Jumatatu, 30 Juni 2014

AMINI NENO LA MUNGU : jumapili 29-06-2014




             UJUMBE:  AMINI NENO LA MUNGU

Uumbaji wa kila ninachokiona chini ya mbingu chanzo chake ni Neno la Mungu.

Nikiliamini Neno la Mungu ninakuwa ninamuamini Mungu mwenyewe,na hii ndiyo inayotakiwa kwa kila mtu anayesema anamcha Mungu lazima aamini maandiko Matakatifu.

( Simuamini Mungu kwakuwa ninamuoa katika machoya damu na nyama bali ninamuamini Mungu kwasababu maandiko Matakatifu yananithibitishia kwamba Mungu ni Roho;na hii imeandikwa katika : Yohana 4:24)

Yohana 4:24 ni agizo kwa kila aaminiye kwamba katika ucha Mungu wake lazima uwe katika misingi ya rohoni (imani).

(Neno la Mungu ndilo linalotoa mpenyo wa baraka za Mungu katika maisha ya mkristo)
(Neno la Mungu ndio chanzo cha kila kitu)

Yesu kristo anaishi ndani ya mwamini anayeliamini Neno la Mungu peke yake,na huyo ndiye mkusudiwa katika ahadi za Mungu.

Neno la Mungu ndilo linalotoa au linaloruhusu mambo yafuatayo kuja kwa mwamini:-
a)Baraka
b) Uponyaji
c)Afya njema
d)Mafanikio ya mwilini kwa jinsi zake
e)Uzima wa milele , vilevile hata maandiko yamelithibitisha hili; Mithali 4:20-22

Ninapo yasoma maandiko na kuyaamini kwenye ulimwengu wa roho huwa napata ulinzi dhidi ya nguvu za giza katika maeneo yafuatayo:-
a)Kuhusu afya yangu
b)Kuhusu familia
c)Kuhusu kazi zangu(biashara)
d)Kuwa na kibali machoni pa Mungu na machoni pa wanadamu.

FAIDA YA KULIISHI NENO:
1.Faida ya kwanza nitakayoipata katika maisha ya kuliishi Neno nitapewa mamlaka.

Neno la Mungu ndilo linalozaa mamlaka ya uumbaji ,na mamlaka hii hufanya kazi katika mazingira gani
a)Kuamuru
b)Kutamka,Hii ni picha wazi katika kitabu cha Mwanzo 1:1,2,3,6,9,14,20 na 24.

Mamlaka ninayoipata katika Neno la Mungu nikiitumia vizuri nitakuwa mtu wa tofauti  katika jamii inayonizunguka.

Wakristo wengi wamepoteza mamlaka ila wokovu wanao,ndio maana wengi wamedumaa kiroho.

Kinacho ruhusu mpenyo wa mkristo kuwepo ni mamlaka inayotoka katika Neno la Mungu.

Ili maisha  yangu yawe salama kiroho na kimwili inatakiwa niikuze mamlaka ya Kimungu  ilioko ndani mwangu.

Kushindwa kuitumia mamlaka iliyoko  ndani mwangu inatokana na mahusiano yangu na Neno la Mungu kuwa mabovu.

2. Faida pili ya kuliishi Neno itanisaidia mimi kupata roho ya uumbaji.

3. Faida ya tatu ya kuliishi Neno ni kupata ufahamu wa rohoni na hii ndiyo inayotakiwa kwa mcha Mungu.

Hali ya ufahamu ikiisha jiumba ndani ya muamini  hupata uwezo wa kupambanua, vilevie halihiyo ya ufahamu itamsaidia muamini kudumu katika Roho.

Hali ya ufahamu huwa inaathirika ndani ya mkristo akiruhusu tabia za asili kumuongoza.

Ili mkristo apate ufahamu wa kuishi maisha Matakatifu inatakiwa yeye na Neno la Mungu kuwa wamoja, vilevile hata Yesu Kristo kuna jambo alilolisisitiza kudhihirisha upendo wa kweli alionao mtu kwa muumba wake  Yohana14:23,24.

Udhihirisho wa upendo wangu kwa Mungu ni namna ambavyo ninavyo iamini Biblia na kusoma Neno la Mungu lililondikwa ndani ya Biblia.



Hakuna maoni: