiri ya Neno maisha kulingana na somo la leo :

- Maisha ni kitu cha kimwili au cha mwilini ambacho kipo katika mzunguko wa mwanadamu chini ya jua.

- Tatizo la watu wengi wanao mwamini Mungu kinacho wadhoofisha katika hali ya kiroho, wamewekeza nguvu nyingi katika kupambana na maisha ya kimwili kuliko kujiongeza katika kuongezeka kiimani, na hii ni kwa sababu wakristo wengi Imani zao ziko kimwili si kiroho,
na Imani iliyoko kimwili mfano wake:-
1. Nimeombewa mpaka nione nimepona ndipo niamini
2. Nimetabiriwa mpaka litokee ndipo nimwamini Mungu, haya ni mambo kadhaa yahusianayo na Imani ya mtu iliyo jengwa katika hali ya kimwili.

- Ukweli ni kwamba maisha ya kimwili yamejawa na hisia na hisia ina tabia hii :-
 a). Hisia huja hisia huondoka, sasa basi pale ambapo hisia inaondoka maumivu huwa vile vile.

ANGALIZO NO 1

 # Anae tamka akiwa rohoni na anaye pokea akiwa mwilini hapo hakuna muunganiko, yaani hakuna matokeo ya lile tamko, mpaka pale ambapo anae pokea awe naye katika roho.

- Tatizo la wakristo wengi wanafuata mikate makanisani hawamtaki Mungu, watu kama hawa uponyaji wao ni mgumu sana halafu watu hawa ni wepesi sana kuwa lalamikia watumishi wa Mungu na kuwalaani wakati wao ndio tatizo.

- Kitu ambacho inatakiwa nifahamu ninapo kwenda kwenye uso wa Mungu kuhitaji msaada tayari Mungu anakuwa amesha lifahamu wazo langu, kwa hiyo maelekezo ninayo pewa na Mtumishi wa Mungu ni kulingana na uhitaji wangu inatakiwa niyatendee kazi kwa sababu siwezi kuelekezwa nje na tatizo nililo nalo bali nitaelekezwa sambamba na tatizo nililo nalo na namna ya kuliepuka.

- Wazo la kila mwanadamu li wazi kwenye uso wa Mungu hata maandiko yanasema 
Isaya 55:8-11.

- ( Ufahamu huleta hekima na busara, na hili ndilo jambo kuu linalo takiwa liwe katika maisha ya mtu anaye mcha Mungu ).

- ( Jambo hili ni la kuwa nalo makini nikiendekeza sana maisha ya kimwili mfumo mzima wa ufahamu wa rohoni una hatari ya kuvurugika ). 

- ( Kudumu katika Roho kwa hitajika sana kwa sababu huilinda Imani isijeruhike na wote tunafahamu chanzo cha Imani kujeruhika ni maisha ya kimwili ). 

- Haya mambo ni muhimu kuyafahamu 
 i). Maisha ya kimwili yako chini ya utumwa wa dhambi 
 ii) Maisha ya kiimani yako chini ya mwongozo wa Roho Mtakatifu katika Roho, na hapa ndipo inapo takiwa tujikite zaidi kwa mtu anaye mtafuta Mungu hata Bibilia imesema. 
Warumi 8:14,16,26

- Mtu mwenye Roho wa Mungu ndani mwake hawezi kukosa hekima na busara.

- Mtu mwenye Imani kwa Mungu hakosi ufahamu wa Neno la Mungu.

- Ninapo hitaji kitu chochote kutoka kwenye uso wa Mungu jambo la kwanza ambalo inatakiwa nilitazame ni kutafuta muunganiko kati ya mimi na Mungu.

- Unapo mpa Mungu nafasi ya kuzungumzia chanzo cha tatizo lako hiyo ni nafasi tosha ya kutatuliwa tatizo hilo. 

- ( Ni vigumu kumfundisha mtu kumjua Mungu akiwa bado hajatubu dhambi zake ). 



Hakuna maoni: