Jumatatu, 28 Aprili 2014

Ibada ya Jumapili ( 27 April 2014 ) - NAMNA YA KUJIENDELEZA KIROHO. By Pastor John

  •  
  • Ukuaji wa kiroho katika maisha ya mwamini ni jambo ambalo huchukua muda, ndio maana mwamini anasisitizwa kujitahidi kutafuta mwendelezo wa kuilisha roho yake Neno la Mungu. 
  • Katika jamii ya waaminio imekuwa ni jambo imekuwa ni jambo la kawaida kwa watu waliowengi kujitahidi kuendeleza akili zao kuliko roho zao
  • Nini Maana ya kuendeleza akili?
    •   Maana ya kuendeleza akili ni mtu kwenda shule kujifunza mambo ambayo yatamsaidia katika maisha yake ya kibinadamu yaani ya damu na nyama
    • ( Kuendeleza akili sio jambo baya  mbele za Mungu )
  • Nini  Maana ya kuendeleza roho?
    • Maana ya kuendeleza roho ni mtu kuamua kutilia mkazo mafundisho ya neno la Mungu. 
  • Mtu anapo endeleza roho yake anapata hali ya mawasiliano na Mungu, ambayo itamsaidia mtu huyo kumuona Mungu anayeonekana katika ulimwengu wa kiroho.
  • Katika Yohana 4:24, Mungu mwenyewe anatutaka sisi waamini kumuabudu katika roho na kweli, yaani katika roho ni katika Imani, katika kweli ni katika Neno Lake.
  • Neno Mungu lina maana gani au Mungu nini?
    • Mungu ni Roho ya milele ambayo haina umbo kama sisi wanadamu ila hufanya kazi vilevile hujidhihirisha katika umbo la kibinadamu.
  • Kwa hiyo mwamini anatakiwa kuendeleza akili zake vilevile kuendeleza roho yake ili maono yake, mipango yake, na yote anayotarajia yaweze kutimia.
  • Katika kitabu cha Mithali 16:1-2, vilevile unatupa picha halisi ya namna ambavyo natakiwa kutimiza wajibu wangu mbele za Mungu.
  • Yesu mwenyewe wakati akiwepo duniani katika mwili wa damu na nyama aliwaeleza wale wayahudi waliomwamini umuhimu wa kujiendeleza kiroho yaani kutafuta zaidi kulifahamu neno la Mungu.
  • Unaposoma Yahana 8:31 na kuendelea, unapata picha halisi ya hili.
  • ( Mwamini asipokubali tabia yake ikabadilishwa na Kweli ya Mungu hawezi kukua kiroho kamwe, kwa sababu Tabia ya mtu ni jumla ya mazoea yake. )
    • Mfano : Uchelewaji wa kanisani, Utoaji wa sadaka, kunong'ona ndani ya kanisa, na mtu mmoja akiamka na wote wanamtolea macho, na mambo mengine mengi yanayo fanana na hayo.
  • Kweli ya Mungu ndiyo inayo muweka mtu huru, lakini itaonekana kana kwamba inamhuzunisha mtu au inamdhalilisha mtu kumbe sivyo
  • Kweli ya Kristo inapoingia ndani ya moyo wa mtu huchimbua mambo mbalimbali na vilevile huvuruga mapenzi ya mwanadamu au makusudi ya moyo wa mwanadamu ili kuleta hali ya mapenzi ya Mungu au makusudi ya Mungu ndani ya moyo wa mtu ambayo itamsaidia mtu huyo kusimama vizuri katika mipango ya Mungu.
  • Mtume Paulo alipotembelea Rumi alikutana na mambo kama haya watu wakiwa na hali ya kutumia akili nyingi zaidi katika kumtafuta Mungu.
  • (Warumi 10:1-4) 
  • Ufafanuzi kuhusu Warumi 10:1-4.
    • Maana ya Mstari wa kwanza. ( Warumi 10:1) .  Mtume Paulo anaonyesha nia ya moyo wake ya kumuomba Mungu watu aliokutana nao waifahamu kweli, maana alifahamu katika kuifahamu kweli kutaleta msaada kamili wa Wokovu kwao. 
    •  Maana ya Mstari wa pili. ( Warumi 10:2 ). Mtume Paulo aliweza kudhibitisha yeye mwenyewe juhudi waliyonayo juu ya Mungu, haikujengwa juu ya ujuzi wa kweli.
    • Nini maana ya neno maarifa?  Maana ya neno maarifa ni hali fulani ya ufahamu iliyozidi ufahamu wa kawaida wa kibinadamu, hali hiyo inaletwa kwa mtu kwa msaada wa Roho Mtakatifu, ina maana ni kipawa maalumu cha Kimungu juu ya mtu.
    • Maana ya Mstari wa tatu. ( Warumi 10:3 ). Hawakufahamu jinsi Mungu anavyo fanya watu wawe waadilifu na wamejaribu kuanzisha mitindo yao wenyewe kwa hiyo hawakukubali njia hiyo ya Mungu ya kuwafanya wawe waadilifu.
    • Maana ya Mstari wa nne. ( Warumi 10:4 ). Maana ya mstari wa nne ni kwamba kuja kwa Yesu Kristo kumeweka kikomo juu ya sheria yaani kuhesabiwa kwa matendo ya kimwili tu. 
    • Biblia inapozungumzia sheria inamaana ya kuzungumzia torati, torati ilitolewa kwa mkono wa Musa kweli na neema zilitolewa na Yesu Kristo, ndio maana Yesu aliulizwa swali umekuja kutengua Torati au Sheria za Musa?, Yeye aliwajibu Nimekuja kutimiliza yote au kukamilisha yote. 
    • Mfano mzuri wa maswali alioulizwa Yesu kuhusiana na Torati au Sheria za Musa unapatikana katika kitabu cha Mathayo 22:15.

Maoni 2 :

Unknown alisema ...

Nimefurahishwa sana na hii blog,Songa mbele kazi ni nzuri sana na sisi tuko pamoja katika kazi ya Bwana.Amen!

Unknown alisema ...

Amen!Mungu akubariki