Jumatatu, 28 Julai 2014

ujumbe: Jumapili 27-07-014: UPENDO



UPENDO
  • Upendo ni roho ya Mungu kwamaana zaidi upendo ni Roho Mtakatifu.

  • Upendo wenye  uhai wa kimungu  huwa unadhibitika katika tendo.

  • Upendo wa kwanza unatakiwa uwe ndani ya mtu binafsi ambao ndio makao ya Roho Mtakatifu,hapo ninaweza kusema mimi ninapenda katika tendo,kwasababu maandiko  yanasema nimpende Bwana Mungu wangu kwa moyo wangu wote ,kwa nguvu zangu zote,kwa akili zangu zote ,na kwa roho yangu yote.
Mathayo 22:34-40.

  • Mkristo ambaye moyo wake umeambatana na upendo wa Mungu ana asili moja na Roho Mtakatifu.

  • Mkristo ambaye moyo wake umejaa hila na visasi moyo wake haujakamilika katika upendo wa Mungu, mkristo wa aina hii huwa hamwabudu Mungu katika roho na kweli,vilevile hawezi kuona uthamani wa kumuheshimu Mungu.

  • Udhihirisho wa kwanza wa upendo wa mkristo ni hali ya kujiheshimu, kwasababu mkristo ni hekalu la Roho Mtakatifu na Mungu ametoa tahadhari kuhusiana na mtu anayelichafua hekalu lake kupitia  kitabu cha
1Wakorintho  3:16-17.

  • Upendo huleta hali ya nidhamu katika maisha ya mkristo.

  • Waamini wa leo hawana upendo,kwasababu hawaliheshimu kabisa hekalu la Mungu ambalo ni wao wenyewe,kwahiyo kama mtu akishindwa kujipenda yeye mwenyewe  ni vigumu sana kumpenda jirani yake katika kweli.

  • Kama mimi sijiheshimu siwezi kuidhibiti nafsi yangu basi upendo unaotoka ndani mwangu hautakuwa wa kweli.

  • Ili upendo  nilionao uonekane ni haki kwenye uso wa Mungu kwanza kabisa inatakiwa nijiheshimu mimi mwenyewe, sambamba  na Neno la Mungu linavyosema katika Mathayo 22:37, hii ni kwasababu Roho wa Mungu anaishi ndani mwangu na amri ya kwanza  inathibitisha  wazi mtu wa kwanza kumpenda ni Mungu, kwahiyo nikilichafua hekalu la Mungu upendo nitakao uonesha kwa watu wengine utakuwa ni wa unafiki kwasababu amri ya kwanza nimeshindwa kuitendea kazi.

  • Upendo ni asili hai ya Mungu ambayo hupandwa ndani ya moyo wa mkristo pale ambapo mkristo anaamua kuokoka .

  • Biblia imethibitisha upendo ni tunda la Roho,na siku zote inafahamika tunda ni kitu cha aina gani.

  • Tunda ni kitu ambacho ni kitamu vilevile hupendwa na kila mmoja.

UFAFANUZI WA NENO TUNDA KATIKA HALI YA KIBINADAMU.
  • Tunda ni  aina fulani ya  mmea ambao ukikomaa ukafikia wakati wa kuiva huliwa na kila mmoja mwenye mwili, vilevile hutamaniwa na kila mmoja anayeishi kwenye mwili wa damu na nyama.Mfano wa matunda :-Tofaa,Nanasi, Embe n.k.

NENO TUNDA KATIKA UFAFANUZI WA KIROHO
  • Tunda katika ufafanuzi wa kiroho ni Neno la Mungu, hili hutamaniwa zaidi na wakristo walioamua kuokoka yaani kumkiri Yesu kristo kuwa Bwana na mwokozi  wa  maisha yao
  • Mahali Neno  la Mungu lilipo upendo hai upo        
                                                  Wagalatia5:22-23.

  • Mkristo aliyeimarika katika upendo huwa na mambo matano kama si saba ndani yake:-
       i.            Furaha      ii.            Amani    iii.            Uvumilivu   iv.            Wema     v.            Fadhili 
  vi.            Uaminifu n.k
.
  • Kwanza kabisa kabla sijaingia kwenye mombi inatakiwa nifahamu huyu ninaye muomba anaishi wapi, ndipo niweze kuhojiana naye.

  • Ili aweze kunisikia inatakiwa nisafishe moyo wangu kwasababu yeye huishi kwenye moyo safi.

  • Je! Moyo safi ukoje?
a.     Una upendo
 b.     Una amani 
c.      Unasamehe
d.     Una utu wema
 
NAMNA YA KUUPATA UPENDO HAI WA KIMUNGU:
  • Ili niweze kuupata upendo hai wa kimungu inatakiwa niruhusu roho yangu kuendelezwa kupitia maandiko Matakatifu na roho yangu itaendelezwa katika misingi ifuatayo:-
a)Kulisikiliza Neno la Mungu mara kwa mara, hapa inabidi niwe na jukumu la kwenda kanisani wakati wote wa ibada.
b)Kujisomea Biblia wakati wa mapumziko au wakati wa  kuburudisha akili, hapo nitapata utulivu ndani ya moyo wangu vilevile roho ya kupambanua.
c)Kuomba mara kwa mara yaweza kuwa hata zaidi mara tatu kwa siku,hapa nitapata Neema ya kuwa rafiki wa Mungu yaani nitakuwa na ukaribu wa ndani zaidi.

  • Hali ya uvumilivu alionao mkristo ndiyo huthibitisha upendo wa dhati alionao kwa Mungu.

  •  Kabla ya kulalamika kwamba  Mungu hajajibu maombi yangu ingawa nimeomba siku nyingi  inatakiwa niangalie historia yangu ya maisha ya wokovu je yanampendeza Mungu? Na inafahamika wazi Mungu ni wa haki.

  • ( Nikitaka Mungu ajibu maombi  inatakiwa  nidumu katika mapenzi yake).

  • Upendo hai kamwe hauhesabu makosa , bali huwa na tabia ya kuvumilia, na uvumilivu ndio huwa unaonyesha wazi uthamani alionao mtu kwa Mungu wake.

  • Yesu kristo alithibitisha wazi upendo alionao katika maisha yangu. Je, aliudhihirisha kwa njia gani?
a.     Kuteswa 
b.     Kusulubiwa

  • Huo ni udhihirisho tosha kwangu mimi kama mwamini kuyaishi maisha aliyo yaishi Mungu akiwa katika mwili, vilevile haijalishi ni mazingira gani nitakutana nayo , cha msingi ni uvumilivu tu.ndio maana Biblia inanitia moyo katika kitabu cha
Waebrania 2:17,18

  • Inatakiwa nifurahie sana ninapo kutana na vikwazo mbalimbali katika maisha yangu ya wokovu , maana vikwazo hivyo vinaniimarisha zaidi katika misingi ya kimungu ili dhoruba itakayo tokea kesho isiweze kuniathiri kiimani.

  • Nivigumu kufanikiwa kupita uwezo wa Imani yangu ilivyo. Mfano: nikiamini kwa 20%, asilimia za Baraka zitakuja kwangu kwa 20%,nikiamini kwa 50%, Baraka zitakuja kwangu kwa 50%. Kamwe haziwezi kuvuka kiwango changu cha Imani yangu.  



Hakuna maoni: