20-07-2014
NAITAMANI SANA KARAMA YA UVUMILIVU.
Katika
ujumbe wa leo kuna maneno makuu matatu yaliyo ubeba ujumbe, kabla ya kuendelea
,inatakiwa nipate ufafanuzi wa maneno haya ,ili ufahamu wangu upate upeo wa
kuelewa yatakayozaliwa katika ujumbe wa leo
.
Neno la kwanza
ni KUTAMANI
Neno la pili
ni KARAMA
Neno laa
tatu ni UVUMILIVU
UFAFANUZI
WA NENO LA KWANZA: KUTAMANI
Kutamani ni
hali fulani inayo andaa maandalizi ya jambo fulani kuthibitika, kwa lugha
nyingine kutamani ni kunia ndani ya moyo, na inafahamika wazi jambo ambalo mtu
amelinia ndani ya moyo wake nilazima
atalitenda tu.
UFAFANUZI
WA NENO KARAMA
Karama ni
zawadi au ni kipawa anacho kiachilia Mungu juu ya mtu, kwa lugha nyingine karama
ni Neema inayo toka kwa Mungu na kuyavaa
maisha ya mtu bila kutazama mazingira ya huyo mtu yalivyo.
TAFSIRI
YA NENO UVUMILIVU
Uvumilivu ni
hali fulani ya kungojea au kusubiria
vilevile ni subira.
Uvumilivu ni
karama yenye msingi wa Imani kubwa ndani yake.
Imani za
wakristo waamini zimejeruhika kwasababu ya kukosa hali ya uvumilivu katika maisha
yao, hii ni picha wazi mtu wa aina hii hawezi kumcha Mungu katika roho na kweli.
Mkristo
aliyekosa hali ya uvumilivu hata kuabudu kwake sio sahihi, kwasababu uvumilivu
ni tendo la Imani, vilevile jambo hili Mungu aliliweka wazi hata kimaandiko
Mathayo 24:9-13
(Msingi
wamaisha yangu ya ushindi upo ndani ya tendo la uvumilivu)
Nitabarikiwa
kulingana na kiwango cha Imani yangu
inavyo kua, ili mfanikio yakija yasije yakanitoa nje ya uwepo wa Mungu.
Mwamini akikosa
uvumilivu ndani ya moyo wake hawezi
kutoa maamuzi sahihi katika kile ambacho anakinia kukifanya ,bali atakuwa mtu
anaye jikatisha tamaa mwenyewe , ndiomaana
Biblia jambo hili imelifunua pia kwa undani
Warumi 14:23
Mkristo
aliyekosa uvumilivu kamwe hawezi fanikiwa katika maisha yake yote atakuwa ni
mtu anayeishi kwa taabu mwanzo wa maisha yake mpaka mwisho wa safari yake,hapa
inabidi nifahamu nililokusudiwa na Mungu kulipitia nitalipitia tu ili maandiko yatimizwe katika maisha yangu.
Uvumulivu niliona
mimi ndio unao andaa historia ya mafanikio kwa kizazi changu kinacho kuja nyuma
yangu, juu ya hili inategemea kama nimekuwa mvumilivu katika kusubiri baraka za
Mungu pamoja na hukumu zake,kizazi changu mimi hakitatoka katika misingi hiyo
kamwe ,zaidi kitakuwa ni kizazi chenye kutoa msaada kwa wengine ‘‘ee Mungu nisaidie’’.
Nikiwa
mwamini niliyekosa hali ya uvumilivu kizazi changu nitakiandalia hali ya
kushindwa.
Haitakiwi
niangalie mazingira ninayoyapitia hata kama yana maumivu kiasi gani bali
inatakiwa nivumilie ili niendane sambamba na Baraka za Mungu alizoziahidi
kupitia maandiko Matakatifu,hata Biblia kuna kitu imegusia katika
Waebrania 11:8-10.
Mkristo
yoyote ambaye hajatambua makusudi ya Mungu katika maisha yake hawezi kuwa
mvumilivu, na hii inasababishwa na upofu wa kiroho alio nao makristo huyo.
Mimi niliye
okoka inatakiwa nifuate nyayo za Yesu Kristo kwa asilimia zote,kwasababu Yesu
Kristo hakushindwa katika mazingira yote ingawa alijaribiwa na kupata
maumivu,kwasababu alikuwa ameuvaa mwili wa damu na nyama,hili jambo ni sahihi
kabisa,ndiyo maana hata katika Zaburi
23:4 inathibitisha.
(Haitakiwi
niogope changamoto yoyote ninayoipitia ,kwasababu hapo ndipo ulipo mpenyo wa Baraka
zangu,cha msingi ni kuwa mvumilivu).
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni