
ujumbe: WOKOVU SEHEMU YA PILI
Ø
Wokovu ni nini?
Ø
Wokovu
ni Neema ya Mungu iliyoko juu ya mtu ambaye amemwamini Yesu Kristo kuwa Bwana
na Mwokozi wa maisha yake, ndio maana Bibllia ikasema Waefeso 2:8.
Ø
Wokovu ni
Neema vilevile Neema ni upendeleo
usio stahili juu ya mtu yaani ‘’hakustahili kuitwa mtumishi wa Mungu lakini
kwasababu ya Neema ya Mungu anaitwa Mtumishi wa Mungu’’.
Ø
(Inatakiwa
niutunze wokovu nilio nao kwasababu
ni zaidi ya dhahabu, kwasababu wokovu ni Neema inayonipa mimi mwamini kuuishi umilele wa Mungu).
Ø
(Wokovu ni zawadi iliyotoka kwa Mungu
juu ya maisha yangu).
A.
KANUNI
ZA KUTEMBEA KATIKA WOKOVU
Ø
Ili niweze kutembea katika kanuni halisi za
wokovu, inatakiwa nisome Biblia nione uhalisi wa maisha ya Yesu kristo alivyo
ishi akiwa katika mwili wa damu na nyama.Kwa maana zaidi Yesu Kristo awe mfano
wangu mimi ninaye muamini , hata maandiko matakatifu yamesisitiza juu ya jambo
hili 1petro2:21-25.
Ø
Katika kutembea ndani ya uhalisia wa Yesu Kristo
Biblia inafunua wazi kwamba , inatakiwa mimi ninaye muamini Mungu, nifuate kwa
wazi nyayo za Yesu Kristo kama ilivyo andikwa katika 1Petro2:21-24.
Ø
Je! Nyayo za Yesu Kristo ambazo Biblia inazisema
ni zipi?
A.
Yesu Kristo hakutenda dhambi , huo ndio mwenendo
wa kwanza wa Yesu Kristo.
B.
Wala uongo haukuonekana kinywani mwake.
C.
Hakuwa mtu wa kulipiza kisasi.
D.
Alikuwa mtu mwenye Upendo wa kweli. ambaye
tayari amekwisha kuwa Roho.
UFAFANUZI WA KIPENGELE (A )KINACHO ZUNGUMZIA DHAMBI
UFAFANUZI WA KIPENGELE (A )KINACHO ZUNGUMZIA DHAMBI
Dhambi ni nini?
Ø
Dhambi ni uasi , vilevile kila jambo lililo
kinyume na mpango wa Mungu ni dhambi , jambo hili hata biblia ime lifafanua,1
Yohana5:17a vilevile 1Yohana3:4,
hapo tunapata ufafanuzi kuhusu dhambi yaani matendo ya giza.
Ø
(Dhambi haina heshima)
Ø
Kazi ya dhambi ni kudhalilisha utu wa mtu,
vilevile huondoa uthamani alionao mtu katika jamii
Ø
Nini kinacho fanya wokovu wa mtu udhalilike?
·
Ni kwasababu ya kukosa maarifa ya ufahamu wa
Neno la Mungu, yaani Maandiko matakatifu(Biblia).
Ø
Wokovu
wa mkristo mwamini utaimarika iwapo mkristo huyo ataruhusu Neno la Mungu
kuielimisha roho yake, kitakacho tokea kwa mkristo aliye elimishwa roho yake
na Neno la Mungu ni kina cha maarifa ya rohoni
kuongezeka, yaani kuwa na kina zaidi cha kumjua
Mungu hapo ndipo wokovu wa mkristo utakuwa salama.
Ø
Nikitaka kuishinda dhambi inatakiwa mimi na Neno
la Mungu tuwe wa moja, hapo nitakuwa na asili moja na Mungu kwaasababu Mungu ni
Neno
Yohana1:1,2
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni