Jumapili, 12 Oktoba 2014

UJUMBE WA LEO: NAMNA YA KUKABILIANA NA ROHO ZA UDHOOFISHAJI



12-10-2014
UJUMBE WA LEO: NAMNA YA KUKABILIANA NA ROHO ZA UDHOOFISHAJI
Roho ya udhoofishaji inamvaa mkristo ambaye hajaimarika kiimani  nahii imekuwa ni ugonjwa kwa asilimia kubwa  katika wakristo wa leo,  kwa maana zaidi nguvu wanayo anzanayo katika kumtafuta Mungu sio wanayo maliza nayo , ndio maana Mgalatia akauliza swali
Wagalatia 3 yote
ANGALIZO 1: Ni hatari sana kwa maisha ya kesho kukiwepo jambo nyuma yangu   ili nimtafute Mungu.
Nivigumu kutambua nina roho ya udhoofishaji nikiwa nimefunga milango ya Neno la Mungu moyoni mwangu.
Mkristo ambaye amefunga milango ya Neno la Mungu ndani ya moyo wake anatabia zifuatazo
A)     Kutokuona umuhimu wa kumuabudu Mungu katika vipindi vya kanisani yaani utoro
B)      Kujali majukumu yake ya kibinadamu kulikokukaa chini kusikiliza Neno la Mungu
C)      Kuheshimu mwongozo wa mwanadamu mwenzake kuliko kuheshimu mwongozo wa Mungu kupitia  Roho Mtakatifu.Mtu wa aina hii hawezi kukwamka katika hali ya kudhoofika ,mpaka pale atakapo funguliwa (Delivarance).

Katika suala la kudhoofika kiimani linatokana na wakristo wenyewe kutokufungua milango ya mioyo yao kulisikiliza Neno la Mungu ndipo  inapoanzia  na mambo mengine kuharibika .

Ukidhoofika kimwili  na mambo haya yatadhoofika  kwasababu imani ndio msingi:-
i)                    Utadhoofika kiuchumi
ii)                   Utadhoofika Kiafya
iii)                 Utadhoofika Kiufahamu
iv)                 Utadhoofika Kifamilia n.k.

Mimi kama mkristo mwamini  katika maisha yangu  ya kiimani lazima nijichunge sana na jamii ninayokutana nayo  katika maisha yangu ya kila siku,kwasababu nisipokuwa makini athari za kuathirika kiroho  ni kubwa mno, vilevile inabidi nitambue jamii  ninayokutana nayo  kuna jamii ya waaminio na jamii ya wasioamini.
Amosi 3:3
ANGALIZO 2:Nikiona ninamwabudu Mungu  alafu hapohapo nia ya moyo wangu inaenda kinyume na kazi za Roho Mtakatifu maana yake ninalipinga Neno la Mungu waziwazi ,mtu kama huyo hawezi kuambatana na Baraka za Mungu kamwe.

Mkristo akiruhusu nia ya moyo wake kuambatana na  Neno la Mungu  ameyaponya maisha yake ya kiroho kwasababu Neno la Mungu litamuongoza  kuyatenda mapenzi ya Mungu tu.
Kumwabudu Mungu ni kufungua milango ya moyo kulisikilza Neno la Mungu hapo ndio mwanzo  wa hekima ya Mungu kujiumba katika maisha Ya mtu.

Nia ya moyo wa mkristo mwamini ikienda kinyume tu na mwongozo wa Neno la Mungu ndio mwanzo wa imani aliyonayo kudhoofika.

JE? NINAEPUKAJE HALI YA KUDHOOFIKA KIIMANI
Ili  niweze kuepuka hali ya kudhoofika kiimani inatakiwa nifungue milango ya moyo wangu kusikiliza Neno la Mungu peke yake yaani nisiruhusu yasiyofaa yapingananyo na Neno La Mungu kuingioa kwenye moyo wangu
Warumi 10:17

Wakristo wengi wamedhoofika kiimani kwasababu haqwataki kuambiwa ukweli na hiyo ndio silaha  ambayo shetani anaitumia kubomoa imani za watu wengi.

Hali ya kukubali kuambiwa ukweli inamsaidia sana mwamini kumuimarisha katika misingi zaidi ya kumjua Mungu.

Hakuna maoni: