Jumapili, 11 Oktoba 2015

VIZUIZI VINAVYO FUNGA MAFANIKIO YA WAKRISTO SEHEMU Y

Somo la leo:
VIZUIZI VINAVYO FUNGA MAFANIKIO YA MKRISTO

SEHEMU YA 2

 1. Kushindwa kusamehe
 2. Kutokuondoa nadhiri kwenye uso wa Mungu

UFAFANUZI KUHUSU KUTOKUONDOA NADHIRI KWENYE USO WA MUNGU

- Nadhiri ni ahadi anayo itoa mtu kwenye uso wa Mungu au kwa mtu mwingine yeyote kwa mapenzi yake yeye binafsi bila kushawishiwa na mtu yeyote yule, yaani ni tendo linalo tendeka na wakati huo huo mtu akiwa na akili timamu.

- Nadhiri huwekwa kwa njia ya neno yaani katika kusema lakini huondolewa kwa njia ya tendo yaani katika kutimiza, na siku zote bila kutimiza nadhiri hiyo hubakia deni hata milele.

- Nadhiri inapokawia bila kuondolewa au kutimizwa hugeuka na kuwa laana na kuyaharibu kabisa maisha ya mtu.

Nadhiri ikisha kuwa laana inao uwezo kusababisha mambo yafuatayo katika maisha ya mtu:-

  i). Magonjwa.

- Mhubiri 5:1-2,4-6.
- Nadhiri inazungumza lakini lazima uwe na masikio ya kiroho ndipo uisikie.

- ( Mungu anapo nionya hanidhalilishi hiyo ni njia ya kuonyesha Upendo wake kwangu ).

- ( Vitabia nilivyo navyo visivyo mpendeza Mungu inatakiwa niviache kuanzia leo ili niendane na kanuni za Mungu zinavyotaka nitaona mafanikio ). 

- ( Maisha ninayo ishi ndiyo yanayo ninyima ujasiri wa kuhojiana na Mungu ili niweze kudai haki zangu ). 

- Suala la mabadiliko ni jambo linalo tekelezeka tena Kwa urahisi kwa mtu ambaye ameamua

- Nikitaka kuiepuka laana isababishwayo na nadhiri, inatakiwa niruhusu vitu vitatu viniongoze :
   1). Hekima
   2). Busara
   3). Ufahamu

- Kujikwaa kwa wakristo walio wengi kunatokana na kukosa ufahamu sawa sawa wa maneno ya  Mungu, yaani Neno la Mungu ( Biblia ). 

ii). Umasikini 

- Umasikini katika maisha ya mtu kuna sababu 

Msemo :- Kosa si kuzaliwa masikini bali kosa ni kufa masikini 

- Umasikini unasababishwa na mtu kukosea kanuni za utoaji.

- Katika ulimwengu huu kuna mambo 5 anayo takiwa kuwa nayo mwamini mkristo ili kuheshimika kwa Mungu wake, kwa lugha nyingine Afya :
  a). Afya ya kiroho 
  b). Afya ya ufahamu
  c). Afya ya kiuchumi
  d). Afya ya kimwili
  e). Afya ya ndoa 

- Umasikini ni roho inayo leta udhalilishaji katika jamii ya watu wengi, 

- Ili niweze kujikwamua katika hali ya umasiki inatakiwa nifanye kitu kwenye uso wa Mungu kitakacho niunganisha na baraka zake ili katika zile Afya 5 ziwe ni sehemu ya maisha yangu ya kila siku.

NAMNA AMBAVYO INATAKIWA NIAMBATANE NA AFYA 5.

- Agano lolote nililo lifanya kwenye uso wa Mungu bila mwongozo wa Roho Mtakatifu halina baraka.

- Sehemu ambayo inatakiwa niweke agano na Mungu inatakiwa iwe ni madhabahuni, ndio maana kabla ya Ibrahimu kumtoa Isaka alitengeneza madhabahu mahali pa kuiweka sadaka ile.

- Sadaka ni sehemu ya Mungu kumjaribu mtu wake vile vile sadaka ni sehemu ya mwamini kumjaribu Mungu wake.
Mwanzo 22: 1-

- Uchumi wa mkristo unategemea utoaji wala sio maombezi.

- Nikitaka niepuke matatizo yanayo husiana na mambo ya kifedha inatakiwa nianze kanuni za utoaji.

- Katika suala la kumtolea Mungu sadaka ni jambo lisilo hitaji majadiliano na kiumbe chochote kisicho kuwa na mbingu.

- ( Mungu hujaribiwa katika ule utoaji unao umiza mtu na kumletea mawazo ). 

- Afya ya uchumi inashikiliwa na agano ninalo liweka kwenye uso wa Mungu.

- Wakati wa mimi kujitambua ndio wakati wa kuanza  maisha katika sura nyingine.

- hakuna aliye weka Agano na Mungu la sadaka akadhalilika .

- Mungu ana heshimu sadaka kuliko kitu chochote.

- Agano ninalotaka kufanya inatakiwa nisikilize tu mwongozo wa Roho Mtakatifu. 

- Agano analo weka mtu na Mungu lazima liwe katika mazingira ya sadaka, na sadaka yenyewe nihakikishe inaniumiza pale ninapo itoa.

- Wakristo wengi wanakosa baraka kwa sababu hawana ufahamu wa kupambanua nyakati za kubarikiwa kwao, kwa sababu baraka zingine zinaweza zikawa kwa njia ya jaribu na Mfano hai ni katika Kitabu cha  2 Wafalme 4: 9-17 

- Matamko ya kinabii yana Neema ya kufanya wepesi.





Hakuna maoni: