Somo la leo: NAMNA AMBAVYO IMANI INASAFIRI NA KUTOA MATOKEO.
By Mtumishi Bab G Power.
Je Imani inasafiri katika mazingira gani?
- Imani inasafiri kwa njia ya mamlaka
inayotoka ndani ya Neno la Mungu, kwa hiyo katika njia hii lazima Imani itoe matokeo.
inayotoka ndani ya Neno la Mungu, kwa hiyo katika njia hii lazima Imani itoe matokeo.
Je nini kinasababisha matokeo ya Imani kudhibitika ?
- Kinacho sababisha matokeo ya Imani kudhibitika ni ile mamlaka ya Neno la Mungu iliyoko ndani ya mtu, ndio maana ukiwa kama mwamini hakikisha Biblia unaisoma katika mazingira ya Imani.
- ( Nikiathirika kiufahamu nimeathirika kimaisha, ndio maana inatakiwa nilipe Neno la Mungu kipa umbele kwenye maisha yangu, kwa sababu linao ufahamu wa KiMungu ndani yake na wenye uwezo wa kuyaponya maisha yangu).
- Imani za waamini walio wengi zimeshindwa kuwapa matokeo mazuri katika maisha ingawa wanatabiriwa, kwa sababu waamini hao wamekosa uaminifu katika maisha yao ya ucha Mungu.
- Ukweli ni kwamba baraka yangu ninaichelewesha mimi mwenyewe kwa kushindwa kuyalingana mapenzi ya Mungu.
- (Imani nikiiboresha ikakua macho ya kiroho yatafunguka)
- Maisha ya wokovu bila maono ni hatari sana
- Imani inahitaji maisha ya uaminifu ndipo mamlaka itadumu katika kutenda kazi. Ufunuo 2:10
- Hali ya hofu ambayo wakristo wanairuhusu ndani ya mioyo yao pale wanapo kutana na changamoto fulani fulani katika ya maisha, ndo kichocheo kikubwa cha kushindwa kustahimili katika maisha yao.
- Kuanzia leo inatakiwa niitunze Imani yangu katika uaminifu itanipa matokeo mazuri.
- Ili tuwe Kanisa lenye Imani na nguvu ya Mungu tunahitajika kuongozwa na ufahamu wa Neno la Mungu katika maisha yetu.
ANGALIZO NO.1
Usinyooshe kidole kwa mtu anaye pita katika jaribu lake haujui wewe utapita katika jaribu gani, unacho takiwa kufanya ni kuomba Neema za Mungu zimfunike.
- Imani inatenda kazi kwenye ulimwengu wa Roho kupita kawaida, ndio maana inatakiwa pia ingependeza sana moyo Wangu kubaki katika hali ya utulivu wa Neno la Mungu ili mamlaka inayo sababisha matokeo isinajisike.
KINACHO ZUIA IMANI ISHINDWE KUFANYA KAZI.
- inaendelea kipindi kingine......
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni