- Imani inatamkwa lakini haishikiki kwa mkono, hiyo ni picha wazi kwamba imani ni kitu cha rohoni, siku zote kitu kilicho katika roho hakina umbo maalumu yaani hakionekani katika macho ya damu na nyama.
(Adui yangu ni yule niliye mzidi kiimani).
- Mahusiano ya ndani na Neno la Mungu ni aina fulani ya mazoezi ya kiroho.
- - Maana ya mazoezi ya kiroho:
- a) Kusoma Biblia usiku na mchana, pia agizo hili alipewa Yoshua
- Yoshua 1:8, lengo ni nini?, ni kubaki katika mfumo ule ule wa
ANGALIZO: Imani yangu haiwezi kuonekana kwamba inauwezo wa kukabiliana na changamoto kama sijakutana na misukosuko ya kunitikisa.
b) Ufungaji wa mara kwa mara.
c) Uombaji.
d) Kulisikiliza Neno la Mungu.
Haya ndio mazoezi ya kiroho halisi yatakayo ipa imani yangu uwezo wa kunifanya ni dumu katika wokovu bila kutikiswa na changamoto ya aina yoyote ile.
- Nini maana ya imani?
a) Imani kuamini pasipo kuona.
b) Imani ni kusadiki, kutarajia pasipo kutilia shaka kile unacho ngojea.
c) Imani ni kumuona mtu anashida na kumsaidia.
d) Imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo ni bayana ya mambo yasiyo onekana Waebrania 11:1.
(Nikifahamu Neno la Mungu katika uhalisia, roho ya uumbaji wa kimungu inaumbika ndani mwangu).
(Nikiendelezwa roho yangu ikamfahamu Mungu nitapata nguvu yakutawala mafanikio ya kimwili).
( Bila kuiendeleza roho yangu ikamfahamu Mungu ni vigumu kupata mpenyo).
* Waebrania 11:1 ni andiko ambalo lina ni dhihirishia mimi kama mwamini ni dumu katika imani, ndipo nitapata mpenyo halisi vile vile nitapata urahisi wa kuhojiana na Mungu katika roho.
- - Maisha ya mkristo ili yaweze kwenda sambamba na baraka za Mungu inatakiwa aruhusu imani yake isitazame vinavyo onekana, hii ni picha wazi hata kimaandiko 2 Wakorintho 4:18.
- (Vinavyo onekana haviwezi kumpa mkristo mpenyo wa kumheshimu Mungu kwa sababu ni vitu vya mwilini).
KINACHOFANYA IMANI YANGU IWE KATIKA MZUNGUKO.
Kinachofanya imani yangu iwe katika mzunguko wa kuniunganisha na baraka za Mungu ni namna ambavyo kinywa changu kitakavyo kuwa kina likiri Neno la Mungu, kwa sababu maisha ya mtu hubadilika kulingana na jinsi yeye mwenyewe anavyo jikiria, ni sawa na kusema anajitabiria.
''By Pastor Bab G Power''
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni