Jumatatu, 5 Mei 2014

Jumapili 4-05-2014; UKUAJI WA IMANI SEHEMU YA PILI by pastor Bab G Power



       
   RIVER OF HEALING MINISTRY
(Kapernaum church by pastor babg power)

                    UJUMBE WA LEO TAREHE 04-05-2014

                                       
             UKUAJI WA IMANI SEHEMU YA 2
KIPENGELE A:    MAZINGIRA YA UKUAJI WA IMANI

  • ·         Ninafahamu wazi kwamba Imani ni kitu cha rohoni , yaani ni kitu ambacho hakina umbo kamili.

  • ·         Mazingira ya kukua kiimani iantakiwa nitafute ushirika na Neno la Mungu.

  • ·         Imani za wakristo wengi waamini zimedumaa kwasababu kuu mbili

             A:Kukwepa kusoma biblia
                   B:Kukwepa mafundisho ya Neno la MUNGU, ndio maana wakristo wengi waamini       
                    wamelemea katika sehemu moja tu, kuombewa.

  • ·         Na watu wa namna hii wameanguka katika mtego mbaya wa kishetani , kivipi

                 A. kulinganisha huduma
                B. Kufanya utafiti
                C.Kusema watumishi wa Mungu,ndio maana biblia ikatoa tahadhari kuu juu ya       
                watu kama hao, kama ilivyo andikwa katika    Tito 1:16

       (Nivigumu kupata mtiririko wa Roho mtakatifu wakati wa kuomba, ikiwa ndani mwangu sina               ufahamu sawasawa wa Neno la Mungu(Biblia)).


  • ·         Imani ya mkristo ikipata ufahamu wa Neno la Mungu huwa hai,huo huwa ndio mwanzo wa imani ya mkristo huyo kuumba miujiza,kuumba baraka, humpa ulinzi dhidi ya roho za uvamizi,juu ya hili jambo kitabu cha 1petro1:5 imefafanua wazi.

  • ·         Msingi wa imani ya Neno la Mungu ukiiwepo ndani mwangu kikamilifu kila kitu kitafunguka wazi katika maisha yangu

  • ·         Ili niwezekufanikiwa katika mazingira ya ukuaji wa  imani yangu inatakiwa nifanye mambo yafuatayo, kibiblia mambo haya huitwa mazoezi ya kiroho

              A: Usomaji wa biblia  marakwamara, juu ya hili kwa wakati mwingine inatakiwa
                   nijilazimishe.
              B:Ufungaji wa mara kwa mara.
              C:Uombaji na kukesha.
·          

 



Hakuna maoni: