SUNDAY SERVICE @ KAPERNAUM CHURCH
11TH MAY 2014 by Bab G power
TODAY’S MASSAGE :
WOKOVU
- · Wokovu ni Neno lenye tafsiri zaidi ya moja.
A :Wokovu ni upendo wa Mungu kwa Wanadamu.
B: Wokovu ni Yesu Kristo.
C: Wokovu ni Imani, ndio maana Biblia imefunua hili wazi katika kiabu
cha 1petro1:5.
- · Imani iliyo ndani ya wokovu wa Yesu Kristo ni imani iliyo hai yenye uwezo wa kuleta mabadiliko.
- · Wokovu ndio njia sahihi itakayo nifanya mimi ni uishi ufalme wa Mungu.
- · Neno kuishi ufalme wa Mungu ni jambo ambalo halina mwisho, ni sawa na kusema uzima wa milele
- · Wokovu ni taasisi iliyoanzishwa na Utatu Mtakatifu yaani Mungu mwenyewe,ili kuleta ukombozi wa kweli kwa mwanadamu anayeishi katika mwili wa damu na nyama, ndio maana wokovu au kuokoka ni jambo linalo fanyika chini ya jua tu peke yake,kwa maana zaidi wokovu uliletwa kwetu kututoa katika utumwa wa dhambi,ndio maana Wokovu ni tendo linalo fanyikia chini ya jua, baada ya kifo hakuna Wokovu.
MSEMO
(Nivigumu kumshawishi mtu kukubaliana na wokovu nilio nao kama mimi sijawa
mfano hai kwake).
- · Yesu Kristo ndiye muasisi na mwanzilishi wa wokovu, vilevile ndiye aliye jitoa kuwa sadaka ya ukombozi kwa wanadamu wanao ishi katika mwili, ndio maana Mungu akampa heshima ya kila amwaminiye Yesu Kristo atauishi uzima wa milele, ndio maana Biblia ikafunua wazi kila mwenye sikio na asikie Wafilipi 4:8-11
- · Yesu Kristo ni Jina ambalo limeleta ukombozi kwa kila anaye liamini Neno la Mungu.
NAMNA YA KUPATA WOKOVU
- · Wokovu uliokuja kwetu kwa njia ya Yesu Kristo unapatikana kwa njia kuu mbili:-
A:Kumkiri Yesu Kristo kwa kinywa
changu kuwa ni Bwana.
B:Kumuamini Yesu Kristo kwa
moyo wangu kwamba Mungu alimfufua katika wafu, na jambo hili
maandiko matakatifu
yamelifunua kwa undani zaidi kama ilivyo andikwa katika Warumi 10:9,10
- · Warumi 10:9-10 ni picha wazi baada ya mtu kupata wokovu tayari ,mtu huyo ni sehemu ya Utatu mtakatifu, huvalishwa mamlaka katika kinywa vilevile hupewa nguvu ya imani katika moyo wake, na vitu hivi huimarika zaidi ndani ya mkristo anaye muamini Yesu kristo, kutokana na mtu huyo anavyo ongeza maarifa ya Neno la Mungu katika moyo wake.
·
(Wokovu
ni agano la kweli kati ya mtu na Yesu Kristo,ndio maana mtu ambaye ameingia
katika agano hili, inatakiwa aishi katika maisha matakatifu kama aliyo ishi
Yesu Kristo alivyo kuwa katika mwili, ndio maana Biblia ikafunua wazi kabisa
katika 1petro2:21-25)………….ujumbe utaendelea wiki ijayo
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni