BIBLE STUDY: 26/6/2014.
USIOGOPE
-Haitakiwi niogope hata kama ninakabiliana na mazingira magumu kiasi
gani,bali inatakiwa nikikutana na ugumu katika maisha yangu ya wokovu
imani yangu niielekeze katika maandiko Matakatifu.
-(Kitendo
cha mimi kama mwamini kuruhusu uoga kuuvaa moyo wangu tayari ninakuwa
nimeijeruhi imani ,huo ndio unakuwa mwanzo wa imani niliyonayo kupoteza mwelekeo).
-Nikiruhusu mpenyo wa moyo wangu kushambuliwa kina cha maarifa ya
rohoni kinajifunga.Kwasababu ndani ya moyo wa mwamini kuna faragha
ambayo Roho Mtakatifu huitumia kuzungumza na mkristo mwamini,ndio maana
Biblia imetoa tahadhari.
Mithali 4:23.
-Mambo ambayo shetani huyatumia kuuchafua moyo wa mwamini upoteze utulivu :-
a). Hofu
b). Kutokusamehe.
c).Mawazo mabaya.
UFAFANUZI WA KIPENGELE ‘A’ KINACHO ZUNGUMZIA HOFU
-Hofu ni adui mkuu wa imani niliyonayo vilevile humpotezea mwamini hali ya ujasiri katika moyo wake.
-Hofu ina kawaida ya kubadilisha mwelekeo wa imani ya mkristo,ili ipoteze uwezo wa kupambanua katika roho.
-Hakuna jambo linalotutokea na kutusumbua katika maisha ya mwilini
,Mfano:Magonjwa, Umasikini,Mauti, ikiwa Mungu hajatupa taarifa katika
roho,ila shida inatokana na kutokuwa na uwezo wa kupambanua kati ya
sauti ya Mungu na roho chafu ,
Amosi 3:7.
-Hofu ya maovu ninayo yatenda ndiyo inayo ninyima ujasiri wa kusimama
kwenye uso wa Mungu kudai haki zangu kama mwana wa Ufalme.
-Moyo wenye hofu, mashaka, uoga, manung’uniko hauwezi kupata ujasiri wa
kuhojiana na Mungu katika roho vilevile katika mwili,kwa sababu Mungu ni
Mtakatifu,ndio maana ninatakiwa nidumu katika misingi ya Neno la Mungu
ili kuulinda moyo wangu usijeruhiwe ukapoteza hali ya ujasiri wa
kujieleza kwenye uso wa Mungu.
-Amosi 3:7 ni Neno alilolisema
Mungu katika misingi ya kiapo lengo kuu ni kumthibitishia mwamini
anayedumu katika maisha ya ucha Mungu kwamba asiogope changamoto yeyote
ile bali aamini tu.
UJUMBE HUU UTAENDELEA WIKI IJAYO………
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni