- Dhambi ni uasi, vilevile kila lisilo la haki ni dhambi
1Yohana5:17a
- Nikitaka kuishinda dhambi inatakiwa niruhusu moyo wangu kufunguka juu ya Neno la Mungu,yaani kuamani kujufunza Neno la Mungu(Biblia).
- (Dhambi haina heshima, vilevile haina aibu)
- (Nikiona ninafanya kitu kilicho kinyume na maandiko nijue imani yangu imepunguka, kwahiyo hapo inatakiwa nijapange upya ili hali hiyo isiendelee)
- Dhambi inatabia moja; kumnyima mwamini hamu ya kusoma Neno la Mungu(Biblia),kwasababu Biblia imefunua kila aina na mbinu zote za shetani anazo zitumia kudhoofisha maisha ya imani za wakristo wanaao mtegemea Yesu kristo.
- Nikisoma Biblia inanipa ufahamu wa kugundua dhambi iliyo jificha ndani mwangu, kwahiyo nirahisi kuikemea na ikaondoka
- (Kama sisomi Biblia nivigumu mimi kujitambua kama niko salama kwenye uwepo wa Mungu)
- (Neno la Mungu ndilo linalo haribu nguvu ya dhambi ndanin ya maisha ya mwamini)
- Ili niweze kushinda dhambi iliyoko ndani mwangu inatakiwa niwe na ukaribu sana na Neno la Mungu, ili Roho mtakatifu anipe msaaada wa kushinda katika mazingira ya rohoni.
- Dhambi huharibu mahusiano ya mtu na Mungu, vilevile huadhiri sana nguvu za Mungu zilizoko juu ya mtu, juu ya hili inatakiwa niwe makini nalo sana.
- Wote tunafahamu dhambi ni kitu kisicho pendeza kwenye uso wa Mungu.
- swali : Kwanini ninatenda dhambi?
- jibu: Nikwasababu mimi mwenyewe sijaamua kutoa utayari kwa neno la Mungu kuielimisha roho yangu ikamjua Mungu.
- Kama jinsi mwanafunzi anavyo tamani kufaulu mtihani ndivyo inavyo takiwa kwa mkristo mwamini kutamani kuishinda dhambi, na hii inategemea bidii ya mtu binafsi vilevile na kutambua udhamani wa Mungu aliye kuokoa.
- Mtu anayeishi na Roho mtakatifu anauwezo mkubwa wa kuishinda dhambi , kwasababu Roho mtakatifu ni nguvu ya Mungu.
- (Nikiona kuwa dhambi inanishinda kuishinda hiyo ni picha wazi kwamba mahusiano yangu na Roho mtakatifu sio mazuri).
- Ufahamu mdogo wa rohoni ndio unao sababisha nikose nguvu ya kushinda dhambi.
- (Mkristo mwenye ufahamu mdogo wa rohoni huwa hakubali maonyo yaani akionywa huona anadhalilishwa).Juu ya hili Biblia imesisitiza 1Timotheo 5:20
- Kunatabia zingine zisipo kemewa hadharani huwa haziondoki kwa mtu.
- Maombi ndio silaha itakayo dhoofisha nguvu ya dhambi ndani mwangu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni