- Suala la mimi kujiimarisha kiimani inatokana na juhudi yangu binafsi; kivipi? Jinsi ninavyokuwa ninajitoa kusoma Biblia , vilevile kusikiliza Neno la Mungu.
- (Nirahisi kubadilika kiimani vilevile kimaisha kama nitaruhusu maarifa ya Neno la Mungu kuniongoza).
- Mtu ambaye anaruhusu maarifa ya Neno la Mungu kumuongoza hupata faida zifuatazo:-
a. Hupewa na Roho wa Mungu uwezo wa kupambanua sauti ya Mungu wakati wote Mungu anapo sema na mtu huyo.
b. Hupata muunganiko wa kweli na Baraka za Mungu, yaani hufanikiwa kwa kila atakacho kigusa
.
(Nikiona ninahangaika sana kimaisha, sifanikiwi, ninatakiwa
nirudi chini nianze kuisoma Biblia usiku na mchana , kama jinsi Yoshua 1:8 inavyo sema , nirahisi
nikafahamu wapi niliko teleza au kukosea; kwasababu Biblia inanifahamu hatakama
ninaisoma, ndio maana inauwezo wa kunielezea mimi nilivyo kiroho vilevile
kimwili).
Kusoma Biblia kunaimarisha imani ya mkristo kwenda sambamba
na misingi ya Yesu Kristo, kwasababu kwenye kusoma Biblia ndipo tunapo ifahamu kweli halisi ya Mungu ni ipi.
Msemo:
Kuifahamu kweli nusu kunamadhara makubwa kuliko uongo mkamilifu, yaani nibora
mtu akakunyima chakula kuliko
kukuonjesha chakula akakuacha bado
unanjaa.
Maisha bila msaada wa kiroho hayaendi ; mwanadamu bila Neno
la Mungu ni sawa na kipofu anyetembea katika njia yenye mashimo, hawezi kufika
safari yake akiwa salama
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni