19/10/2014
UJUMBE WA LEO:VITA
VYA KIIMANI.
Vita vya kiimani vinapiganwa kwenye ulimwengu wa roho kwasababu imani ni kitu cha Rohoni.
Vita vya kiimani havipiganwi katika ulimwengu wa damu na
nyama kwasababu imani haishikiki kwa mkono.
Wakristo walio wengi wanashindwa kwasababu vita vya kiimani
wanavigeuza kimwili,kamwe mtu wa aina hii hawezi kushinda
.
Vita vya kiimani anaweza kuvishinda mwamini mwenye mambo
matatu;
a)Msimamo.
b)Ujasiri.
c)Uvumuliviu, mtu mwenye asili hizi tatu ndani mwake ni mtu wa imani.
Vita vya kiimani vinamtaka mwamini jasiri.
Waamini walio wengi wanashindwa kufikia maono yaokwasababu wanapoingia kwenye
uwanja wa mapambano wanakuwa hawajavaa
silaha kamilifu,Je! Silaha kamilifu katika uwanja wa mapambano ni zipi?.
i)Neno (Biblia)
ii) Imani (Yesu Kristo)
iii)Uvumilivu (Ushindi).,Hizi ndizo silaha muhimu
anazotakiwa kuwa nazo mkristo mwamini atakapoingia kwenye uwanja wa mapambano
yaani (majaribu).
Mimi ninayemtegemea
Yesu Kristo inatakiwa maisha yangu yawe haki ndipo nitaendana
sambamba na baraka za Mungu vilevile katika uwanja wa mapambano nitapata
mpenyo.
Kipindi cha kujaribiwa ndio nafasi sahihi ya mwamini
kuinuliwa.
Mungu anafurahia sana tunapopita katika kipindi cha
kujaribiwa tukiwa tunalitumainia jina
lake kwasababu hata maandiko yanasema wazi uweza wa Mungu hutimilika katika udhaifu katika maisha ya mtu.
2 Wakorinto 12:1-10.
Hii ni hatari sana na
ndio inayosababisha watu wengi kuishia njiani yaani wasifikie maono yao wanapokuwa katika kipindi cha kujaribiwa hutoa maneno mengi sana ,na maneno hayo huwa hayana
Baraka katika maisha yao zaidi kuwaharibu
kabisa,na mojawapo ya maneno ni kama haya:-
i)Nimemkosea nini Mungu mbona mimi tu?
ii)Yesu amenisahau
iii)Mbona sijatenda dhambi?
iv)Mbona mimi sadaka natoa na michango mbalimbali
n.k.;Maneno kama haya katikati ya uwanja wa mapambano ndio yatakayo
kufanya ushindwe.
HATARI NAMBA MBILI
Wakati wa kujaribiwa wakristo wengi hutoa nadhiri nyingi sana ambazo baadae
hushindwa kuzitimiza ndio maana watu
hufa vifo vya ghafla na matatizo mengi
huwashukia ,pia mojawapo ya nadhiri wanazozitoa
ni kama hizi :-
i)Yesu ukinipa mtoto nitatoa sadaka ya gari .
ii)Mungu ukinibariki sitakuibia fungu la kumi .
iii)Yesu ukiniponya ugonjwa wangu hili ndilo kanisa langu nitakalosali siku zote.
iv)Mungu ukinifungulia milango nitamjali mtumishi wako,maneno
kama haya yasipotimizwa kwa wakati wake huleta madhara sana katika maisha ya
watu.
Vita vya kiimani atavishinda
mkristo mwenye ufahamu sawasawa na Neno la Mungu.
NINI
KIFANYIKEKATIKA UWANJA WA MAPAMBANO
Kitu ambacho ninatakiwa kukifanya ninapokuwa katika uwanja wa mapambano ni kuhakikisha imani yangu iko hai yaani niwe na imani yenye tendo,hili jambo hata kitabu cha Yakobo kimesema
Yakobo 2:14- 26
Imani ya mkristo inahesabiwa kuwa hai pale matendo yanapodhihirika.
Ujumbe utaendelea wiki ijayo…………..
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni